Tafuta

Padre Piloni:Ziara ya Papa Assisi ishara za dhati na mkoma anapokuwa mgumu

Ni tabia ipi ya kuwa nayo mbele ya wenye hitaji?Katika sehemu ya nne ya tafakari katika Mzunguko wa ‘Mama maskini mtakatifu’ ambayo inajikita kwenye fursa ya maandalizi ya Papa Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Malaika Assisi.Mkuu wa Shirika la Wafranskani (OFM) wa Umbria na Sardegna anatoa baadhi ya tafakari kuanzia na tukio la mkoma aliyekutana na Mtakatifu Francis.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Katika tafakari ya nne ya Padre Francesco Piloni inazungukia juu ya upendo na kupenda, ambapo anasisitiza juu ya ulazima wa kumfuata Kristo, hasa katika uhusiano na mwingine mwenye kujikuta na uhitaji. Ni katika mzunguko wa tafakari wakati wa maandalizi ya ujio wa Papa Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Malaika, Assisi unaotarajiwa kufanyika mnamo tarehe 12 Novemba 2021. Mada inayoongoza tafakari ya Padre Piloni ni ‘Mama Maskini Mtakatifu’ kwa kujikita kutazama tukio lile la Mtakatifu Francisko la kukutana na mgonjwa wa ukoma ambalo lilimbadilisha maisha yake ya awali na kuanza mchakato mpya wa uongofu. Katika tafakari hii, Padre Piloni anazungukia ulazama wa upendo na kupenda kwa dhati na kusisitiza umuhimu wa kufuata mfano wa Kristo, hasa katika mahusiano na mwingine ambaye anajikuta kwa hakika na uhitaji, akikimbusha kwamba zawadi ya kwanza ya maskini ambayo anasubiri kweti sisi si suala la  sahani ya chakula cha moto, badala yake ni kudumisha ule urafiki na udugu wa kweli. Mshikamano kamili lazima ueleweke na muhimu kwa sababu mwingine anaweza kuelewa vizuri zaidi, uhusiano unapojikita juu ya upendo wa kweli.

HABARI ZA KANISA NA KIJAMII 10 NOVEMBA 2021

Kuhusu tafajari hii si tu ile ya kutunza mkoma kwa upande wa Mtakatifu Francis, lakini ni suala la Mtakatifu huyo kuweza kuchagua kwa ajili yake na kwa ajili ya ndugu wadogo wake hali hiyo hiyo, “kwa sababu Kristo anataka kwetu sisi kutambuliwa kama mkoma” (rej. FF, 1857). Katika maandiko kuhusu Mtakatifu Francis, (Fioretti) yanasimulia juu ya mmoja wa watu hawa waliotengwa na kusemwa kuwa: “mtu asiye na subira na asiyeeleweka na mwenye majivuno, asiyestahimili mtazamo wa ndugu wadogo wanaomtunza na kwa hivyo anakuja kukataa utunzaji wao. Kwa maana hiyo, kukutana na mtakatifu Francis, ambaye mwenye ukoma,  alitoa malalamiko kwake kwa kudai kwamba si lazima tu avumilie ugonjwa wake, lakini pia kwamba wale ambao Francis amewaweka kuwa karibu  yake “hawamtumikii inavyopaswa”.

Jibu la maskini Francis lilikuwa ni thabiti.  Yeye lijitoa kumtunza binafsi na kujiweka katika  hali yake kamili ya kuwa hovyo.  Kwani amkoma alimwambia kwamba: “Ninataka unioshe mzima kwa  maana ninanuka vibaya sana kiasi kwamba hata mimi mwenyewe siwezi kustahimili”  kwa maana aliomba huyo mtu masikini na kupata alichoomba. Kwa kutoa viungo vyake vilivyo jeruhiwa viliguswa kwa mikono ya Mtakatifu Francis, na maoni ya simulizi hiyo inaeleza juu ya miujiza ambayo hufanyika katika nafsi kwamba: “mwili ulipoanza kupona, ndivyo ulivyoanza kupona hata nafsi”. Kwa njia hiyo Padre Piloni amethibitisha kwamba kwa kutomia huruma  iliyo tolewa kwake, iliruhusu uponaji kamili na kugusa matumbo yake, kwa kumkomboa kutokana na hali ya mateso ya kimwili na ya akili.

Ni upendo katika njia ambayo iliruhusu muujiza na kuhitimisha uhusiano huo wa kusaidia. Kwa jinsi tunavyotambua upendo na kuutimiza, ndivyo lilivyo suala zito, amesisitiza Padre Piloni, kwa ufupi amesema chanzo cha upendo ni kutoka kwa Mungu na Kristo ndiye kielelezo cha upendo wa kweli. Na hii inatakiwa iwe pia kweli leo hii. Padre Piloni katika kipengele cha uelewa wa  huruma amesisitiza  kama sehemu  msingi ya ushuhuda. Mfano uliotajwa ni wa kijana anayetumikia Caritas  na ambaye siku moja, baada ya kupeleka huduma ya  mfuko wa chakula kwa wiki kadhaa kwa familia ambayo bado ilikuwa ya baridi na imejitenga, aliamua kupeleka shada la maua. Na kwa kufika katika nyumba hiyo mjumbe wa nyumba hiyo alimjibu:“Hatimaye umetuona”. Hii ndiyo maana ya kupenda kama Kristo apendavyo, amesema Padre Piloni.

Mfano wa Injili wa Msamaria Mwema unaeleza vizuri kile ambacho huruma hii inajumuisha  kuiga. Maandishi ya Mjinjili Luka  yanasema kwamba mtu mwenye bahati mbaya aliyepigwa n ana kubwaki  butwaa na majambazi aliokolewa na Msamaria ambaye alimwona, alimhurumia, na kumtunza. Kwa maana hiyo hatua zote ni muhimu na zinaonesha hatua inayoanzia na macho na baadaye inahusisha moyo na mikono. Kwa kufafanua zaidi Padre Francesco amesema siyo rahisi juhudi ile ya kuwahuduma maskini. Ni suala la kujiachia, huku akisisitiza haja ya kiwango fulani cha upendo kuanzishwa na kila kitu kukuzwa ndani ya  moyo. Kutunza bila upendo ni sawa na utendaji mkame na mtupu ambao katika Injili unawakilishwa na ule kwenda zaidi ya, mtu kwenda njia zake mwenyewe. Kama alivyofanya kuhani Mlawi kwenye simulizi la Msamaria Mwema.

10 Novemba 2021, 14:05