Kila tarehe 6 ya kila mwaka nchini Marekani ni siku ya Wafanyakazi.Maaskofu wameandika ujumebe unaoangazia matatizo ya kijamii. Kila tarehe 6 ya kila mwaka nchini Marekani ni siku ya Wafanyakazi.Maaskofu wameandika ujumebe unaoangazia matatizo ya kijamii. 

Marekani,siku ya wafanyakazi:tuote ndoto iliyo bora ya uchumi

Katika ujumbe wa Baraza la Maaskofu nchini Marekani,kwenye fursa ya Siku ya Wafanyakazi nchini humo ifanyikayo kila tarehe 6 Septemba,kila mwaka, unaangazia matatizo ya kijamii yaliyoongezeka zaidi kipindi cha mwaka na nusu kutokana na dharura ya janga la UVIKO-19.Ujumbe huo una kaulimbiu ‘ndoto ya uchumi uliobora’.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika Siku kuu ya wafanyakazi ‘Labour Day’, ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 6 Septemba nchini Marekani, Baraza la Maaskofu, Marekani wameandika ujumbe wao ambao umeongozwa kauli mbiu ya tafakari ya “ndoto ya uchumi uliobora”. Katika ujumbe huo uliotiwa saini na Askofu Paul Coakley, rais wa Kamati ya Maaskofu kwa ajili ya Haki za ndani na maendeleo ya binadamu, maaskofu wanatazama awali ya yote hali ngumu iliyosababaishwa na janga la UVIKO-19 katika mwaka wa mwisho na nusu na kuwashukuru wafanyakazi ambao wamewezesha nchi yao kusimama tena katika kipindi kigumu sana, na wanaendelea kufanya kazi katika hali ngumu na mara nyingi isiyo hesabiwa. Mawazo yao baadaye yamewaendea wale wote ambao wamepoteza chanzo cha mapato kwa sababu ya dharura ya kiafya, ambayo ni asilimia  47% ya watu wote. Lakini sio tu: ujumbe huo unakumbusha kwamba ‘Covid’ imeongeza uwezekano wa watu kunyonywa, kiasi kwamba, wakati wa janga, maombi ya msaada kutoka kwa wahanga wa usafirishaji haramu wa binadamu yameongezeka kwa asilimia 40. Wenye kuathiriwa zaidi kwa namna ya pekee ni jumuiya za wenye asili ya kiafirika kwa upotezaji wa kazi na mapato na wanawake waliathiriwa hasa.

Kwa wote bila kusahau zaidi ya watu 600elfu waliokufa kwa Virusi vya Uviko-19 nchini Marekani. Takwimu nzito ambazo zinaifanya kuvunja moyo hasa kwa  kutambua kwamba karibu watoto elfu 43 nchini wamepoteza mzazi katika janga hilo na kwamba watoto milioni 13 wanakabiliwa na ukosefu wa chakula,wanaandika maaskofu. Mbele ya kukabiliwa na hali hii ya kustaajabisha, Maaskofu wa Marekani kwa wito wao wanabainisha kuwa ni jambo la dharura zaidi kuliko hapo awali kufikiria uchumi bora na ulimwengu wa kidugu zaidi, ikizingatiwa zana mbili zilizotolewa na Papa: Uchumi wa Francisko. Hii ni, harakati inayoundwa na vijana wajasiriamali na wachumi, ambayo inakusudia kutoa roho kwa uchumi kwa kutengeneza michakato ya ujumuishaji, na  Fratelli tutti yaani Wote ni ndugu ambayo ni maandishi ya Papa  juu ya udugu na urafiki wa kijamii. “Ni jukumu letu, sio tu kutafakari juu ya ubaya wa sasa wa uchumi wetu, lakini pia kujenga makubaliano karibu na utu wa binadamu na faida ya wote, kujibu mwito wa Papa wa kutoa uchumi mpya na ubunifu mapendekezo ya mahitaji ya ubinadamu, ndani na ulimwenguni”, ujumbe unabainisha.

Kwa upande wao Kanisa la Marekani hakika wanasema halisimami na kuangalia tu kwani Askofu Coakley anakumbuka kwamba wakati wa shida hii, parokia za kitaifa, Katoliki na jumuiya zimekuwa visiwa vya huruma katikati ya bahari ya kutokujali na sitnofahamu zaidi. Inatosha kusema kwamba, katika miezi 6 ya kwanza ya janga hili, mashirika ya misaada ya Kikatoliki iligawanya karibu dola milioni 400 za misaada ya dharura pamoja na chakula, vifaa vya kinga binafsi, vifaa vya watoto na makaazi ya karantini kwa wasio na makazi. Sio hivyo tu na wakati wote, maaskofu waliunga mkono mipango ya lishe, kusitisha uhamisho, mapato na msaada wa ajira, hatua za usalama kwa wafungwa na upatikanaji wa huduma za afya.

Pamoja na wanachama wa Bunge walishirikishana  suala kubwa la kisiasa la kupunguza ukosefu wa usawa wa kiuchumi; walisisitiza umuhimu wa kuunda ajira kwa wale ambao ni maskini na wanaotengwa, wakitoa kipaumbele cha kazi za kupangwa na kuendelea kulinda haki za wafanyakazi; na pia waliomba sheria kusaidia familia zinazofanya kazi na kushughulikia mgogoro wa kiikolojia ambao una athari kwa wafanyakazi wote, kwa sababuikiwa watawapuuza maskini na hawaturuhusu maombi yao kugusa mioyo yao, basi matendo yao hayatatosha . Hati ya Baraza la Maaskofu Marekani (USCCB) kwa maana hiyo inahitimisha na maelezo ya matumaini kwamba wakubali kwa pamoja changamoto zinazojitokeza ili kutoka kwenye mgogoro huo na uchumi ambao unafanya kazi kwa watoto wote wa Mungu.  “Janga hili limetupatia uzoefu wa pamoja wa ulimwenguni kote. Tumaini ni kwamba tunaweza kujenga ushirikiano wa kimataifa ambao unashinda ubinafsi na kumaliza udhalimu wa kila mtindo wowote”.

06 September 2021, 16:50