Tafuta

Jula la Kuombea Umoja wa Wakristo 18-25 Januari 2022. Jula la Kuombea Umoja wa Wakristo 18-25 Januari 2022. 

Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo:Ujumbe wa Makanisa ya Italia

Sisi ni kama nyota ndogo ambazo zinakarimu jirani kama ndugu na si kumwona kama mgeni.Ni kutoka katika Ujumbe wa Viongozi wa makanisa ya Italia:Wakatoliki,Wainjili na wakiorthodox walioandika pamoja kwa ajili ya waamini wao wote katika fursa ya Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo kuanzia Jumanne 18-25 Januari,siku ambayo Mama Kanisa anamkumbuka Mtakatifu Paulo Mtume wa Watu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika ujumbe wa mwaka 2022  wa  Makanisa Katoliki, ya kiinjili na kiorthodox nchini Italia walio uelekeza kwa jumuiya zao kwa ajili ya tukio la kiutamaduni la  mwaka la la Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo wanaandika kuwa: “Tukiangazwa na ubatizo wa pamoja, kwa pamoja sisi ni kama nyota ndogo ambazo hupamba kwa akili anga la kiroho la Kanisa la Kristo na ulimwengu mzima. Oikos kubwa yenye uwezo wa kukaribisha wengine na si kama mgeni bali kama kaka na dada anayetafuta familia ambapo atapata unafuu, mwanga na matumaini”. Juma la Kuombea umoja wa Wakristo linaanza Jumanne tarehe 18 Januari hadi 25 Januari 2022 sambamba na Siku Kuu ya Mtakatifu Paulo Mtume wa Watu. Katika fursa hiyo Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kuongoza masifu ya pili ya Jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta, Roma. Katika Juma hili kutakuwa na mikutano mbali mbali, sehemu za maombi, meza za miduara na maadhimisho mengine.

Ujumbe wa Viongozi wa Makanisa Italia umetiwa saini na Askofu Derio Olivero, wa Jimbo la  Pinerolo na rais wa Tume ya Maaskofu kwa ajili ya Uekumene na mazungumzo ya Baraza la Maaskofu Italia, Mchungaji Luca Negro ambaye ni Rais wa Shirikisho la Makanisa ya Kiinjili, Italia na Askofu Mkuu Polykarpos, wa Kiorthodox, Italia na Kisiwa cha   Malta  pamoja na Upatriaki  wa Kiekuemene wa Ulaya Kusini. “Kutoka Mashariki tuliona nyota yake ikitokea nasi tukaja hapa kumwabudu” ndiyo kaulimbiu ya Juma ambayo ilichaguliwa kimataifa na Baraza la Makanisa la Mashariki ya Kati, ambalo mwaka huu lilikabidhiwa jukumu la kuandaa na kupendekeza maandiko kwa ajili ya mikesha ya maombi. Katika ujumbe huo  viongozi wa Makanisa wa Italia wanaandika kwamba  katika nchi  ya mbali hivyo machoni mwa mwanadamu ilikuwa ni ya kutunza, lakini leo hii imekuwa ni maeneo yenye mateso, migogoro na vita. “Nchi iliyo ya mbali sana na njia yetu ya kuishi maisha ya kila siku ambayo leo imekuwa chimbuko la aina nyingine ya Uekumeni, ambayo tunaweza kufafanua kama eukumene  wa ufiadini”.

Nchi hiyo ndiyo inayotoa wafiadini ambao huiangaza mbingu ya kiroho ya Kanisa zima la Kristo kwa miali yao yenye nuru. Nchi hiyo ndiyo wapeleka kuwa na umakini wa mfano wa imani iliyo hai  ambayo inaweza kushinda tofauti zinazomgawanya Kristo, msingi wa pekee wa imani yao.  Kwa Wakristo wa nchi hizo za mbali, Makanisa nchini Italia yanatoa zawadi ya shukrani na ua dogo ambalo wanaliweka katika kutoka kwao mahali ambapo ndugu zao waliouawa kwa ajili ya Kristo wamelala. Wakati Juma la Kuombea Wakristo, waamini  Wakristo wanaombwa kusali kwa ajili ya umoja unaoonekana wa Kanisa. Sala hiyo inafanywa kwa upya kila mwaka na mwaka huu wanataka kutuliza majeraha ya woga, uchungu na kutokuwa na imani kwa wengine, ambayo yanaweza kuhatarisha kuwa sababu ya mateso ya wote.  Picha iliyoainishwa katika ujumbe kwa ajili ya Maombezi ya Umoja wa Wakristo kwa mwaka  huu ni muhimu. Ubinadamu wa leo unajifunga wenyewe, na unajaribu kuvunja uhusiano na wengine na kuishi sio tu kwa kujitenga kimwili, lakini hata katika kutengwa kwa kiroho, ambapo husababisha kukua kwa kasi kwa upweke na mateso ya kisaikolojia. Wakiwa wamekwama katika upweke wao wa kuishi, wanaume na wanawake wa siku hizi wanajililia wenyewe na kujiuliza: “ Je sala yetu inaweza kuwa na thamani gani mbele ya migawanyiko mingi inayorarua vazi moja la Kristo? Sala inaweza kuwa na thamani gani mbele ya utawala wa kifo?” Kwa maana hiyo mwaliko wao ni kuomba na kushirikiana kwa ajili ya upatanisho na kushinda migawanyiko iliyopo wanashauri viongozi hawa wa makanisa ya Italia.

17 January 2022, 15:14