Tafuta

Twenda kuhubiri Ulimwenguni kote Twenda kuhubiri Ulimwenguni kote 

Italia:21 Oktoba utafanyika mkesha wa kimisionari na utume wa ad gentes

Kardinali Angelo De Donatis makamu wa Papa, ataongozaia Mkesha katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane, Laterano Roma tarehe 21 Oktoba usiku na kuwabariki wamisionari watakaoondoka kwenda kwenye utume wa watu (missio ad gentes).Shuhuda za wamisionari zitatolewa wakati wa tafakari na sala katika kesha hilo.

Na Sr. Angella rwezaula – Vatican.

Tarehe 21 Oktoba 2021, utafanyika Mkesha wa Kijimbo wa kimisionari na kwa ajili ya kutuma wamisionari kwenda kwenye utume wa kimisionari ( Missio ad gentes). Mkesha huo utaongozwa na Kardinali Angelo De Donatis makamu wa Papa, majira ya usiku, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane, Laterano Roma na wakati wa tukio hilo, Kardinali atawakabidhi na kuwabariki wote ambao wataondoka kwenda kwenye utume wa watu missio ad gentes.  ‘Mashuhuda na manabii’ ndiyo mada itakayoongoza wakati huo muhimu wa tafakari na sala ambapo wanatarajia kuwapo na shuhuda mbili kutoka kwa watawa wawili na familia moja.

Kardinali Angelo De Donatis, Makamu wa Papa jimbo la Roma
Kardinali Angelo De Donatis, Makamu wa Papa jimbo la Roma

Watawa hao ni Sr. Lucia Bortolomasi, wa Shirika la Wamisionari wa Consolata, ambaye anatoa huduma ya kimisionari kwa  miaka 15 huko Mongolia, Sr. Shenhaz Bhatti, wa Shirika la Wamisionari wa Mtakatifu Yohana Antida, ambaye ametoka nchini Afghanistan hivi karibuni kufuatia na kurudi tena katika utawala wa Watalebani na ushuhuda wa tatu  ni wa Mariarita Loporchio akiwa na mtoto wake, ambao wanamkaribisha mkimbizi pamoja na mtoto wake wa umri wa miaka 4. Watakaoongoza maadhimisho hayo ya sala, kwa nyimbp watakuwa ni kwaya mchanganyiko inayojumuisha watawa kutoka nchi mbali mbali na kikundi  cha Parokia ya Mtakatifu Pio X.

Naye Sr Elisa Kidane mwanashirika wa kikomboni  ambaye hivi karibuni amepewa jukumu la kuongoza kituo cha ushirikiano wa kimisionari kati ya Makanisa ya jimbo la Roma amesema “kile wanachotaka kufanya kuishi siku hiyo kitakuwa ni muda wa sala lakini pia hata siku kuu,  wakati mzuri sana utakuwa ule wa kutumwa kwa wamisionari ulimwenguni lakini pia hata ni tunda la safari, iliyoandaliwa kwa muda, na ambayo sio chaguo lisilofaa. Kuondoka daima ni matokeo ya ushuhuda na pia chaguo la wale wanaobaki, kwa sababu mtu anaweza pia kuwa mmisionari  mahali alipo katika mazingira yake mwenyewe, nyumbani, katika parokia, au kazini.

15 October 2021, 15:57