Tafuta

2022.01.22 Misa ya Mazishi ya Padre Timothy Andulile Mwanjonde wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya Tanzania, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Andrea, huko Subiaco Italia 2022.01.22 Misa ya Mazishi ya Padre Timothy Andulile Mwanjonde wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya Tanzania, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Andrea, huko Subiaco Italia 

Majonzi yatanda kwa Jimbo la Tivoli-Palestrina na Mbeya Tanzania

Padre Timothy Mwanjonde,aliyefariki tarehe 20 Januari 2022 mwenye umri wa miaka 46,mwili unasafirisha kwenda Tanzania 24 Januari. Askofu Parmeggiani wa Jimbo la Tivoli- Palestrina alisema,Marehemu alikuwa mpole,mnyenyekevu na kusifiwa na wanaparokia na mapadre wenzake katika jimbo lake.Misa ilifanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Andrea Mtume,Subiaco.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Askofu Mauro Parmeggiani wa jimbo katoliki la Tivoli na Palestrina, Italia aliongoza misa ya kuaga Marehemu Padre Timothy Andulile Mwanjonde, aliyefariki tarehe 20 Januari 2022 akiwa na umri wa miaka 46, na ambaye alikuwa anatoa huduma ya kichungaji katika jimbo lake kwenye  Parokia ya Mtakatifu Maria Mpalizwa, la Cerreto Laziale, nchini Italia. Misa hiyo lilifanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Andrea Mtume, huko Subiaco na kuudhuriwa na Mapadre wa Jimbo, Mpadre na watawa kutoka Jumuiya ya Watanzania, Roma pamoja na wawakilishi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, viongozi wa serikali mahalia na vikundi vya Vyama Katoliki vya Parokia ya Cerreto Laziale, aliyokuwa anatoa huduma ya kichungaji marehemu. Katika misa hiyo kwa hakika ilijawa simanzi na majonzi makubwa ya kuondokewa na mpendwa Padre Timothy. Askofu Parmeggiani akianza mahubiri yake mara baada ya masomo na Injili aliwakaribisha wote walioudhuria  na zaidi wazo lake liliwandea kwa namna ya pekee, Askofu Mkuu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga, wa Jimbo Kuu la Katoliki la Mbeya, familia yake, ndugu zake na marafiki wa Padre Timothy ikiwa ni pamoja na Mapadre wenzake wa Jimbo Kuu katoliki la Mbeya nchini Tanzania, na ambao walikuwa wanafuatilia liturujia kwa njia ya mtandao.

Misa kwa ajili ya Marehemu Padre Timothy Andulile Manjonde wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya,Tanzania
Misa kwa ajili ya Marehemu Padre Timothy Andulile Manjonde wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya,Tanzania

Askofu Parmeggiani katika mahubiri yake alielezea alivyopata pigo gumu sana la kupokea taarifa ya kifo cha Padre Timothy, hasa kwa jinsi maisha ya ujana wake yalivyokutana na kifo kwa sababu ya ugonjwa uliojitokeza ghafla miezi michache iliyopita, na taratibu katika kufanya vipimo  jinsi ambavyo saratani ya damu haikuwezekana kutibiwa katika Hospitali ya Umberto I mjini Roma, mahali alipokuwa kalazwa hadi Jumatatu asubuhi 17 Januari 2022, alipoitwa kwa simu na Dk. aliyekuwa anamfuatilia katika matibabu  akimjulisha kwa uchungu kuhusu  mtu ambaye  tayari amemzoea hapo kuwa alikuwa mtu mwema na mpole na kwamba hata njia nyingine waliyokuwa wameanzisha kumtibu haikuleta mafanikio, na kwa maana hiyo kilichokuwa kimebaki ni kutafutia sehemu nyingine (Hospice- ahome providing care for the sick or terminally ill) nyumba ya kuweza kumsindikiza katika utunzaji kwenye hatua  yake ya mwisho wa maisha ili hasiteseke sana.

