Tafuta

Mke wa Marehemu Luka Attanasio,Padre Maccalli na Carlssare wametoa ushuhuda katika uzinduzi wa Tamasha la Utume Milano 2022 Mke wa Marehemu Luka Attanasio,Padre Maccalli na Carlssare wametoa ushuhuda katika uzinduzi wa Tamasha la Utume Milano 2022 

Italia:Uwakilishi wa Tamasha la Utume Milano 2022:Maandalizi na mipango mingi

"Milano inahitaji kusikia wanasema hamka na ishi".Amesema hayo Askofu Mkuu wa Milano wakati wa kuhitimisha mkutano na vyombo vya habari na kuzindua Tamasha la Utume litakalofanyika katika mji huo kuanzia tarehe 29 Septemba hadi 2 Oktoba 2022.Ushuhuda:Seddiki mke wa Luka,Askofu Carlassare na Padre Maccalli.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Katika uwakilishi wa Tamasha la Utume Milano,2022 nchini Italia uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2021, walitoa mada mbali mbali na hatua za maandalizi, ushuhuda mbali mbali  umetolewa kwa mfano na Seddiki, mwanaharakati na mke wa Luka Athanasio aliyekuwa Balozi wa Italia nchini Conngo DRC na kuuawa mnamo tarehe 22 Februari iliyopita, Askofu Carlassare, Mtawa wa kikomboni kutoka Vincenza Italia na Askofu wa Jimbo la Rumbek nchini Sudan Kusini  aliyepigwa risasi akiwa nyumbani kwake na Padre Maccalli mtawa na mmisionari wa Crema, Italia  aliyekombolea baada ya miaka miwili kutoka kwenye kifungo cha kwa wateka nyara wa kijihadi  huko Niger.

Akizungumza katika uwakilishi huo wa Tamasha la Milano 2022 Askofu Mkuu Delpini amesema kuwa: "inabidi kuondokana na jinamizi la janga ili kuwa na  shauku ya kuishi kwa ajili ya zawadi. Milano ilihisi jinamizi wakati wa janga. Jangwa katika barabara, shughuli za uzalishaji mali kusimama, jinamizi la umaskini unaoendelea, na sasa bado hali ipo ya kuona kila kitu kimechelewa na kama vile adui  bado anazidi kutufuata, anatusukuma kukimbia. Lakini mafanikio, utukufu, fedha ni mambo ya kifikirika.  Inahitaji kwa kusikia mtu anayesema, hamka, kwa kuwafanya watambue kilio cha wasio na furaha ulimwenguni, wimbo wa hekima ya watu na kilio cha maskini. Tamasha la utume litakuwa ni tukio muhimu tu ikiwa linaweza kuamsha Milano na kulitia moyo ili kuishi na kuhisi joto la Roho ambaye aliwaka katika karne na anaendelea kuwaka kwa kutoa shauku katika mioyo ya wamisionari. Moto huo lazima uwake na kutoa mwamko mpya wa kuwasha moto mwingine."

Akianza ushuhuda wake Bi Zakia Seddiki amesema kuwa: “Si idadi ya miaka ya maisha inayohesabiwa, lakini ni maisha ambayo yamo katika miaka hiyo. Luka alitoa maisha yake hata kwa kifo chake. Sisi sote tuko safari ya kupita, lakini ni vizuri kutumia vema kile ambacho tulipewa kuishi, yaani kitu chochote  kwa ajili ya wengine. Sisi sote tunao utume: wa kwangu ni kuishi kwa ajili ya watoto wangu, lakini hata kuishi kwa ajili ya watoto wa ulimwengu kama mimi na mme wangu tulivyo kuwa tunapenda na ndoto yetu ya pamoja.

