Tafuta

Maaskofu wa AMECEA Maaskofu wa AMECEA 

AMECEA:Lazima kusimamisha vurugu na kuhamasisha kuishi pamoja

Katika mkutano wa Tume ya Kuhamasisha amani na amaendeleo Fungamani ya binadamu na haki ya AMECEA,ulioanza tarehe 29 Novemba hadi tarehe 2 Desemba,wamechapisha ujumbe wao wa mwisho kwa kutazama masuala ya migogoro ya kikanda kama vile Ethiopia na Sudan na changamoto za sasa hasa za janga la UVIKO-19 na mengine.

Na Sr Amgella. Rwezaula – Vatican.

Maaskofu wa Tume ya kuhamasisha amani na maendeleo Fungamani ya binadamu, haki na amani ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki (AMECEA), waliokusanyika kuanzia tarehe 29 Novemba hadi tarehe 2 Desemba 2021 huko Nairobi Kenya kwa ajili ya mkutano wao wa kiutendaji  wa kila  mwaka na baada ya hitimisho la wameandika ujumbe wao kwa kuonesha wasi wasi mkubwa mno kutokana na kuongezeka kwa migogoro katika Kanda. Ujumbe wao unasema: “Tunahuzuni na migogoro na vurugu zinazoendelea katika baadhi ya maeneo yetu, hasa huko Ethiopia. Watu wengi wamekufa na mali zao zinaharibiwa katika mikoa iliyokumbwa; amani ambayo ni utukufu wa ubinadamu, unahitaji uwezekano. Tunashauri sehemu zenye migogoro, kusitisha vurugu za kikabila, kukamata watu na kuhamasisha amani ya kuishi”.

Sudan wameanza kutafuta njia ya kutotumia vurugu

AMECEA anaunga mkono na watu wa Sudan ambao wanatafuta njia za kutotumia vurugu kama ilivyo mtindo mpya wa kisiasa kwa ajili ya amani kuelekeza mpito wa kidemokrasia. Katika ujumbe huo baada ya jukwaa lao wanashauri mashirika mengi ya kiserikali pia kujihusisha kutia moyo juhudi kuelekea mpito wa amani.  Maaskofu wanasifu kazi ya binadamu kwa ajili ya maendeleo ya chanjo, dawa na zana nyingine za matibabu, wakisisitiza kwamba ukosefu wa usawa katika kupata madawa daima uko wazi kwa kukosolewa. Kwa sababu hiyo, Makanisa ya AMECEA yanaomba usawa katika usambazaji wa dawa na chanjo dhidi ya UVIKO-19 ulimwenguni kote na kuwataka watu kuheshimu mazoezi na kanuni zilizowekwa  mtindo wa maisha muhimu kwa kuzuia na kinga.

Changamoto za biashara haramu ya binadamu, wakimbizi wa ndani, ajira na itikadi kali

Mkutano wa Maaskofu wa Afrika Mashariki pia ulijadili changamoto za biashara haramu ya binadamu, wakimbizi na wakimbizi wa ndani, ukosefu wa ajira kwa vijana, itikadi kali, ubaguzi na masuala ya mazingira, utawala bora, kampeni za uchaguzi katika baadhi ya maeneo. Katika maeneo haya yote, inahimizwa kuzingatia njia ya mazungumzo kwa ujumla na watu, na serikali na viongozi wa kisiasa. Waamini na watu wenye mapenzi mema wanapaswa kujituma katika kazi ya kuzuia migogoro na kujenga amani. Wote wanaitwa kuwa na mshikamano na maombi kwa ajili ya watu walioathirika na migogoro na migogoro mbalimbali,kuendeleza msamaha, upatanisho na kuishi pamoja kwa amani.

06 December 2021, 15:02