Tafuta

Open Doors World Watch List 2022 Open Doors World Watch List 2022 

Open Doors World Watch List 2022:Nchi 50 za juu ambazo Wakristo wanateswa

Imetolewa "The Open Doors World Watch 2022",’Orodha ya Kutazama Duniani kwa Milango Huria’,ambao hukusanya kila mwaka na kuorodhesha nchi 50 za juu zaidi ulimwenguni ambazo Wakristo wanakabiliwa na mateso mabaya zaidi kwa ajili ya imani yao katika Yesu.Orodha hii inatokana na maelezo ya kina kutoka kwa wafanyakazi wa Open Doors,katika zaidi ya nchi 65,pamoja na wataalam huria.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mateso ya Kikristo ni uadui wowote, unaopatikana kutoka kwa ulimwengu, kwa sababu ya utambulisho wa mtu na Yesu Kristo. Hii inaweza kujumuisha hisia za uadui, mitazamo, maneno na vitendo. Lakini Biblia inamaanisha nini kwa neno “mateso”? Katika Injili ya Mathayo 5:10-12, Yesu anasema katika Heri za Mlimani kwamba mateso ni baraka. Sio moja ambayo wengi wetu tunatamani! Yote hayo ni katika muktadha wa orodha ilitolewa na  “The Open Doors World Watch List 2022”, yaani “Orodha ya Kutazama Duniani kwa Milango Huria” ambao hukusanyaa kila mwaka na kuorodhesha nchi 50  zaidi ulimwenguni ambazo Wakristo wanakabiliwa na mateso mabaya zaidi kwa ajili ya imani yao katika Yesu. Orodha hiyo inatokana na maelezo ya kina kutoka kwa wafanyakazi wa ‘Open Doors’, katika zaidi ya nchi 65, pamoja na wataalam huria.

Heri za mlimani

Katika maelezo zaidi kuhusu mateso hayo, Yesu pia anafafanua neno kwa ajili yetu katika Injili ya Luka 6:22 akitumia vitenzi vine na kusema, “Heri ninyi watu watakapowachukia, watakapowatenga na kuwatukana na kulikataa jina lenu kuwa ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.” Kumbuka kwamba ni Yesu yumo ndani yako ambaye ndiye sababu ya, na shabaha ya mateso. Katika somo la Warumi 8:17, mtume Paulo anatuambia, kuwa: “Basi ikiwa sisi tu watoto, basi tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo, ikiwa tunashiriki mateso yake ili pia tupate kushiriki naye utukufu.” Kwa maana  hiyo, tunaposhiriki mateso ya Yesu (chuki, kutengwa, matusi, na kukataliwa) tunakuwa warithi ambao pia watashiriki utukufu wake. Vitenzi vinne hapo juu vinaweza kupatikana katika viwango tofauti vya kina.

Ukweli ni kwamba kuna ushiriki kimwili wa Kristo katika mateso 

Kwa bahati mbaya,  lakini Wakristo wengi leo, wanafanya kazi chini ya dhana kwamba mateso ni sehemu ya zamani ya Kanisa. Ukweli ni kwamba kuna washiriki wa mwili wa Kristo ambao kwa sasa wanakabiliwa na mateso makali na vikwazo kwa sababu ya imani yao katika Yesu Kristo. Kila siku ya kila mwaka, na katika kila bara, wanaume na wanawake hukabiliana na mateso kwa sababu ya imani yao katika Yesu Kristo. 

Baadhi ya mateso kifungo, kuteka nyara, uharibifu wa mali, unyanyasaji kimwili

Hapa kuna mifano michache ya aina za mateso ambayo Wakristo wanakumbana nayo leo hii kama vile: Unyanyasaji wa kimwili na matusi, kifungo, utekaji nyara, rushwa na ufisadi, uhamisho, uharibifu wa mali, faini, mateso na mauaji.

Orodha ya nchi 5 za juu ,ambapo wakristo wanapitia mateso mengi

Nchi 50 zilizo za juu  ambapo Wakristo hupitia mateso mengi zaidi zilizofanyiwa na chunguzi na “The Open Doors World Watch” ni :Afghanistan, North Korea, Somalia, Libya, Yemen, Eritrea, Nigeria, Pakistan, Iran, India, Saudi Arabia, Myanmar, Sudan, Iraq, Siria,Maldives, China, Qatar, Vietnam, Egypt, Uzbekistan, Algeria, Mauritania, Mali, Turkmenistan, Laos, Morocco, Indonesia, Bangladesh, Colombia, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Burkina Faso,Niger, Bhutan,Tunisia, Oman, Cuba, Ethiopia, Jordan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji, Uturuki, Mexico,Cameroon, Tajikistan, Brunei, Kazakhstan, Nepal,Kuwait, na Malaysia

19 January 2022, 16:18