Shambulizi la kigaidi Ijumaa 3 Septemba katika Supermaket ya Auckland nchini New Zealand Shambulizi la kigaidi Ijumaa 3 Septemba katika Supermaket ya Auckland nchini New Zealand 

New Zeland:Maaskofu walaanishambulizi la kigaidi,Auckland

Maaskofu wa New Zealand wanalaani vikali shambulizi ya kigaidi lililotokea huko Aucland na kuuwa watu sita wasi katika supermarket ya New Lynn, Auckland, Ijumaa tarehe 3 Septemba.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Maaskofu wa Aotearoa huko New Zealand wamelaani vikali shambulizi la kigaidi kwa watu wasio na hatia na kuwaombea marehemu walipoteza maisha yao na wale wote ambao wamejeruhiwa katika tukio hilo ili waweze kupona. Maaskofu wanaonesha masikitiko makubwa na mioyo yao inawakumbuka wote wa whānau, na kwa jumuiya kubwa iliyokumbwa na mkasa huo. Maaskofu wa New Zealand wanaeleza kwamba wanatambua kuwa ugaidi wa kushambulia kila wakati ni kutaka kugawanya jumuiya na kama ilivyo hata kuleta migogoro moja kwa moja wa vurugu binafasi. Vile vile wanatambua kuwa matendo ya kutisha namna hii ni uhalifu. Jumuiya Katoliki ya Aotearoa, New Zealand inasimama kidete kwa imani na mazungumzo kwa watu wote wanaokiri imani yao na wasio, na watu wote kuungana pamoja dhidi ya aina zozote za vurugu, wanaandika maaskofu katika ujumbe wao kwa jumuiya nzima.

Ujumbe wa maaskofu umesainia na Kardinali John Dew, Askofu Mkuu wa Wellington, na msimamizi wa kitume wa Palmerston Kaskazini na rais wa Baraza NZCBC, Askofu Michael Dooley, wa jimbo la  Dunedin, Askofu  Patrick Dunn, wa jimbo la  Auckland, Askofu Michael Gielen, msaidizi wa Auckland, Askofu Stephen Lowe, wa jimbo la Hamilton na katibu wa Baraza la Maaskofu NZCBC Askofu Paul Martin SM, Mwandamizi wa Askofu Mkuu wa Wellington na Msimamizi wa kitume wa Christchurch.

Taarifa za Waziri Mkuu wa Ne Zealand

Kwa mujibu wa tarifa kutoka kwa Waziri Mkuu wa New Zealand amesema Polisi ya nchi hiyo Ijumaa tarehe 3 Septemba imemuuwa kwa kumpiga risasi mshukiwa wa ugaidi, aliyewachoma kisu na kuwajeruhi watu wasiopungua sita ndani ya duka moja kubwa mjini Auckland. Polisi ya New Zealand imesema wateja watano walioshambuliwa na mwanamume huyo ndani ya Supermarket walikimbizwa hospitali wakati wawili kati yao wakiwa hali mahututi. Waziri Mkuu Jacinda Ardern amesema shambulio hilo lilikuwa la kigaidi. Ameongeza kuwa mwanamume huyo ni raia wa Sri Lanka na kwamba alihamasishwa na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu, IS.

Mshukiwa huyo ambaye amekuwa akiishii New Zealand kwa miaka 10 tangu mwaka 2011, alikuwa anafuatiliwa kwa ukaribu na vyombo vya usalama nchini humo. Bi Ardern amesema aliwahi kujulishwa na vyombo vya usalama kuhusu mienendo ya mwanamume huyo, japo hakukuwa na sababu yoyote ya kisheria ya kumkamata. “Kabla ya kutoa fursa ya kujibu maswali, kilichotokea leo hakifurahishi, ni makosa na tukio la chuki. Shambulio hilo lilifanywa na mtu binafsi- sio dini, sio tamaduni wala kabila la mtu bali ni shambulizi la mtu binafsi ambaye alihamasishwa na itikadi kali isiyoungwa mkono na mtu yeyote hapa. Anabeba dhamana yeye binafsi. Huo ndio uhalisia.”

04 September 2021, 10:13