Tafuta

Rumbek; Sekobdri ya Sudan Kusini ya Wanawafunzi wanaoongozwa na Wanashirika wa  La Salle. Rumbek; Sekobdri ya Sudan Kusini ya Wanawafunzi wanaoongozwa na Wanashirika wa La Salle. 

Sudan Kusini waadhimisha siku ya Shule Katoliki:kufanya kazi kwa ajili ya amani ni kukubali Kanisa

Kila mwaka katika Jimbo la Tombura Yambio hufanya Siku ya Shule Katoliki.Kwa 2021 wameongozwa na kauli mbiu “watoto wa shule tupo kwa ajili ya amani.Katika ujumbe uliosomwa na Makamu, Askofu wa jimbo hilo amebainisha ambavyo ili kufikia utume wa kielimu katoliki katika jimbo hilo lazima kuendelea katika uweza wao wa kutenda kama jumuiya inayoendelea kujifunza.

Na Sr. Angella. Rwezaula – Vatican.

Wakati nchi inaendelea kuishi kipeo cha kibinamu kizito sana vijana wa Jimbo la Tombura Yambio hawakuacha kuadhimisha Siku ya Shule Katoliki, kwa lengo la kuleta tumaini na imani binafsi, katika nchi iliyojaribiwa ya Ikweta ya Magharibi. Maadhimisho ambayo hufanyika kila mwaka yanaingia moja kwa moja katika mpango wa kijimbo. Kwa kawaida uunganisha pamoja, taasisi zote katoliki za jimbo hilo. Miongoni mwake, Chuo Kikuu katoliki, sekondari za kike na kiume zote na shule zote  misingi za kike na kiume..

Aliyeongoza Liturujia ya misa kwa mamia ya wanafunzi na vijana kutoka katika Parokia ya Mtakatifu Maria Mama wa Mungu ya Yambio, alikuwa ni kaimu Mkuu wa Mpito wa Jimbo, Padre Tombe Charles. Kwa kukumbusha kuwa Mtakatifu Daniele Comboni, Msimamizi wa jimbo katika mafunzo aliyepanda mbegu ya kwanza ya imani na katika elimu katoliki ya wakati huo Sudan alisema kwamba Mtakatifu Daniele Comboni anawaalika kuanza kwa upya maisha mapya ili kuweza kuwa karibu na Yesu Kristo na kupitia mafunzo ili kupata lolote jipya ambalo mwanzo halikuwapo. Licha ya changamoto ni muhimu kujikita kwa kina juu ya kile ambacho wanafanya kwanza. Akiendelea amewambia wanafunzi hao kuwa wote wanaweza kujikamilisha lakini ikiwa wote watafanya kazi kwa ajili ya amani inayotoka kwa Mungu tu na ndiyo maana ya kukubali Kanisa.

Kwa hakika alisema wao walikuwa wameunginika na Mungu kwa ajili ya utume wa kupeleka amani kwa watu na kwamba wanafunzi ambao wanajifuznia wanaweza kweli kuwa watu wataalam na ambao wanapaswa kufanya kazi kwa ajili ya umoja na upendo kwa ajili ya ubinadamu wa sas ana ujao. Naye Askofu wa Jimbo Eduardo Hiiboro Kussala katika ujumbe wake uliosomwa kwa niaba yake na Mkamu wakati wa maadhimisho hayo amesema kuwa Wanaamini kwamba ili kuweza kufikia utume wa kielimu katoliki katika jimbo katoliki la Tombura-Yambio, ni lazima kuendelea katika uweza wao wa kutenda kama jumuiya inayoendelea kujifunza. Amewatia moyo wanafunzi wote, walimu na wote wanaofanya kazi katika sekta ya kielimu ya kijimbo kwamba lengo kuu la shule zote katolki ni lile la kutoa elimu katoliki ambayo wanafunzi wote wanauhishwa, wanajifunza na kufanya uzoefu wa kukua kialimu katika mazingira salama na makarimu yenyem msingi wa thamani za Injili.

Karama ya shule katoliki ya jimbo ni kuhudumia Mungu na jumuiya kwa ujasiri na ufungamanishwaji kwa kuhakikisha mwanga unaangaza kwa kila mtoto. Watoto wa shule kwa ajili ya amani ndiyo ilikuwa  kauli mbiu iliyoongoza toleo hili la mwaka 2021 huku likiwaunganisha shule zote katika Uwanja wa Uhuru wa Yambio kuanzia asubuhi na  maandamano kupitia mji hadi kifikia Kanisa la Mtakatifu Maria Mama wa Mungu la Yambio. Kwa sasa Jimbo Katoliki la Tombura-Yambio lina taasisi 5 za mafunzo ya juu, shule 8 za sekondari katika Parokia mbali mbali, shule 28 za msingi na 24 za Awali.

25 October 2021, 15:06