Viongozi wa kidini wa Cabo Delgrado wakutana kuimairisha amani
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Ni masuala kumi na tano yaliyomo kwenye mpango wa kuweza kujenga amani katika wilaya ya Cabo Delgrado na kwa ajili ya kufanya kazi pamoja katika mazungumzo, na katika mkutano pamoja na tofauti zao walizo nazo. Ndiyo waliyoandika kwenye Waraka wao kwa kuongozwa na Hati ya Udugu wa Kibinadamu, uliotiwa saini huko Abu Dhabi 2019, kwa ajili ya Amani ulimwenguni ambayo imewaongoza viongozi hawa wa kidini wa wilaya ya Cabo Delgado Pemba nchini Msumbiji, mbapo waliunganika kuanzia tarehe 14-15 na 22 Desemba 2021. Lengo kwa hakika ya Semina yao ni kutaka kutafakari kwa kina juu ya Dini ambayo inaweza kuwa sehemu muhimu ya kuleta suluhisho la mgogoro wa Cabo Delgado.
Kiwango cha juu cha kutojua kusoma na kuandika na ukosefu wa usawa kijamii
Viongozi hao wanakumbusha kuwa wilaya hiyo niakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kibinadamu unaosababishwa na vurugu za kigaidi, ambapo maendeleo yanawekwa chini na hatua za kuzuia janga la Covid-19 na sababu zingine za kutisha, kama vile kukosekana kwa usawa wa kijamii, kiwango cha juu cha kutojua kusoma na kuandika, mzozo wa maadili ya kimaadili na migawanyiko ya kikabila na kidini ambayo inatishia muktadha wa sasa na kuishi pamoja kijamii, ambayo inakiuka hadhi ya mwanadamu.
Inahitajika umoja wa nguvu kukabiliana na mipasuko na kukataa vitendo vya kigaidi
Waraka huo wa pamoja aidha unasisitiza juu ya umoja wenye nguvu katika kukabiliana na tishio lolote la mpasuko na kukataa kwa pamoja vitendo vya kigaidi lakini pia dhamira ya kutembea bega kwa bega kuelekea amani na udugu. Dini, wanasisitizwa, sio sababu ya migogoro na hasa wakisisitizia juu ya Uislamu, dini iliyoathiriwa zaidi na ubaguzi. Kwa maana hiyo wanabainisha kwamba dini inalenga kujenga furaha, upatanisho na amani katika jamii na, kwa sababu hiyo, wanakataa na kujitenga na vitendo na watu wanaopotosha mafundisho ya dini ili kuhalalisha aina yoyote ya vurugu. Hivyo kujitoa kwa ajili ya mazungumzo na madhehebu mengine, kushinda kutoaminiana na kukuza maelewano kwa sababu dini zote ni sehemu ya mpango wa Mungu Mkuu, na hakuna kiongozi wa kweli wa kidini au nabii aliyewahi kufundisha vurugu.
Wasi wasi wa vijana wanaongukia mitego ya kiitikadi
Mazungumzo, kukutana na kutambuana ni misingi ambayo imependekezwa kwa upya ili kuunda jamii jumuishi. Jitihada na ahadi yao pia ni kufanya mijadala na makongamano ili kusaidia watu kukua na sio tu kwa na mtazamo wa kidini lakini pia katika taaluma nyingine ili kuelewa vyema ukweli unaoishi. Katika mioyo ya viongozi wa kidini zaidi ni kuhusu vijana wote wanaoangukia katika wavu wa itikadi kali na vurugu, kwa lengo la kuwasindikiza, kuwarekebisha kwa shughuli muhimu na inayodai kisaikolojia na kiroh". Jitihada za kudumu ni ile ya kusali kwa pamoja kwa ajili ya amani ya kudumu daima kushirikiana na serikali, taasisi na mashirika ambayo yamejitolea kwa amani katika wilaya ya Cabo Delgado.