Papa Francisko akitoa Biblia kwa watu mbali mbali kwa ajili ya uenezi wa Neno la Mungu. Papa Francisko akitoa Biblia kwa watu mbali mbali kwa ajili ya uenezi wa Neno la Mungu. 

Afrika:makatekista wa Afrika ni sehemu msingi ya jumuiya ndogo ndogo

Makatekista wanapaswa kuwa ni mashuhuda wa imani na walimu wanaofundisha kwa niaba ya Kanisa.Yote haya yanaweza kutekelezwa kwa njia ya sala, masomo na ushiriki wa moja kwa moja katika maisha ya jumuiya yanayoweza kukuza utambulisho na uwajibikaji wake wote.Ni sehemu ya Barua binafsi ya Papa Francisko Motu Proprio“Antiquum ministerium.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Padre wa Kimisionari wa Shirika la Kimisionari la Afrika (SMA), Walter Maccalli akizungumza na Shirika la habari za kimisioanri Fides alikuwa ameeleza ni kitu gani katekesia katika Kanisa la Afrika anafanya, akigusia juu ya Barua binafsi ya Papa Francisko Motu Proprio “Antiquum ministerium” ya Utume wa Katekista. iliyochapishwa mnamo tarehe 10 Mei 2021. Katika ushuhuda wake Padre huyo alisema “Barani Afrika nisingeweza kutoa huduma yangu ya kimisionari kikamilifu bila msaada wa makatekista wengi”.  Katika   Barua yake Binafsi ya Papa Francisko "Motu Proprio", "Antiquum ministerium" yaani “Huduma ya kale” ilikuwa ndiyo inaanzisha rasimi Huduma ya Katekista ambayo msingi wake umepitia karne nyingi za kale na kuendelea hadi leo hii.

Padre Maccalli alisema makatekista ndio mahali pa mrejesho kwa Wakristo katika jumuiya ndogo ndogo zilizoundwa, kwa kuwa wanaishi karibu nao na huhuisha maadhimisho ya ibada za Neno la Mungu kila Dominika wakati wamisionari au Maparoko hawawezi kufanya hivyo kutokana na umbali wa maeneo na ukubwa na wakati wachungaji hawatoshi. Padre huyo alitoa mfano nchini Angola, kuwa “wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyo dumu muda mrefu makatekista kila wakati walibaki mahali pao, hata wakati makuhani na watawa walilazimika kuacha utume wao kwa sababu za usalama wao. Walitoa uthibitisho wa imani yao, licha ya hatari na mateso”, alisisitiza Padri Maccalli. Aidha alisema kuwa hawa hawakuacha kazi ya uinjilishaji, waliendelea kutoa malezi na msaada wa Kikristo kwa waamini, hata katika hali mbaya, katika vijiji vilivyojitenga na kuwa msituni, katika vitongoji vya waliokimbia makazi yao, au katika kambi za wakimbizi ng'ambo ya mipaka ya Angola.

Kama ushuhuda wa jukumu lisiloweza kubadilishwa la katekista, mmisionari wa SMA alikumbusha mmoja wapo, wa nchi hiyo anayeitwa Estêvão Tomais, aliyezaliwa miaka miwili kabla ya 1961, mwaka ambao vita vya ukombozi vya Angola vilianza. “Alikusudiwa kuawa kwa sababu alikuwa chotara. Hii ni kwa sababu baba yake alikuwa Mreno. Aliokolewa na mama yake wa Angola, aliyekimbilia msituni. Katekista kwa wito na kuwajibika kwa jumuiya zilizotawanyika katika parokia kubwa ya Nambuangongo, na ambaye amekuja kuwa mshirika mwaminifu wa wamisionari.  Hata leo hii yeye ni kiongozi wa kufundisha viongozi wapya wa jumuiya ndogo ndogo, anafundisha liturujia na namna ya kufafanua Biblia. “Kanisa Katoliki la Angola lina deni kubwa kwa makatekista kwa mchango mkubwa ambao wamefanya katika uinjilishaji kwa miaka arobaini ambayo vita vilidumu, alithibitisha Padre Walter.

Muktadha wa maneno ya mkatekista wa kiafrika kwa Wakristo na jumuiya zao ni kubwa kuliko ule wa wamisionari wa Ulaya. Kama mjuzi wa tamaduni na mila mahalia, neno lake Katekesta ni kichocheo na kitia moyo ili kuishi imani ya Kikristo katika hali hizo ambazo Injili inajikita na mazoea na akili za mababu. Makatekista wanajua jinsi ya kuunganisha mambo mengi mazuri ambayo yapo katika mila za Kiafrika na mapya ya tangazo la Yesu. Miongoni mwa huduma mbali mbali zinazotolewa, na makatekita: huandaa wakatekumeni ambao ni watu wazima kwa ajili ya Ubatizo, hufanya huduma ya kusafiri katika vijiji, katekesi na liturujia katika lugha ya kienyeji, pia kusaidia kurejesha amani katika familia na vijiji ambavyo mizozo mara inapotokea kwa maana hiyo tunaweza kuthibitisha kwamba uzuri ndiyo ukweli wa njia za uunjilishaji wa dhati na zaidi kwa makatekista ambao kwa wanahudumia Kanisa mahalia kwa shauku kubwa.

Kwa uthibitisho huo, barua binafsi ya Papa “Antiquum ministerium” kuhusu Utume wa Katekista inastitiza suala hilo: “Makatekista wanaitwa kuwa ni wataalamu na wahudumu wa jumuiya ya waamini katika kutangaza, kushuhudia na kurithisha imani katika hatua mbalimbali. Waanzie hatua ya kwanza ya kutangaza Injili, “Kerygma”, kufundisha maisha mapya katika Kristo Yesu sanjari na kuwandaa waamini kwa ajili ya kupokea Sakramenti za Kanisa na hatimaye, kuendelea na majiundo endelevu ili kila mwamini aweze kuwa tayari siku zote kumjibu kila mtu anayemuuliza habari za tumaini lililo ndani mwake; lakini kwa upole na kwa hofu.  (taz. 1Pet.3:15). Makatekista wanapaswa kuwa ni mashuhuda wa imani, waalimu, wandani wa imani na walimu wanaofundisha kwa niaba ya Kanisa. Yote haya yanaweza kutekelezwa kwa njia ya sala, masomo na ushiriki wa moja kwa moja katika maisha ya jumuiya yanayoweza kukuza utambulisho na uwajibikaji wake wote.

03 September 2021, 15:08