Tafuta

Ziara ya Kitume ya Patriaki wa Kilatino Pizzaballa huko Jordan. Ziara ya Kitume ya Patriaki wa Kilatino Pizzaballa huko Jordan. 

Nchi Takatifu:Mazungumzo ni changamoto inayoendelea

Patriaki Pizzaballa wa Yerusalema amesema mazungumzo ni changamoto inayoendelea.Amesema hayo kufuatia na fursa ya Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo,kuanzia 18 Januari na itahitimishwa tarehe 25 Januari,sambamba na Siku Kuu ya Mtakatifu Paulo, lakini katika makanisa ya Kirothodox na wengine ya kiarmeni Juma linaanza tarehe 22 Januari.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kuanzia tarehe 18 hadi 25 Januari ni Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo. Katika fursa hii, Patriaki wa kilatino wa Yerusalemu, Pierbattista Pizzaballa, amezungumzia juu ya uekumene wa maisha ya wakristo wa Nchi Takatifu na shauku yao ya umoja. Katika Barua yake aliyoiandika kwa ajili ya Wakuu wa Makanisa ya Yerusalemu, amewalezea jinsi ambavyo wanayo shauku ya kutaka kusheherekea Sinodi kwa pamoja, kuishi pamoja, na wanataka  kuonana wakiwa pamoja. Mwaka huu, katika Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo, ambalo limeongozwa na Kauli Mbiu:“Tuliona Nyota ikichomoza kutoka Mashariki na tumekuja kumwabudu (Mt 2,2)”  na ambayo imeandaliwa na Baraza la Makanisa la Mashariki ya Kati , Patraikia anaongeza kuwa ni katika nchi ambayo imegeuka  kwa mara nyingine tena kuwa ya utunzaji wa uekumene. Hapo ni eneo ambalo linaishi kati ya mivutano na migorogoro iliyojitokeza na vita vinavyoendelea kushinda tofauti ambazo zinagawa makanisa kwa wastani na ni changamoto za kila siku.

Utofauti kati ya makanisa 

Masuala yanayotokana na utofauti kati ya Makanisa mbali mbali Patriaki ameandika kuwa yalepelekea matokeo ya kufanya mazoezi katika makanisa, ambapo si tu katika  sghuli za kichungaji lakini pia inatosha kufikiria  hata kalenda yao. Kwa sababu yapo makanisa ambayo yanafuata Kalenda ya litutujia ya  Gregoriani na mengine ya Kijuliani. Kutokana na hiyo, ndipo unaweza kuona kwamba Yerusalemu , Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo litaanza tarehe 22 Januari, kutokana na kwamba siku kuu za Kuzaliwa kwa Bwana imehitimishwa katika Ibada ya Kiarmenia tarehe 18 Januari 2022. Hata hivyo Patriaki Pizzaballa baada ya kufika huko Jordan mahali ambapo yupo kwenye ziara ya kichungaji, amezungumzia juu ya shauku ya watu wa Kikristo ya kutaka kuishi kwa amani, maelewano na kuwa na uhusiano mwema. Katika neno moja tunaweza kusema ni kuishi pamoja.

 Kuhusiana na kushirikishana

Hata hivyo kwa kuelezea amesema Nchi Takatifu na Yerusalemu ni maabara ya Uekumene ambayo ni hali halisi waliyoishi katika karne za waamini wao, familia zao za kikristo ambazo asilimia 90 za kesi ni mchanganyiko kati ya Wakristo na Waorothodox. Kuishi kwa pamoja, kunawalazimu kuhusiana, kushirikiana  na mmoja na mwingine daima na kila siku.  Simulizi ya kiekumene katika Nchi Takatifu kwa mujibu wa Patriaki Pizzaballa amesema haiwezi kuishia katika picha za mivutano za  Kaburi Takatifu, kati ya madhehebu tofauti, ambayo huwa wanaonesha kwenye Televisheni, kwa sababu wao hawaoneshi sababu ya kitu kilicho halisi cha Nchi Takatifu na ambacho kinyume chake ni hari na shauku ya umoja wa Wakristo mahalia. Kama mchungaji wa Kanisa hilo alisisitiza kwamba hayo ndiyo maombi ambayo wanaombwa  na  nguvu za waamini wao. Kila mahali anapokwenda iwe shuleni, makanisani na maparokia wanaelezea juu ya   shauku waliyo mayo kwa kusema kwamba wanataka kusheherekea pamoja, kukaa pamoja na  kuishi pamoja.