Kwa upande wake  Padre  Padre Pierluigi Maccalli  katika ushuhuda wake amesema: “Wakati wa kufungwa kwangu, niliishi miaka miwili daima nikiwa mahali palipo wazi, katika jangwa la sahara  na nilikuwa nikilalia mkeka chini ya ardhi na nilikuwa nakunywa maji ambayo nilijua ni ya mafuta, lakini jambo muhimu ambalo sikuwa nalo ni ukosefu wa kuwasiliana”. Nilihisi hili ni jambo muhimu sana ambalo tumeumbwa kwa ajili ya uhusiano na tupo katika mahusiano. Kwa hakika katika wakati ule nilitambua vema kuwa utume ni ubinadamu”.

Na katika ushuhuda wa Padre Christian Carlassare ambaye alipata shambulizi nchini Sudan Kusini, mara baada ya kutangazwa kuwa Askofu, alisema: “washambulizi walipoingia kwenye chumba changu, nilihisi kuwa maisha yangu sasa yanatolewa sadaka na kwa lolote lile ambalo lingetokea muda huo. Nilipoamka nikiwa hospitalini, neno la kwanza lilikuwa ni “msamaha”.  Hili lilitoka ndani ya moyo. Na kiukweli neno hilo liliniokoa dhidi ya hofu na chuki. Lilinipatia uhuru. Leo hii ninatamani kurudi Sudan Kusini, kwa sababu ninamini kuwa uzoefu wangu unaweza kusaidia watu hao kwa namna hiyo walivyogawanyika ili kuweza kushinda vurugu na kuishi kwa uwajibikaji wa uhuru ambao waliupata”.

Kutokana na kwamba bado muda ni kidogo ulio baki kufikia kilele cha tamasha, hata hivyo shughuli za maandalizi zimeanza kwa kasi sana hadi kufikia mwezi Agosti 2022, na ambapo tamasha hili litatanguliwa na mada muhimu ambazo zitakuwa ndizo kitovu cha kweli cha Tamasha la Utume Milano. Katika Nchi yote kuanzia Torentono hasi Sicilia kupita Lombardia, Italia  watafanya uhuishaji katika shule mbali mbali, vile vile haya kwa kufanya watembelene kutoka katika mabara au kwenda katika vijana kwa vijana wa Italia ambao wanaishi katika mabara ya Afrika, Asia, na Amerika ya Kusini. Katika vyuo vikuu wanafunzi watafanya kazi kuhusu utekelezaji wa malengo yaliyokusudiwa ya Ajenda ya 2030 katika nchi za Kusini mwa ulimwengu, shukrani kwa ushirikiano na Vyuo vikukuu vingine vya Italia. Katika parokia zote huko Milano wameweza kutangaza tayari kuhusu ufunguzi wa safu za mkutano tofauti katika kuandaa kilele hiki cha tamasha la Utume.  Katika magereza nne tofauti za Kaskazini mwa Italia, watafanya maabara kuhusu ukarabati wa haki. Katika jimbo Kuu la Milano kwenye monasteri mbali mbali zitafanyika mikesha ya sala.

Tarehe 29 Septemba hadi 2 Oktoba 2022, ndipo Tamasha la kweli litafanyika. Kwa siku  nne kwa namna ya pekee katika eneo la Nguzo ya Mtakatifu Lorenzo, kwenye moyo wa maisha ya kila siku ya Milano, kati ya nyumba ya makumbusho ya kijimbo, na Kanisa Kuu la Kizamani zitafanyika mikutano mbali mbali. Vile vile wamefikiria kufanya hivyo katika ratiba ya kabla ya Tamasha hilo ambalo kwenye tamasha hili inawezakana kuwaunganisha wote  kwa kuchanganya lugha na watu tofauti ili kuwafikia kila rika na umma kuwa ambayo inajulikana katika harakati za kimisionari lakini pia hata kwa ajili ya wote. Anayetaka kujua zaidi anaweza kubonyeza kwenye tovuti ya maandalizi  ya tamasha hilo (www.festivaldellamissione.it) vilevile kwenye mitandao ya kijamii  Facebook, Instagram, Twitter e YouTube.   

26 October 2021, 15:46