Tafuta

Uharibifu wa msitu wa amazonia:ukataji hovyo miti, uchomaji moto,kilimo kikubwa cha soya,utupaji wa sumu na vitu vya uharibifu wa msitu huo. Uharibifu wa msitu wa amazonia:ukataji hovyo miti, uchomaji moto,kilimo kikubwa cha soya,utupaji wa sumu na vitu vya uharibifu wa msitu huo. 

Amazonia:imehitimishwa semina huko Belém kwa ushiriki wa Repam

Imehitimishwa Oktoba 23 katika Kampasi ya Chuo Kikuuu cha Pará,Belém,Brazil,semina kuhusu mabadiliko ya tabiachi kuelekea kilele cha mkutano UN huko Glasgow.Mwakilishi wa Repam:“Tutakuwapo Scotland katika mkutano mkuu wa Cop26,Glasgow kuhusu tabianchi,kwa maamuzi na kwa dharura:bila Amazonia hakuna wakati ujao wa ubinadamu".

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Katika kuelekea kwa Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuhusu mabadiliko ya tabianchi, Padre Dario Bossi, Mkuu wa Provinci ya wa Wakomboni nchini Brazil ambaye ni mmoja kati ya washiriki kwa niaba ya Repam (Mtandao wa Kikanisa wa Amazonia) amethibitisha kuwa: “Tutakuwapo huko Scotland, katika mkutano mkuu wa COP26 huko Glasgow kuhusu tabianchi, kwa maamuzi na kwa tabia za dharura na msimamo kwa sababu bila Amazonia hakuna wakati ujao wa ubinadamu”. Amesema hayo katika Semina kuhusu “Amazonia na madiliko ya Tabianchi”, iliyohitimisha Jumamosi tarehe 23 Oktoba 2021 katika Kampusi ya Chuo Kikuu shirikishi cha Pará, huko Belém, mji mkuu wa pili wa Amazoni ya Brazil.

Semina hiyo ilikuwa ni hatua ya kwanza katika kuelekea Jukwaa la Kijamii la Amazonia (Fospa), linalotegemea kufanyika huko Belém mnamo Julai 2022. Katika hati yao kwenye mkutano, imewaelekeza wakuu wa nchi na watu wote wa ulimwengu kwa kusema katika muktadha wa dharura kubwa kwa ujumla ya ongezeko la hali ya joto ambapo,  Amazonia ni kutovu kikuu maji ulimwengu na sehemu kubwa ya msitu wa kutropiki unaendelea wa kisayari kwa uwepo wa zaidi ya watu asilia 300. Msitu huo ni uhai wa msimamo wa hali ya hewa ya ardhi na mashambulizi dhidi ya msitu huo ni mashambulizi ya ubinadamu.

Hati hiyo pia inashutumu matukio mbali mbali yanayoendelea kuongezeka kama vile ukataji hovyo wa miti na uraruaji wa mazingira, kwa sababu ya shughuli za uchimbaji madini, uchomaji hovyo wa msitu, umwagaji sum una vitu vingine vya hatari ambavyo vinatupwa ndani ya maeneno ya msitu. Imefikia wakati kwamba mambo yanafanya uamuzi wanaandika. Washiriki wa semina wamekumbusha kuwa ukataji hovyo wa misitu unahatarisha madhara makubwa ambayo tayari yanaonekana wazi katika bara lote na kusema kuwa: “Huu ni wakati sasa kuacha katu kukata hovyo miti na kuchoma  moto”.Washiriki hao wa semina waomba yawepo mabadiliko ya sera za kisiasa na uongofu wa kweli wa tabia hasa katika nchi kama Brazil na Colombia  kwa kuweka kipaumbele cha kufikiria tena. Ni matazamio yao pia ya kuweza kulinda eneo pia la watu wa asilia.

Padre Bossi amesema kwamba “seminari ilikuwa ya maana sana kwani iliweka pamoja uzoefu tofauti na mikakati kwani kwa upande mmoja, wawakilishi wa watu asilia, waafro, wazalendo na wavuvi, na kwa upande mwingine watu wa kisayanis kama wanabaolojia, wataalam wa mambo ya watu, wataalam wa masuala ya kijamii, na wa mabadiliko ya tabianchi. Kulikuwa na hali ya kutajirishana kati yao kwani walisikiliza karibu uzoefu wa watu 40. Walikusanya kilio cha maskini, lakini pia hata majeraha ya ardhi. Na onesho la mwisho ni kilelezo cha nguvu sana, mbele ya kuweka umakini wa mazingira ambayo mara nyingi yanapitiwa kijuu juu na si kutenda kwa dhati katika ulinzi na utetezi wake.

Kwa mfano Padre Bpsso  amesema ukataji wa miti hovyo na uchomaji ni kama majinamizi makuu ya kuogopesha ambayo yanachocheana, lakini pia hata sababu nyingine kama utupaji wa sum una kilimo kikubwa cha soya kwenye msitu huo. Kwa mujibu wa Padre Bossi, vipaumblele vitatu muhimu katika matazamio ya mkutano wa Cop26 wa Glasgow ni: matendo ya haraka ya kufanya kuisha  kuchoma moto, kusitisha ulimaji na uzalishaji mkubwa kupitia kiasi katika ardhi na kuacha kuharibu Amazonia na mwisho kutambua kazi ya Umbaji kama kitu cha haki na cha kulindwa kwa haki zake.

26 October 2021, 15:35