Mwezi Novemba AMECEA itazindua Mkutano wake mkuu wa XX
Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa AMECE, Padre Anthony Makunde wakati akihojiwa mnamo Ijumaa tarehe 22 Oktoba 2021 amethibitisha kuwa “Baada ya kutathimini hali halisi ya sasa ya UVIKO -19 katika kanda, tumeona kuwa inahitajika kuzindua Mkutano Mkuu wa 20 mwezi Novemba ili kuanza maandalizi na kuona jinsi gani tutaweza kukabiliana na janga. Hata kama tunazamia kufanya mkutano kwa uwepo mwezi Julai ujao, bodi bado itatazama hali halisi ya janga kufikia mwishoni mwa mwezi Januari 2022 kwa kutathimini uwezekano wa kuwa na mkutano huo au hapana na kwa maana hiyo maamuzi ya mwisho yatafanyika mwezi Februari”.
Kama mambo yatakwenda sawaJulai mkutano wa XX utafanyika Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa AMECEA aidha alisema kwamba ikiwa kila kitu kitakwenda vizuri, mkutano huo utaweza kufanyika katika Juma la pili la mwezi Julai 2022, jijini Dar es Salaam Tanzania, kwa ufunguliwa na Misa, siku ya Jumapili tarehe 10 Julai 2022. Wakati wa mkutano wao uliofanyika kwa njia ya mtandao wa Bodi ya utendaji, wajumbe hao waliidhinisha pia Mbinu bora za AMECEA za mtiririko wa Misa na Ibada maalum ambazo zitatoa miongozo ya mazoezi ambayo hata hivyo yamekuwa ya kushangaza kufuatia na hatua za kuzuia UVIKO-19 na ambazo ziliwafanya waamini wa kikristo wengi kufuatilia misa mtandaoni.
Mbinu na njia za kuweza kufanikisha tukio
Kwa mujibu wake amemsea “Mazoea haya bora yataongoza hata mikutano ya washiriki kuzingatia kanuni za Ibada Takatifu kwa wote katika Kanisa Katoliki na mawazo msingi ya utangazaji ili kutoa matokeo mazuri yanayotarajiwa katika mazingira ya maombi na ubora wa maudhui huku waamini wakifuatia liturujia kwa karibu. Akiendelea Padre Makunde alifafanua hitaji la miongozo ya utiririshaji wa moja kwa moja wa Misa na kuongeza kuwa AMECEA itashirikisha hati kwa wajumbe mabaraza ya maaskofu kwa ajili ya kufuatilia. Zaidi ya hayo, sera na miongozo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) iliyorekebishwa kwa Sekretarieti ya AMECEA pia imeidhinishwa.
Sera ya ICT ya AMECEA imebadilishwa kuenddana na wakati uliowekwa na janga
Kwa mujibu wa Padre Makunde, amesema sera ya ICT ya Sekretarieti ya AMECEA ya 2015 imerekebishwa kufuatia mabadiliko ya kiteknolojia yanayobadilika kila wakati, habari zinazoibuka, vitisho vya usalama na changamoto na janga la UVIKO-19 ambalo limebadilisha shughuli na sasa wafanyakazi wanaweza kufanya kazi kutokea nyumbani na kazi zaidi rasimi zimefanyika mtandaoni. Mapitio hayo yanalenga kutoa mfumo makini unaoendana na hali halisi ya kiteknolojia na mienendo ya sasa, na ambao utaongoza utoaji wa huduma kwa ajili ya utaratibu kwa njia bora na yenye ufanisi zaidi kuelekea utekelezaji wa majukumu ya Sekretarieti ya AMECEA, alisema Katibu Mkuu siku ya ya mahojiano. Ijumaa 22 Okotba. Sera hiyo imeanzisha miongozo mipya ikiwa ni pamoja kati ya nyingine, kulinda watoto na uonevu kwa njia ya mtandao, kufanya kazi nyumbani na matumizi ya runinga (CCTV), katika eneo la kazi.