Tafuta

2021.10.15 Ni muhimu kufahamisha umma juu ya Biashara mbaya ya binadamu ambayo leo hii ni jeraha kubwa katika ulimwengu. 2021.10.15 Ni muhimu kufahamisha umma juu ya Biashara mbaya ya binadamu ambayo leo hii ni jeraha kubwa katika ulimwengu. 

Hispania:Mafunzo juu ya"Safari ya maisha yangu"kuhusu biashara mbaya ya binadamu

Baraza la Maaskofu nchini Hispania wamefafanua juu ya mafunzo yanayohusu biashara mbaya ya binadamu kwamba yanajikita juu ya historia za kweli ili kuwezesha umma kuhusika zaidi na kuhamasisha juu ya mada hiyo hasa kwa vijana.Mafunzo hayo yanaongozwa na kauli mbili "safari ya maisha yangu".Papa alisema moja ya majeraha ya uchungu sana katika nyakati zetu ni jeraha la biashara ya binadamu.

Na Sr. Angella rwezaula - Vatican.

Hivi karibuni itaanzisishwa safu za mafunzo katika Kitengo cha Kuzuia Biashara ya Binadamu, kilichomo ndani ya Tume ya Maaskofu kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi nchini Hispania. Mafunzo hayo yanaongozwa na mada ya “Safari ya maisha yangu” kwa malengo ya kutaka kukaribia na kuufahamisha umma juu ya janga hili baya la biashara mbaya ya binadamu iliyopo katika ulimwengu mzima na katika kila nchi kwa ujumla.

Taarifa hizi zimetolewa na Baraza la Maaskofu nchini Hispania wakifafanua kuwa mafunzo  hayo yanajikita juu ya historia za kweli ili kuhusika zaidi na kuhamasisha juu ya mada hiyo hasa kwa vijana.  Safu hiyo ya mafunzo itawakilishwa na Askofu Juan Carlos Elizalde, Rais wa Tume ndogo ya Baraza la maaskofu kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi na Mkurugenzi wa Sekretarieti Marifran Sánchez Vara, mmoja wa waanzilishi wa Mpango huo mnamo tarehe 20 Oktoba 2021 mara tu baada ya Siku ya Ulaya dhidi ya Biashara ya binadamu ambayo kilele chake ni tarehe 18 Oktoba.

“Safari ya maisha yangu ni matokeo ya kazi ya kikundi cha watu ambao wanafanya kazi moja kwa moja na waathiriwa wa biashara ya binadamu, ambao wamekaribishwa na kusindikizwa na taasisi za Kikanisa.  Onesho la mchoro linatoa rangi  mbali mbali na mwanga katika kuongoza mada hiyo na ambayo ni kazi ya kisanii ya Liliana Coronado, mwenye asili ya kutoka Peru ambaye pia ni mjumbe wa kikundi kazi cha wajumbe  kwa ajili ya wahamaji katika jimbo la Jaén. Mpango huo unawakilishana mchakato wa  safari nne unaojikita juu ya uzoefu wa wanawake waathiriwa wa biashara haramu ya binadamu. Na zaidi, wanasaidiwa na shughuli hii kwa ajili ya kujikita kwa undani zaidi na tafakari ya mada ya biashara mbaya ya binadamu kwa shuhuda za kweli.

"Moja ya majeraha ya uchungu sana katika nyakati zetu ni jeraha lililowazi la biashara ya binadamu, mtindo mpya wa mamboleo ya utume ambao unakiuka hadhi, zawadi ya Mungu, kwa kaka na dada wengi sana.” Ni maneno ya Papa Francisko ambayo kwa mujibu wa wahamasishaji, yamekuwa kama injini  kwa  kuzaliwa mpango wa mafunzo hayo, kwa ajili ya vijana zaidi lakini pia itawawezesha wote ambao wanataka kufuatilia kwenye jukwaa la Youtube la Baraza la Maaskofu nchini Hispania.

15 October 2021, 15:39