Tafuta

2021.11.15 Padre  Patton katika eneo la Ubatizo wa Yesu 2021.11.15 Padre Patton katika eneo la Ubatizo wa Yesu  

Nchi Takatifu,Noeli 2021:Padre Patton,Mungu yuko karibu na familia

Katika madhabahu ya Groto la Maziwa,linalosimamiwa na Usimamizi wa Nchi Takatifu,ndipo umetolewa jumbe Heri ya Matashi mema ya Kuzaliwa kwa Bwana hasa kwa mtazamo maalum wa familia zilizo kwenye matatizo ulimwenguni.Ni ujumbe wa matumaini wa Noeli ambao umetolewa kama zawadi ya Mwana wa Mungu,kutoka kwa Padre Patton Msimamizi wa Nchi Takatifu.

Na Sr. Angella Rwezaula-Vatican.

Ni mwaka wa pili tena, familia za Bethlehemu zinateseka sana kutokana na matokeo ya kiuchumi yaliyosababishwa na janga la uviko mji ambao ulikuwa umezoea utalii, na watu wengi kuishi maisha yao ya kiuchumi na kibiashara kwa utalii. Kutokana na hilo, ujumbe wa matashi mema ya Noeli 2021 unawagusa wao kwa namna ya pekee ulioandikiwa na Padre Francesco Patton ofm, ambaye ni Msimamizi wa Maeneo ya Nchi Takatifu.  Kwa mujibu wake kuhusu  mgogoro huo amesema ni familia ambazo wazazi ni kama Yosefu na Maria mchumba wake ambao wanatafuta kila iwezekanavyo kuwatunza watoto wao katika kipindi hiki kigumu cha  matatizo kihistoria. Wazo la Padre Patton linawaelekea familia zote zenye matatizo ulimwenguni na ambazo zimelazimika kukimbia nyumba zao, nchi zao, maeneo yao kutokana na kuteswa na sera za kisiasa ambazo zinafuata mantiki ya Herode au majanga makubwa ya kiuchumi, uharibifu wa mazingira utokanao na majanga ya asili au kwa njia ya mkono wa mwanadamu unaonaondelea na ambao unalazimisha kuacha kila kitu na kuhama kwenda mahali popote pale la muhimu kutafuta hali bora

Ujumbe wake Padre Patton unatolewa akiwa katika mazingira yaitwayo:“Groto ya Maziwa” ni Madhabahu ambay katika maandishi limetokea kwa Familia zote kama Familia Takatifu ya  Yesu, Maria na Yosefu, mahali ambapo Mama Maria anawaombea familia zote wanaojimudu vema na zile ambazo zinalazimika kukimbia ili zitambue kufungua mioyo yao.  Padre Pattoni akifafanua juu ya ujumbe huo amesisitiza kuwa Matashi mema ya mwaka huu yamefanyika katika mazingira maalum kwa makusudi katika Kanisa kuu lijulikanalo la kutoa Maziwa ambalo liko na mbali wa  kilometa mbili kutoka katika Groto ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu. Eneo hilo kwa mujibu wa utamaduni ni mahali ambapo inasemekana Familia Takatifu wakati wa kukimbia Herode kuelekea nchini Misri walisimama hapo ili kumnyonyesha mtoto Yesu. Kwa maana hiyo ujumbe unahusiana moja kwa moja na hali za kila mmoja wetu, kwani mwana wa Mungu aliweza kubeba janga la historia yetu, ambayo siyo rahisi, lakini iliyowezekana. Alionja ugumu na hatari ambazo ni sehemu ya maisha.

Padre Patton amesema, ujumbe huo pamoja na kwamba ni wa Noeli, lakini unao mtazamo mwingine tayari wa Pasaka kwa sababu kukimbia kwake Yes una wazazi wake  huko Misri ni kutokana na kwamba Herode alitamani kuwaondoa watoto wote kwa kufikiria ataweza pia kumuua mridhi wa ufalme na hivyo matukio hayo na maendeleo hayo yanakufanya utambue jinsi mwana wa Mungu, tangu utoto wake aliweza kukabiliana na ulimwengu wa vikwazo na wakati huo huo, Mwana wa Mungu tangu mtoto alikuja kutoa maisha kwa ajili ya wokovu wetu. Padre Patton ameeleza kwamba kipindi  cha Noeli ni kipindi cha matumaini, kwa sababu ikiwa mtoto wa Mungu kwa kufanyika mwili alifika kwa kila mtu, ina maana sana kwamba kila mmoja anaweza kuwa bora na kwamba inawezekana kubadilika na kwamba upendo huo mkubwa ambao unajionesha unaweza kubadilisha ulimwengu ambao kwa bahati mbaya unaokana upendo huo kupungua.

Ujumbe wa matumaini ni ujumbe wa matumaini, amesisitiza. Katika siku kuu hii, Padre Patton anafikiria Betlehemu, yaani kutoka Nchi Takatifu iweze kweli kusikika neno la tumaini, ambalo ni matashi mema kwa familia zote na watu wote. Liturujia katika kipindi hiki amesema kuna nyimbo za zamani sana na nzuri ambazo zinashangilia kuzaliwa kwa Yesu kama kuzaliwa kwa Jua ambalo linakuja kuangaza kiza la ulimwengu. Kwa maana hiyo hata katika usiku wa giza ni lazima kukumbuka kuwa Yesu ni mwanga wa kweli, alikuja ulimwenguni ili kuangazia kila mtu, kuangaza hata matatizo, ambayo kila mmoja anaishi, kuangazia familia, kuangazia kila maisha binafsi ya kuishi. Na ndiyo matashi mema ya kutambua namna kuchota hata cheche ndogo sana za moto unaongaza huko Betlehemu, ili kuweza kuhisi angalau kidogo faraja ya ndani ya Moyo.

24 December 2021, 14:02