Misa kwa ajili ya Marehemu Padre Timothy Andulile Manjonde wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya,Tanzania
Misa kwa ajili ya Marehemu Padre Timothy Andulile Manjonde wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya,Tanzania

Siku hiyo hiyo kwa bahati nzuri  sehemu ilipatikana kwa haraka katika kituo cha (Italian Hospital Group), Kikundi cha Hospitali ya Italia, kilichopo Guidonia na  hivyo kurudishwa kwenye eneo la Jimbo hilo. Askofu alibitibisha jinsi ambavyo alitegemea si kumpigia simu tu, lakini pia kwenda kumtembelea ili hasijihisi peke yake. Askofu Parmeggiani ameongeza kusema  "Janga lisilosemekana la Uviko ambalo tunapitia", lakini halikuruhusu hata suala hilo. Hiyo ni kwa sababu alikuwa ni Padre mhusika wa kikanisa cha Jengo hilo, Padre Marco Savaresi ambaye pia amemshukuru, aliweza kumsalimia Padre Timothy wakati wa kufika  katika Jengo hilo. Japokuwa Jumanne terehe 18 Januari habari ngumu ikafika baada ya kuitwa na Padre huyo kwa simu kumweleza hasiende kwa Padre Timothy, kwa sababu alikuwa  amekutwa akiwa na virusi vya Uviko na kwa maana hiyo hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kuingia ndani ya chumba chake na hata Padre Marco ilibidi ajitenge kwa ajili ya tahadhari. Jambo hilo lilimwongezea wasi wasi mkubwa, alikiri Askofu. Kifo kwa hakika amesema ni tukio ambalo daima linatia wasiwasi kwa sababu, linavunja uhusiano wa upendo, wa urafiki na ushirikiano. Kifo cha kijana mwenye umri wa miaka 46 kinatia shaka zaidi na zaidi. Lakini unafika hata ule upweke, amesisitiza. Kwa hakika kila mmoja anakufa akiwa peke yake, lakini Askofu amethibitisha jinsi alivyokuwa na utambuzi kwamba wauguzi waliokuwa na wajibu waliweza kuwa wakarimu. Lakini haukukosekana  hata uchungu mkubwa kwa kujua kwamba, Tomothy kijana,  Padre mwema na mpole, aliyesifiwa na wote waliomfahamu na kukutana naye amefariki akiwa peke yake.

Misa kwa ajili ya Marehemu Padre Timothy Andulile Manjonde wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya,Tanzania
Misa kwa ajili ya Marehemu Padre Timothy Andulile Manjonde wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya,Tanzania

Kwa njia ya kifo hicho, alifikiria Yesu haraka.  Na hasa kilio chake cha mahangaiko akiwa juu ya  msalaba na kupendekeza kusoma Injili iliyosikika. Askofu amesema, kilio cha namna hiyo cha kibinadamu ambacho bila shaka kilikuwa ndicho kilio cha Padre Timothy na kama kilivyo cha wengi katika miaka hii kwa sababu  watu wako wanakufa wakiwa peke yao katika hospitali na zaidi kwa ajili ya Padre Timothy, aliyekuwa mbali na nchi yake, na wapendwa wake, na Parokia yake ya Cerreto…  ni kilio kile cha “Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha”. Askofu Permiggiani ameongeza kusema: "hili ni Swali halali, Swali la kibinadamu, Swali linaloeleweka. Linaeleweka hivyo kwamba hata Yesu, Mungu ambaye alipendelea kufanyika mwili, aliinua kwa Baba yake. Swali ambalo lakini Baba alijibu kwa kumfufua katika wafu. Swali ambalo lilipata jibu mara moja na daima katika siku ile ya Pasaka, ambayo kwetu sisi imekuwa sababu ya maisha na matumaini, sababu ya maisha yetu hata kwa kifo chetu na kwamba Injili iliyosomwa kwa hakika ilikuwa inapendekeza hilo: “ Siku ya kwanza ya Juma yaani mwanzo mpya wa Juma baada ya kazi ya uumbaji ulioharibiwa na dhambi na kifo, wanawake walikwenda katika kaburi la Yesu ili wahitimishe ibada ya maziko. Baada ya kuingia katika kaburi walimwona kijana ameketi upande wa kulia, akiwa na mavazi ya kumeta meta na wakaogopa sana. Lakini yeye aliwambia: “Msiwe na hofu! Mnamtafuta Yesu wa Nazareth aliyesulibwa. Hayupo hapa, amefufuka!

