Tafuta

2021.10.18: Ufunguzi wa Sinodi kwa ngazi ya kijimbo katika Kanisa la Cairo nchini Misri 2021.10.18: Ufunguzi wa Sinodi kwa ngazi ya kijimbo katika Kanisa la Cairo nchini Misri 

AMECEA inawatia moyo waratibu kufanya kazi kimkakati kwa ajili ya mchakato wa Sinodi

Umefanyika mkutano wa wajumbe wa Amecea ambapo wanasisitizia waratibu wa majimbo yote kufanya kazi kimkakati kwa ajili ya kuhusisha idadi kubwa ya waamini katika mchakato wa sinodi 2021-23.Nchi zinazojumuishwa na AMECEA ni Eritrea,Ethiopia,Kenya,Malawi,Sudan,Tanzania,Uganda na Zambia.Jumapili tarehe 17 Oktoba umefanyika uzinduzi wa mchakato wa Sinodi kwa ngazi ya kijimbo ulimwenguni kote.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Inahitaji kushirikiana ili kuhakikisha kuwa makanisa ya Afrika Mashariki yanaendelea kuratibu na kuheshimu muda uliopangwa kwa majimbo yote na kwa namna ya kupeleka mbele sauti ya Afrika katika hatua ya kibara katika  safari ya Sinodi. Ndiyo maelekezo yaliyotolewa hivi kwa waratibu wa majimbo na kitaifa katika mchakato unaoendelea wa Sinodi ya Makanisa,  kwa wajumbe wa AMECEA.

Katika mkesha wa ufunguzi wa hatua ya kijimbo katika mchakato wa Sinodi ambao umezinduliwa  tarehe 17 Oktoba 2021 kwa nchi za Eritrea, Etiopia, Kenya, Malawi, Sudan, Tanzania, Uganda na Zambia, wajumbe wa nchi hizo wameshiriki mkutano kwa njia ya mtandao ili kuweka sawa maandalizi katika nchi hizo. Katibu wa Amecea  Padre Anthony Makunde akizungumza na washiriki hao amekumbusha kwamba muda ni mfupi kwani kufikia Aprili 2022 majimbo yote ulimwenguni yanapaswa kukukabidhi maoni katika majimbo yao mchango uliokuswanywa ambao utasaidia katika mikutano ijayo ya miezi sita ili wao waweza kuwekwa kwa pamoja kwa ufupi  kwa ajili ya hatua nyingine ya kibara.

Kwa njia hiyo, Katibu Makunde ametoa mwaliko kwa kuratibu vema kwa namna ya kuheshimu muda uliopangwa na Skretarieti ya Sinodi, ili kuhakikisha kuwa tukio hili linakuwa kweli safari ya pamoja kama ilivyombwa na Papa Francisko. Jambo hili pia lilikumbushwa na Padre Emmanuel Chimombo, mratibu wa kichungaji wa Amecea, ambaye alisisitiza kuwa lengo la Shirikisho hilo ni kukuza mchango wa Makanisa ya Afrika Mashariki kwa Kanisa zima la ulimwengu. Padre Chimombo amebainisha jinsi ambavyo kwa muda wamegundua kuwa sauti ya Afrika haisikilizwi katika programu za sinodi. Kwa maana hiyo wanataka kuhakikisha kuwa Amecea inapata sauti yenye nguvu, inashiriki kikamilifu na inachangia vyema katika mchakato wa sinodi na mafanikio yake kwa ujumla.  Kwa sababu hiyo, pia alisisitiza kwamba  Amecea imejipa dhamira ya kuongeza uelewa na kutangaza mchakato wa Sinodi katika vyombo vya hbari na taasisi mbali mbali za Kanisa, pia kwa kushirikiana na Baraza la Wajesuiti wa Afrika na Madagascar (JCAM).

Kwa upande wake, mratibu wa Kiteknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) ya Amecea, Bernard Mberere alisisitizia hitaji la mtandao kuhusisha waamini wengi iwezekanavyo katika mchakato wa sinodi. Yeye amesema kwamba wakitembe kwa pamoja wataweza kuwafikia watu wengi, watashiriki habari nyingi na Sinodi inaweza kuadhimishwa na kila mtu. Ili kufikia hatima nzuri ya hatua hizi za maadalizi ya sinodi, tovuti ya Amecea tayari imeweka zana kwenye ukurasa wa mtovuti yao kuhusu Sinodi 2021-2023 , zana ambazo zinasasishwa mara kwa mara. Ni mwaliko kwa wote watumiaji kujitoa kushirikisha maoni yao juu ya mikakati bora  na  kukusanya idadi kubwa ya maoni kutoka kwa Makanisa mahalia kwa namna ya pekee yanaoyohusu Amecea yaani  Eritrea, Etiopia, Kenya, Malawi, Sudan, Tanzania, Uganda e Zambia.

18 October 2021, 12:35