Rais Hichilema wa Zambia ameombwa na Caritas Zambia kutoa kipaumbele cha kilimo endelevu na kulinda haki za wakulima Rais Hichilema wa Zambia ameombwa na Caritas Zambia kutoa kipaumbele cha kilimo endelevu na kulinda haki za wakulima  

Caritas Zambia imeomba Rais kutoa kipaumbele cha kilimo endelevu&kutetea haki za wakulima

Caritas nchini Zambia imemwomba Rais Hichile kutoa kipaumbele cha kilimo endelevu na kulinda haki za wakulima.Kuhusu shida ya deni la taifa,Caritas inaomba serikali mpya kwa wazi zaidi na kuhusika zaidi katika Bunge.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kukuza sera endelevu ya kilimo mara moja na kuzingatia haki na maslahi ya wakulima wadogo. Hiki ndicho kipaumbele kilichooneshwa na Caritas Zambia kwa Rais mpya Hakainde Hichilema, ambaye alishinda uchaguzi mnamo Agosti 12 iliyopita. Kujikita kwa kina kama chanda na pete  inayodumisha mazingira, kushinda mitindo ya kilimo cha viwandani kulingana na utumiaji wa kemikali, itasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na wakulima wadogo, kwa mujibu wa barua kutoka shirika Katoliki ambalo linabainisha kuwa kilimo kinachoheshimu mazingira pia ni rahisi na huunda ajira.

Rais Hichilema akihutubia Taifa baada ya kuapishwa
Rais Hichilema akihutubia Taifa baada ya kuapishwa

Caritas Zambia baadye  imesisitiza hitaji la sera na sheria inayolinda mbegu za asili na mifumo ya chakula kupunguza nguvu nyingi za mashirika ya kimataifa ambayo yanaamuru sheria za soko kwenye uuzaji wao. “Mbegu hizi ni zawadi kutoka kwa Mungu na ni za wakulima wetu ambao wamezipitisha kutoka kizazi hadi kizazi” barua hiyo inasisitiza. Kwa mujibu wa Caritas pia ilimwomba Rais mpya kutekeleza Azimio la Maputo juu ya kilimo na usalama wa chakula. Hati hiyo iliyosainiwa mnamo 2003 inawapa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika kuwekeza angalau 10% ya jumla ya mgawanyo wa bajeti zao za kitaifa katika sekta ya kilimo. Kwa maana hii, ombi la shirika la misaada kuwekeza kidogo katika shughuli za uchimbaji madini, ambazo zinawakilisha sekta ya kuendesha uchumi wa Zambia, kwa niaba ya kilimo.

Rais Hichilema akiwapungia umati wa watu mkono
Rais Hichilema akiwapungia umati wa watu mkono

Ujumbe huo pia unaonesha wasiwasi juu ya Mpango wa Kusaidia Wakulima wa sasa (Fisp) ambao umenufaisha kampuni kubwa na waamuzi badala ya wazalishaji. Kinachohangaisha Caritas ni Programu ya Kitaifa ya Kumiliki Ardhi (Nltp), mpango uliozinduliwa na serikali iliyopita ambayo inatoa uuzaji wa ardhi kwa watu binafsi, kwa hatari ya jamii za wenyeji na maskini zaidi. Kuondoa jumuiya hizi kutoka katika ardhi yao inaonya Caritas kuwa itasaidia tu kuunda mvutano mpya wa kijamii. Mpinzani wa kihistoria wa Rais anayemaliza muda wake Edgar Lungu, Hichilema, kiongozi wa Chama cha Umoja na Maendeleo ya Kitaifa (Upnd), alishinda uchaguzi wa urais kwa tofauti kubwa, baada ya kampeni ya uchaguzi iliyooneshwa na mvutano mkali, na akaanza kazi rasmi mnamo 24 Agosti. Mbele yake ana changamoto ya kufufua uchumi mbaya wa nchi uliopondwa na madeni ambayo tangu mwaka jana hayajaweza kulipa tena. Baada ya zaidi ya muongo mmoja wa ukuaji wa uchumi ambao mnamo 2011 uliileta Xambia kuwa nchi ya kipato cha kati, uchumi wa Zambia kwa kweli umepata kushuka kwa kasi ambayo janga la Covid-19 lilichangia.

Ongezeko la bei ya shaba ulimwenguni, ambayo ni mzalishaji wa pili kwa ukubwa ulimwenguni, na kupunguza hatua za kuzuia dhidi ya janga katika sehemu ya mwisho wa  2020 kumeruhusu kupona kidogo, ingawa mfumuko wa bei umefikia kiwango cha juu cha 22% mwezi Februari mwaka huu. Kuhusu shida ya deni, Caritas inaomba serikali mpya kwa uwazi zaidi na kuhusika zaidi kwa Bunge.

30 August 2021, 15:29