Kuishi pamoja

Licha ya hayo lakini Patriaki Pizzaballa amekubali kuwa kuna ugumu fulani kwa upande wa idadi ya watu kuelekea taasisi za kikanisa ambazo, kwa upande mwingine, wanakumbana na vizzingiti. Kinacholeta uzito ni historia, masuala ya kiliturujia, sheria, makanisa ambayo kwa waamini wengi yanasikika kuwa hayaeleweki. Wakristo lakini wanataka kuwa pamoja, kuomba pamoja na kuishi kama jumuiya moja. Msukumo huo unatoka chini na unaosukuma taasisi hata zile zenye kinzani zaidi kama Wagiriki wa Korthodox kuafikiana, amesisitiza. Ikiwa katika ngazi ya kiliturujia na kikanisa, umoja unahitaji muda kidogo zaidi, lakini kwao umoja wa kijamii tayari ni ukweli halisi unaojionesha. Kwa maelezo ya Patriaki Pizzaballa amesema: “Kama Makanisa sote tunafahamu kwamba, licha ya tofauti fulani, ni lazima tuzungumze kwa sauti moja kutoka katika mtazamo wa kisiasa na kijamii kuhusu hali halisi kwa ujumla. Hii imekuwa dhahiri zaidi ya yote katika miaka ya hivi karibuni, kama inavyooneshwa na mfululizo wa matamko ya kawaida juu ya matukio mbalimbali ya ndani”. Patriaki amesema wanajaribu kuifanya karibu kila wakati na kwa kuonesha mfano ni tamko la hivi karibuni ambalo lilitolewa  tarehe 15 Desemba 2021  ambalo Mapatriaki  na wakuu wa Makanisa ya Yerusalemu, walitoa kwa sababu  Wakristo walikuwa walengwa wa kushambuliwa na misimamo mikali ya Kiyahudi.

Uekemene na Ufiadini

Patriaki Pizzaballa pia amezungumzia huu ya uekuemene na ufiadini kwamba kuna ufiadini unaoonekana katika nchi ya Iraq, Siria, na Nchi nyingine ya Mashariki ya kati, tofauti na hali ya Nchi Takatifu na ambayo haitofautishi kati ya makanisa tofauti. Kuawa wa Kristo inawafanya kuwa sawa wao kwa wao mbele ya watesi wao . Pia kuna aina tofauti ya kifo cha kishahidi, kama ile ya kuwa idadi ndogo katika 'bahari' ya Kiyahudi na Kiislamu, kulingana na mahali. Hii inawalazimisha kila wakati kuthamanisha kile walicho wao na hii pia inawaunganisha kati ya Wakristo, alisisitiza Patriaki  Pizzaballa. Ni changamoto ya mara kwa mara ambayo ina kitu cha kuwafundisha katika nchi za Magharibi pia, ambao wanataka kuona matokeo ya matendo yao mara moja. Hapo Yerusalemu, hata hivyo, mtu hujifunza kuishi na kutoa ushauri na maana ya kusubiri. Inabidi wafikie nyakati za wengine ambazo kamwe sawa na za kwao. Mazungumzo ya kiekumene lazima yakumbuke kipengele hicho ambacho hakiwezi kutenganishwa na kusikiliza. Alisisitiza Patriaki

Sinodi

Patriaki katika kipengele cha mwisho alisema wanasumbiriwa na wakati muafaka kwa ajili ya kusikiliza na ndiyo mchakati wa safari ya Kisinodi  ambapo ametangaza kuchapicha barua yake ya kichungaji inayotarajiwa kutolewa katika Juma lao la “Kuombea Umoja wa Wakristo kuanzia tarehe 22 Januari 2022 katika Nchi Takatifu. Patriaki amesema: “Katika barua nitawataarifu juu ya Sinodi moja yenye mada msingi ambayo itakuwa ni ‘Usikivu’. Tutakuwa na furaha, si tu kwa kujifunza lakini hasa kwa kusikiliza maoni yao kuhusu Sinodi. Kanisa la Kiorthodox lina uzoefu huu mkubwa”.

20 January 2022, 15:31