Yesu amefufuka ameshinda mauti

Yesu amefufuka, amesisitiza Askofu Parmeggiani kwamba ameshinda mauti na kuhakikisha kuwa wale wote ambao watamwamini yeye watapitia hatima hiyo hiyo. Amefufuka! Ni fumbo la imani yetu. Na hiyo ilikuwa imani ya maisha yote ya Padre Timothy na ndiyo ukweli ambao aliutoa maisha tangu alipokuwa katika Jimbo lake la Mbeya, ambapo mnamo tarehe 5 Julai 2007 katika Parokia ya Kisa, alipata daraja la ukuhani. Ukweli ambao ulitangazwa na upole na tabasamu  kwa miaka 15 ya huduma yake; kuhani mtiifu katika amri ile ambayo alisema Mtume Petro katika Somo la Pili: “Mungu alimfufua Yesu siku ya tatu na anataka kujionesha si kwa watu wote lakini kwa mashuhuda waliochaguliwa na Mungu na sisi ambao tumekula na kunywa na Yeye baada ya ufufuko wake kutoka kwa wafu. Na alituhamuru kutangazia watu na kushuhudia kuwa Yeye ni hakimu wa wazima na wafu, aliyewekwa na Mungu… na kila amwaminiye atapata msamaha wa dhambi kwa njia ya neno lake….”

Askofu akiendelea na mahubiri yake alisisitiza kuwa, Padre Timothy alifanya hivyo, kwani  Yeye aliamini katika Mfufuka! Katika mchakato wa maisha yake alikutana naye katika umakini wa Neno la Mungu, katika sala na katika sakramenti.  Aliamini na kujikabidhi kwa  Mungu wa maisha na wa huruma ambaye alikutana naye kwa njia ya ushuhuda wa wapendwa wake, wa mapadre wake na wa Kanisa lake la Tanzania. Kwa maana hiyo alitangaza Mfufuka kwa njia ya  maisha yake na sasa “tusali ili kila aina ya dhambi iweze kuondolewa na aweze kushiriki utimilifu wa Ufufuko, aweze kukaa katika karamu ya maisha ya milele na kupokea zawadi ya utimilifu wa maisha ya milele waliyo ahidiwa watumishi wema na waaminifu wa Injili. Ni Injili ile aliyoutangaza, ambayo aliacha nyumba yake na kuja Italia katika ardhi ya jimbo hilo, amesema Askofu Parmeggiani. Awali ya yote alianzia Palestina, mara baada ya mwaka mmoja tu tangu apewe daraja la ukuhani, akiwa Padre mwanafunzi wa Kitivo cha Sayansi Jamii katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana kuanzia 2008-2013 na baadaye kuanzia 2014- 2016 katika kitivo cha Sayansi Jamii,  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Tomas wa Aquino, Roma huku akitoa huduma yake ya kichungaji katika Parokia ya Palestrina, Carchitti na Caprania Prenestina.

Misa kwa ajili ya Marehemu Padre Timothy Andulile Manjonde wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya,Tanzania
Misa kwa ajili ya Marehemu Padre Timothy Andulile Manjonde wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya,Tanzania

