Tafuta

17.01.2022: Siku ya XXXIII ya tafakari na maendeleo ya mazungumzo kati ya wakristo na Wayahudi. 17.01.2022: Siku ya XXXIII ya tafakari na maendeleo ya mazungumzo kati ya wakristo na Wayahudi. 

CEI na ARI:Siku XXXIII ya tafakari na mazungumzo ya wakristo na Wayahudi

Tarehe 17 Januari 2022 ilikuwa ni siku ya XXXIII kwa ajili tafakari na maendeleo ya mazungumzo kati ya wakristo na Wayahudi Italia.Ni fursa kwa ajili ya kuhamasisha kati ya sehemu zote mbili heshima ya mazungumzo na ufahamu wa utamaduni wa Wayahudi.Mkutano wa siku hiyo umefanyika katika Baraza la Maaskofu Italia kwa kuwaona viongozi wa Kanisa Katoliki na wa Kiyahudi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jumatatu tarehe 17 Januari 2022, umefanyika Mkutano katika Baraza la Maaskofu wa Italia wa kitaasisi kati ya Baraza la Maaskofu Italia (CEI na Jukwaa la Kiyahudi Italia(ARI). Katika mkutano huo walishiriki Askofu Stefano Russo, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI). Derio Olivero, Rais wa Tume ya Maaskofu kwa ajili ya Uekumene na Mazungumzo, Padre Giuliano Savina, Mkurugenzi wa Ofisi Kitaifa kwa ajili ya Uekumene na Mazungumzo ya Kidini, Rav Alfonso Arbib, Mkuu wa Wayahudu huko wa Milano na Rais wa ARI, na  Rav Riccardo Di Segni, Rabbino Mkuu wa Wayahudi wa Roma.

Mkutano wa mazungumzo kati ya wakristo na Wayahudi ulikuwa wa kidugu

Tarehe haikuchaguliwa tu kwa bahati bahati mbayao bali ilikuwa  tarehe 17 Januari ambayo ilikuwa ni siku ya XXXIII kwa ajili tafakari na maendeleo ya mazungumzo kati ya wakristo na Wayahudi Italia. Ni fursa kwa ajili ya kuhamasisha kati ya sehemu zote mbili heshima ya mazungumzo na ufahamu wa utamaduni wa Wayahudi. Mkutano huo uliofanyika katika hali nzuri na kidugu kwa kujkita kuandaa hata mikutano mingine ijayo ya kila tarehe 17 Januari ambayo pia usindikizwa na Ujumbe wa Maaskofu wa Italia CEI na Ujumbe wa ARI.

Ni jambo jema kuwa na ufahamu na shauku ya pamoja

Katika mchakato wa mkutano huo, ulioandaliwa chini ya uratibu wa sehemu zote mbili CEI na ARI, Askofu Russo Katibu Mkuu wa Maaskofu wa Italia wakati wa kutoa neno alisema kile ambacho wamefanya, kilikuwa ni wakati muhimu kuishi  kwa haki na matarajio ya siku ya mazungumzo kati ya wakristo na wayahudi. Walikutana pamoja ili kutafakari mchakato shirikishi. Katika Ujumbe wa Baraza la Maaskofu Italia kwa ajili ya siku hiyo mwaka huu, ambao uliliridhiwa na Baraza la Kudumu la Maaskofu alisisitiza kwamba unafafanua vizuri shauku ya pamoja ya Maaskofu kuweza kupeleka mbele mpango wa mazungumzo yao. Askofu Russo alisema kama anavyokumbusha Baba Mtakatifu katika Waraka wake wa Fratelli tutti na kunukuu kwamba;“Kufanya mazungumzo bila kuchoka na ujasiri haifanyiki habari kama  mapigano na migogoro, lakini ambayo yanasadia kwa dhati ulimwengu kuweza kuishi vema,  zaidi ya kile ambacho tungeweza kutambua (198). Kwa maana hiyo leo hii ni lazima kupyaisha utashi wa kukutana, inapotokea na ina manufaa ya kijamii. Dini daima ni kwa ajili ya amani.”

Tofauti zipo lakini lazima kuzishinda na kuzielewa

Naye Rav Arbib Mkuu wa Wayahudi huko Milano alisisitiza kuwa mkutano  uliwakilisha fursa muafaka kwa ajili ya kubadilishana mitazamo yao na maoni yao. Kwa mkutano huo waliweza kuona kuwa na mtindo wa kazi ambayo itajifafanua katika uratibu wa kazi. Hii itasaidia kuelewa vizuri maana yake na thamani ya mazungumzo. Kwa hakika kuna mambo mengi yanayozungukia mazungumzo. Yote hiyo lakini kwa kusisitiza inahitaji kuelewa vema ni tofauti zipi zinaweza kuunda mitafaruko ambayo lazima kuishinda au kwa urahisi kuielewa. Mazungumzo yanafanyika kutokana na wazo kwamba tofauti zipo au zinaweza kuwapo. Kwa maana hiyo ni matashi mema kwamba inawezekana kufikia ufahamu mkubwa wa pamoja. Mkutano huu wa kitaasisi umefuatiliwa na kusindikizwa na mipango mingi iliyohamasishwa kwa ngazi mahalia ili kuthamanisha Siku ya Mazungumzo hayo ambayo ni kielelezo cha ukuaji wa utambuzi wa lazima kwa kujuana vizuri na kuweza kukabiliana kwa pamoja.

18 January 2022, 15:20