Askofu Eduardo Hiboro Kussala wa Tombura-Yambio, Sudan Kusini Askofu Eduardo Hiboro Kussala wa Tombura-Yambio, Sudan Kusini  

Sudan Kusini:Mwanga kidogo kuonekana katika mzozo wa Tombura

Anayeridhika na matokeo hayo ni rais wa Baraza la kidini kwa ajili ya Amani Askofu Eduardo Hiiboro Kussala wa jimbo Katoliki la Tombura-Yambio.Kwa mujibu wake kiongozi huyo amesema kwamba ushirikiano wao ni baraka. Walikutans pamoja kama familia kubwa kujadili mambo ambayo yanayowasumbua pamoja,hasa shida ya ukosefu wa usalama na kuzungumza juu ya amani ambayo hawawezi kuifikia peke yao lakini kwa pamoja.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kuna aina ya mwanga kidogo unao anza kujitokeza katika mzozo ambao umezuka hivi karibuni katika kata ya Tombura, katika serikali ya Sudan Kusini ya Ikweta ya Magharibi, eneo ambalo limekuwa uwanja wa mapigano makali ya kijamii tangu tarehe 19 Juni na ambayo yamelazimisha maelfu ya watu kukimbia. Baada ya mito mingi kutoka kwa viongozi wa kidini wa kukomesha vurugu hizo, Uwakilishi kutoka Baraza la Kidini  kwa ajili ya Amani huko Magharibi mwa Ikweta ulikutana na gavana wa serikali na maafisa wengine wa serikali za mitaa ili kujadili utatuzi wa mzozo huo. Viongozi wa kidini na wawakilishi wa serikali walijadili hasa juu ya jinsi gani ya kufanya kazi pamoja kutuliza mkoa na kusaidia wakimbizi wa ndani waliosababishwa na vurugu. Gavana Alfred Futuyo amewapatia uhuru Baraza la Dini kwa ajili ya kuandaa mkutano wa amani.

Hata hivyo kuridhika na matokeo ya mkutano kulioneshwa na rais wa Baraza hilo, Askofu Eduardo Hiiboro Kussala wa jimbo Katoliki la  Tombura-Yambio. Kwa mujibu wake kiongozi huyo amesema: “Ushirikiano wetu ni baraka. Tulikutana pamoja kama familia kubwa kujadili mambo ambayo yanatusumbua pamoja, hasa shida ya ukosefu wa usalama, na kuzungumza juu ya amani ambayo hatuwezi kuifikia peke yake lakini kwa pamoja”. Mwenye kauli sawa na hiyo pia ni askofu Samuel Peni ambaye alisema anashukuru kwa umoja huu wa kusudi: “Makanisa na Serikali wanahudumia jumuiya moja na kufanya kazi pamoja na ni maendeleo makubwa. Kukutana hapa leo kujadili shida na jinsi ya kushughulikia mzozo ni jambo kubwa na tunaomba kwamba Mungu atupe baraka zake na alete amani huko Tombura na Ikweta yote ya ya Magharibi.”

Ikumbukwe kwamba vurugu katika eneo hilo zilitokea mnamo Juni 19 baada ya upigaji risasi, uporaji na uharibifu uliofanywa na watu wenye silaha wasiojulikana dhidi ya vijiji kadhaa. Mgogoro huo ulisambaa hata katika jamii ya Azande na Balanda hadi mji wa Yambio na kusababisha zaidi ya watu 21,000 waliohama, nusu yao wakiwa watoto. Mnamo Julai 22, viongozi Katoliki, Kianglikana, Kilutheri, Pentekoste na Kiislamu walikusanyika pamoja katika Baraza la Kidini la Mpango wa Amani huko Magharibi mwa Ikweta ambao walikuwa wameanzisha ombi la kusitisha mapigano mara moja na kukomesha vurugu zinazoelezewa kama “zisizo na akili” na  iongozi wa pande zote kuwajibika. Askofu Kussala pia alizungumzia vurugu zisizo na maana, ambaye katika wiki za hivi karibuni amehamasisha parokia za jimbo la Tombura-Yambio kusaidia wakimbizi wa ndani. Hali hiyo inaonekana kuwa imerudi katika utulivu kwa takriban siku kumi baada ya kupelekwa vikosi vya usalama katika eneo hilo.

Vurugu huko Magharibi mwa Ikweta ni mojawapo ya mizozo mingi nchini Sudan Kusini ambayo inatishia mchakato mrefu na wa kuchosha wa amani ulioanzishwa mnamo tarehe 12 Septemba 2018 na Mkataba wa Addis Ababa (Mkataba uliofufuliwa juu ya Utatuzi wa Migogoro huko Sudani Kusini - R -Arcss) baada ya miaka mitano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ukosefu wa usalama unaoendelea, pamoja na hali ya shida ya uchumi iliyozidishwa zaidi na janga la Uviko-19, inachangia kuzidisha mivutano nchini.

02 August 2021, 15:56