Peru:Kutembea kuelekea huduma ya kilei ya Katekista
Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Tume ya Maaskofu kwa ajili ya Katekesi na Uchungaji wa Kibiblia la Baraza la Maaskofu nchini Peru, wametangaza kufanya Juma la Mafunzo kwa ajili ya Makatekista kwa mwaka huu, kuanzia tarehe 7 -11 Februaria 2022. Toleo hili jipya litafanyika kwa njia ya mtandao, kutokana na hali halisi inayoendelea ya janga la uviko-19, kwa kuongozwa na kauli mbiu: “Kutembea kuelekea huduma ya Walei ya Katekista”.
Kusasisha mafunzo kwa makateksita na wahudumu wa kichungaji
Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la habari za kimisionari Fides, linasema kwamba Juma la Katekesi ni nafasi moja ya kufanya mafunzo kwa ajili ya kusasisha kwa makatekista, wahudumu wa kichungaji, wahusika wa maparokia, wahuduma wa mafunzo ya kibiblia na liturujia harakati za kitume, vyama vya kitume kwa lengo la kutafakari kuhusu huduma ya kilei ya Katekista, ili kuweza kuwa hai katika Kanisa la Peru na kuenzi kile kilichoanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko mnamo tarehe 11 Mei 2021 , alichapicha Barua Binafsi “Motu Proprio” ambayo inajulikana “Antiquum ministerium” yaani “Huduma Kale”. Hii ni wazi kwamba katika migogoro na changamoto za kila siku za Uinjilishaji katka ulimwengu mambo leo, unahitaji kupyaishwa kwa huduma hii ambayo kama asemavyo si huduma mpya kabisa kwa watu wa Mungu maana huduma ya makekista imekuwepo tangu zamani na hawa wamekuwa siku zote mashuhuda wa imani.
Watoa wada watakuwa ni wa kimataifa 7-11 Januari 2022
Mwaka huu, tukio hili nchini Peru litawaona washiriki wa kutoa mada wa kimataifa. Kwa mujibu wa ratiba ya Juma la mafunzo litaanza siku ya Jumatatu tarehe 7 Februari, kwa kuanza na utangulizi wa sala na jukwaa litakaloongoza na mada: “Kanisa leo hii”. Zitafuata kazi za makundi. Ratiba hiyo hiyo itaendelezwa kwa siku zinazofuata, kwa kutoa mada kuhusu: “ Huduma ya walei na huduma ya walei Makatekista; Utambulisho na wito wa Katekista; Kuwa Katekista katika udugu; Katekista; Mhudumu: Mtume mmisionari kwa ajili ya Kanisa linalotoka nje. Juma la mafunzo litahitimishwa kwa adhimsho la Neno la Mungu na kuwatuma mnamo tarehe Ijumaa 11 Februari 2022.