Akiwa Palestrina, alikuwa na sifa nzuri sana hata  kuchaguliwa kuwa Katibu wa Baraza la Mapadre wa Jimbo. Mnamo 2015 kabla ya kuunganishwa kwa jimbo  hili aliomba kupokelewa Tivoli. Na kwa kutambua vizuri sababu ya maombi yake, Askofu amethibitisha alivyompokea vizuri , kwa sababu alikuwa anamjua vema alivyo kuwa Padre mwema na muwazi. Kwa njia  hiyo alimtuma katika Parokia ya Mtakatifu Maria Mpalizwa la Ceretto Laziale, kwanza msaidizi na baadaye mnamo tarehe 8 Desemba 2016 hadi mauti yalipomfikia alikuwa ni mhusika mkuu wa Parokia na kwa ajili ya kuwa kitovu cha mapadre wengine wanafunzi kutoka jimbo lake la Mbeya Tanzania, hata wa Tivoli na Palestrina, Italia. Alikuwa Padre mwenye sifa nzuri kwa mapadre wenzake na ambao walimchagua hata Tivoli kuwa mwakilishi wa V, wa makamu wa Baraza la Kichungaji la Jimbo.  Na alikuwa anasifiwa hata Tanzania mahali ambapo mnamo tarehe 15 Novemba 2018, alikuwa amechaguliwa awe  Mkurugenzi wa Kitengo cha Vijana cha Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC).  Lakini kwa unyenyekevu wake mara baada ya kuombwa na Askofu mwenyewe  wa Jimbo la Tivolo- Palestrina, kwa makubaliano na Askofu wake Mbeya, alikubali kubaki tena Cerreto kati ya watu wake, kwa mkataba wa kichangaji ambao uliokuwa umalizike mnamo 2024.

Padre Timothy akabidhiwe kwa Mungu wa maisha na huruma

Askofu Mauro Parmeggiani akiendelea alisema  kwamba kwa sasa ni kumkabidhi kwa Mungu wa maisha, na wa huruma na kwa Ayubu kwa kurudia maneno yake ambayo Padre Timothy angesema: “ Nami baada ya ngozi yangu kuharibiwa, bado nikiwa na mwili huu nitamwona Mungu; mimi nitamwona kwa macho yangu mwenyewe: mimi, wala si mwingine” (Ayubu 19,26 -27). "Na wakati tunasali kwa ajili ya wokovu wa roho yake milele iliyochaguliwa, tumwombe Padre Timothy, kwa kufikiria kwamba Yeye tayari yupo katika Fumbo la Muungno na Upendo wa dhati wa Mungu katika matarajio ya ufufuko wa mwili, ili asali kwa ajili yetu, kwa ajili ya Kanisa la Tivoli na Palestrina, kwa ajili ya Parokia ya Cerreto Laziale na kwa ajili ya Jimbo lake Kuu la Mbeya, ili lisikosa kamwe miito mitakatifu ya kikuhani, jasiri kama alivyokuwa jasiri Padre Timothy kwa kukabiliana na ugonjwa, ambapo alikuwa na utambuzi na wa kifo. Miito ambayo itambue kuhusisha mizigo yetu midogo kwa kuitazama kwa mtazamo mpana na wenye utajiri wa imani kwa Mungu na kwa ndugu", alisema Askofu.

Mama Maria wa Neema amwakilishe Padre Timothy kwa Mungu kwa upendo wa kimama

Kwa kuhitimisha amesema, Padre Timothy amekufa siku ambayo katika Parokia yake Cerreto walikuwa wanaadhimisha  siku kuu ya Mtakatifu Sabastiano Msimamizi wa parokia hiyo. Hata yeye alikuwa ni kijana shuhuda wa Kristo.  Kwa maana hiyo Askofu amemwomba Padre Timothy  ili asali hata kwa ajili ya vijana, licha ya nyakati ngumu zilizopo waweze kuwa na nguvu ya kuanza maisha yao kwa upya na kama yeye, waweze kuyatoa kwa Bwana wakiwa na uhakika kwamba,  kwake Yeye hakuna lolote linalopotea,  badala yake wanayapata tele hasa duniani na katika milele. Askofu Mauro, amemgeukia Mama wa Mbingu na kusema Maria wa Neema anayefanyiwa ibada kuu katika Parokia ya Cerreto, amwakilishe Padre Timothy kwa Baba kwa upendo wa kimama ili aweze kupewa amani ya milele. Amina.

KIFO CHA PADRE TIMOTHY MWANJONDE
22 January 2022, 13:39