Wanajeshi nchini Mali wakishiriki dharura katika mashindano ya Kimataifa 2021 Wanajeshi nchini Mali wakishiriki dharura katika mashindano ya Kimataifa 2021 

Mali:viongozi wa kidini watoa wito wa amani katika mzozo wa kisiasa,Mali

Udharura wa kuwa na mabadiliko ya serikali ya mpito ya amani,umoja na makubaliano ya amani ambayo viongozi wa dini wa Mali wanatoa wito kwa mara nyingine tena,kwa pande zote zinazohusika ili kufanya kila liwezekanalo kurejesha utulivu wa nchi. unamsihi rais wa mpito,serikali,taasisi zoteza Jamuhuri,asasi za kiraia kuhakikisha kuna serikali ya mpito ya amani.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Udharura wa kuwa na mabadiliko ya serikali ya mpito ya  amani,umoja na makubaliano ya amani ambayo  viongozi wa dini wa Mali  wanatoa wito kwa mara nyingine tena, kwa pande zote zinazohusika ili kufanya kila liwezekanalo kurejesha utulivu wa nchi. Tunamsihi rais wa mpito,serikali,taasisi zoteza Jamuhuri,asasi za kiraia na vyama vya siasa,vikundi vyenye saini,vikosi vyenye silaha,kila mmoja kwa haki yake kuchukua hatua zote ili kuhakikisha kuwa kweli kuna serikali ya mpito ya amani,unaojumuisha na wa kukubaliana.

Bado kuna upepo wa mgogoro nchini Mali, miezi mitatu baada ya mapinduzi ya Mei 24 wakati, kwa amri ya Kanali Assimi Goïta, askari yule yule ambaye alikuwa ameongoza mapinduzi mnamo Agosti 2020, askari wengine wa jeshi walimkamata na kumtimua Kaimu Rais Bah N Daw na Waziri Mkuu Moctar Ouane, wakiwaachilia baada ya siku tatu. Muda mfupi baadaye, Mahakama ya Kitaifa ya Katiba ilimteua Kanali Goita kuwa rais wa mpito. Na kweli ni katika kwa mabadiliko ya mpito huo wa amani, umoja na makubaliano ya amani ambayo  viongozi wa dini wa nchi hiyo wanatoa wito kwa mara nyingine tena, wakitoa wito kwa pande zote zinazohusika ili kufanya kila liwezekanalo kurejesha utulivu wa nchi. Tunamsihi rais wa mpito, serikali, taasisi zoteza Jamuhuri, asasi za kiraia na vyama vya siasa, vikundi vyenye saini, vikosi vyenye silaha, kila mmoja kwa haki yake kuchukua hatua zote ili kuhakikisha kuwa kweli kuna mpito wa amani, unaojumuisha na wa kukubaliana.

Barua iliyoandikiwa tarehe 30 Agosti ambayo  ilisainiwa na Askofu Mkuu wawa Bamako, Kardinali Jean Zerbo, na rais wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mali Cherif Ousmane Madani Hadaira, n na rais wa Chama cha Vikundi vya Kanisa vya Kiinjili nchini Mali, Mchungaji Nouh Ag Infa Yattara. Wakati huo huo, viongozi wa kidini wanahimiza raia wafanye kazi kwa utulivu wa nchi: Tunawaalika watu wa Mali kuchukua hatua ya ujasiri katika imani, kubadili tabia zao na kuhamasisha amani ya kitaifa. Kwa upande wao, viongozi wa kidini wanathibitisha kujitoa kwao kuendeleza utume wetu wa kiroho na uzalendo, kwa ujenzi wa serikali na mafanikio ya mpito.

Akikutana na waandishi wa habari, Kardinali Zebro pia alitangaza kwamba, katika siku chache zijazo, watakuwa na mkutano mamlaka ya mpito ili kusaidia mchakato wa amani nchini. “Tutaanzisha hatua ya utetezi wa maridhiano na serikali na watendaji wa kijamii, vikundi vyenye silaha na jamii ya kimataifa, aliongeza kardinali huyo. Kuna uwezekano pia wa kuandaa Siku ya Kuombea Kuombea Amani. Kwa upande wake, Cherif Madani alikumbuka hitaji la mazungumzo kati ya taifa, kwa sababu hakuna mtu atakayebadilisha Mali kwa Wamaliia. Lazima mazungumzo ya kutafuta suluhisho”. "Wamaliya wanapaswa kushikana mikono kama ndugu, kama watu katika mashua moja , Mchungaji Yattara aliunga mkono kuwa "Hatupaswi kuharibu mtumbwi huu wa kipekee ambao ni nchi yetu, ili hata vizazi vijavyo viweze kukopa kwa amani na utulivu"

02 September 2021, 16:00