2021.09.13 Kongamano la IV la Ekaristi Takatifu nchini Tanzania 9 -12 Septemba. 2021.09.13 Kongamano la IV la Ekaristi Takatifu nchini Tanzania 9 -12 Septemba. 

Kongamono la IV la Ekaristi kitaifa,Tanzania limehitimishwa

Wakati Baba Mtakatifu Francisko alikuwa anafunga Kongamano la 52 la Ekaristi Kimataifa huko Budapest nchini Hungaria,Dominika Septemba 12,ilikuwa sambamba na kufungwa kwa Kongamano la IV la Ekaristi Kitaifa nchini Tanzania.Katika tukio la Tanzania ni pamoja na zawadi ya Monstrance iliyotolewa kutoka kwa Rais Samia Suluhu kutumika kwa kuabudu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Hitimisho la Kongamano la IV la Ekaristi Takatifu Kitaifa nchini Tanzania limekwenda sabambamba na Hitimisho la Maadhimisho ya Kongamano la 52 la Ekaristi Takatifu Kimataifa huko Budapest, nchini Hungaria likiongozwa Visima vyangu vyote vimo kwako” Zab. 87:7. Na kwa upande wa Kongamano la IV la Ekaristi Takatifu Kitaifa nchini Tanzania limeongozwa na kauli mbiu “Ekaristi Takatifu chemchemi ya uzima wetu”. Baba Mtakatifu Francisko katika ziara yake ya kitume, kituo chake cha kilikuwa ni kuanza kufunga kongamano hilo lililoanza tarehe 5-12 Septemba 2021, huko Jimbo kuu la Esztergom-Budapest, nchini Hungaria. Katika mahubiri yake Papa Francisko alisistizia juu ya msalaba na kwamba Msalaba wa Kristo Yesu Ni Nguzo ya Wokovu wa Binadamu. Msalaba wa Kristo Yesu utakuwa ni chemchemi ya matumaini mapya kwa watu wa Mungu ndani nje ya Hungaria kwa sasa na kwa siku za usoni.

Katika maadhimisho ya Sherehe zote nchini Tanzania yalifanyika katika Kituo cha Hija ya Huruma ya Mungu Kitulizo cha Moyo, kuanzia tarehe 9 hadi Jumapili 12 Septemba 2021.  Katika tukio hilo  huko Tabora  matukio yalikuwa ni ya kina kwani kuanzia Alhamisi tarehe 9 Septemba 2021 asubuhi, ilifanyika maadhimisho ya Kutabaruku Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu. Katika ibada hiyo iliongozwa na Askofu mkuu Paul Runangaza Ruzoka wa Jimbo kuu la Tabora. Wakati jioni kulikuwa na Masifu ya Jioni, Kuabudu Ekaristi Takatifu na Mkesha, ambapo ibada hiyo iliongozwa na Askofu Joseph Roman Mlola, ALCP/OSS, wa Jimbo Katoliki la Kigoma.

Zawadi ya Monsrance iliyotumwa na Rais Samia H.Suluhu wa Tanzania kwa tukio la Kongamano
Zawadi ya Monsrance iliyotumwa na Rais Samia H.Suluhu wa Tanzania kwa tukio la Kongamano

Ijumaa tarehe 10 Septemba 2021, Askofu Flaviani Matindi Kassala, Makamu wa Rais Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania aliadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya ufunguzi wa Kongamano la IV la Ekaristi Takatifu Kitaifa nchini Tanzania. Wakati wa mahubiri yake Askofu Kasala akitafakari somo la kwanza alijikita juu ya uhusiano na Mungu kwa kutazama sura ya mfalme daudi aliyetaka kumjenga nyumba kwa kutaka kurudisha hisani kwa mwenyezi Mungu kwa yote aliyotendewa. Kila mcha Mungu anaweza kufikia busara kwa mtu aliye na haki. Katika tukio hilo, Rais Samia Suluhu Hassan alituma zawadi ya Monstrance ili iweze kutumika kwa ajili ya kuabudu wakati wa Kongamano la Ekaristi.  Zawadi hiyo iliwakilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.

Zawadi ya Monsrance iliyotumwa na Rais Samia H.Suluhu wa Tanzania kwa tukio la Kongamano
Zawadi ya Monsrance iliyotumwa na Rais Samia H.Suluhu wa Tanzania kwa tukio la Kongamano

Kati ya mada walizojikita nazo katika Kongamano la ekaristo takatifu ni pamoja na  Historia ya Makongamano ya Ekaristi Takatifu. Ekaristi Takatifu na Mtakatifu Yosefu na Bikira Maria. Ekaristi Takatifu na Maandiko Matakatifu. Zab 87:7. Mada nyingine ni Katekesi Kuhusu Ekaristi Takatifu, Ibada ya Upatanisho na Maungamano. Ekaristi Takatifu na Liturujia ya Kanisa. Historia ya Ukristo/Ukatoliki na Changamoto zake katika mchakato wa uinjilishaji Kanda ya Magharibi. Kongamano la IV la Ekaristi Takatifu Kitaifa nchini Tanzania linanogeshwa na Ibada ya Kuabudu Ekaristi Takatifu, Sala za Kanisa, Sakramenti ya Upatanisho pamoja na Katekesi.

Jumamosi tarehe 11 Septemba 2021 Ibada ya Misa Takatifu kwa Heshima ya Bikira Maria ilongozwa na Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwa’ichi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, ambapo kwa  jioni Askofu Simon Chibuga Masondole wa Jimbo Katoliki la Bunda aliongoza Ibada ya Kuabudu Ekaristi Takatifu, Rozari na Kutoa Tafakari. Katika kilele cha siku ya kuhitimisha Kongamano la IV la Ekaristi Takatifu Kitaifa Dominika tarehe 12 Septemba  ibada ya Maandamano ya Ekaristi Takatifu iliongozwa na Askofu Beatus Christian Urassa, ALCP/OSS, wa Jimbo Katoliki la Sumbawanga pamoja na Askofu Msaidizi Prosper Lyimo wa Jimbo kuu la Arusha.  Askofu mkuu Paul Runangaza Ruzoka wa Jimbo kuu la Tabora aliongoza Ibada ya Misa Takatifu ya Kufunga maadhimisho haya.

14 September 2021, 17:00