Tafuta

 Maandamo kwenda wa Bikira maria wa CAACUPE nchini Paraguay Maandamo kwenda wa Bikira maria wa CAACUPE nchini Paraguay 

Paraguay:Vijana waliunganika Caacupé,Ni wa leo ya Mungu na ya Nchi!

Vijana wakatoliki nchini Paraguay hivi karibuni waliunganika pamoja huko Caacupé kusali na kuomba Baraka ya Mama Yetu wa Miujiza katika muktadha wa Hija yao ya kila mwaka.Mwisho wa hija hiyo walitoa ujumbe wao.Kama vijana wanataka kuwa wale ambao wamewawezesha kufikia ndoto zao na matumaini hata wale ambao hawawezi kusikilizwa sauti zao na kutoa huduma kwa Kanisa.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Mnamo tarehe 4 Desemba 2021 karibu vijana 500 kutoka nchini Paraguay wameunganika huko  Caacupé  kusali na kuomba baraka ya Mama Yetu wa Miujiza na msimamizi wa Paraguay, katika muktadha wa utabaduni wa hija ambayo inaandaliwa na Huduma ya kichungaji kwa vijana kitaifa ya Baraza la maaskofu nchini humo. Mwisho wa Misa Katibu Mtendaji wa kichungaji kwa ajili ya vijana, Bianco Prieto, alisoma ndoto na nia zao wanaso kusudia ambazoi waliandika kwa Pamoja. Mwisho wa siku vijana wa jimbo Concepción walikabidhi msalaba wa hija kwa vijana wengine wa Jimbo la Caninenyú. Toleo la mwaka 2021 lilikuwa linawalekea wachungaji na vijana wote waliokuwapo na wale ambao walifuatilia hija hiyo kwa njia ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwakilisha shauku na jitihada ambazo zimechukulwa na vijana wakristo wa Paraguay.

Waamini wakiwa wamefika katika Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Miujiza huko Caacupe,Paraguay
Waamini wakiwa wamefika katika Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Miujiza huko Caacupe,Paraguay

Kama vijana wanataka kuwa wale ambao wamewawezesha kufikia ndoto zao na  matumaini hata wale ambao hawawezi kusikilizwa sauti zao na kutokana na huduma ya Kanisa  na wanataka kuota ndoto na kujitahidi kuendelea kufanya kazi pamoja na wachungaji wao ili kufikia malengo yao. Kwa mtazamo wa Kanisa, vijana hao wanataka kujitahidi kwa ajili ya kuwa Kanisa la huruma, la ushiriki na kisinodi. Kanisa lenye milango wazo na si kwa maneno tu lakini kwa vitendo ili wote waweze kuingia wanapokwa wanahitaji na waweze kupata msaada wa kiroho na kibinadamu. Kanisa ambalo ni shuhuda kwa wasiostahili, wasiombuliwa na kueleweka, waathirika ambao hawapati katika jamii nafasi za kupata haki zao na usawa. Kanisa la kinabii bila kuwa na aibu ya kutangaza haki, magumu, matendo yasiyo ya kibindamu ambayo yanashambulia adhi ya binadamu.

Waamini wakiwa wamefika katika Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Miujiza huko Caacupe,Paraguay
Waamini wakiwa wamefika katika Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Miujiza huko Caacupe,Paraguay

Vijana wa Uruguay wanatambua kuwa Kanisa ni sehemu muhimu ya kijamii ambalo linafundisha kuwa na tazamo wa huruma, wa kujiuliza, muhimu na lengo kwa kile ambacho kinatoka na ili lisifunge macho na kubaki na sintofahamu mbele ya hali halisi za ucungu, ukosefu wa haki na ishara za utamaduni wa kifo ambao unaonekana kuwazunguka wao. Kwa baahati mbaya wanabainisha kuwa vurugu zimeongezeka katika nchi kwa nguvu sana, mauaji, kukamatwa, kutendewa vibaya kimwili na kisaikolojia kwa sababu nyingi lakini kati ya wote ni vijana ambao wanakataa hasa ufisadi usio wa haki ambao unanunua na kuuza kila kitu. Vijana kwa maana hiyo wanasema kuwa kuna haki na inawasubiri kama wazalendo wa nchi hiyo yenye utajiri mwingi lakini kwa kuwa na uendeshaji mbaya sana katika kesi nyingi na sekta.

10 December 2021, 16:37