Sierra Leone ni nchi tajiri ya almasi na madini mengine ya thamani na ambayo uchimbaji wa madini unachukua zaidi ya asilimia 80 ya mapato ya nchi yote kutokana na mauzo kwenda nje lakini wakazi hawafaidiki nayo.. Sierra Leone ni nchi tajiri ya almasi na madini mengine ya thamani na ambayo uchimbaji wa madini unachukua zaidi ya asilimia 80 ya mapato ya nchi yote kutokana na mauzo kwenda nje lakini wakazi hawafaidiki nayo..  

Sierra Leone:Utajiri mkubwa wa maliasili,ufisadi na umaskini

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Caritas nchini Sierra Leone amesema ushuru wa haki unahitajika kwa mataifa na kimataifa na uwazi zaidi katika usimamizi wa utajiri wa nchi zao.Hii ni kutokana na kwamba utajiri mkubwa wa maliasili,ufisadi na umaskini vimekuwa majeraha makubwa barani Afrika na nchi za Kusini mwa Ulimwengu.Kuepukwa kwa ushuru kwa mashirika ya kimataifa ni shida ulimwenguni inayoathiri mataifa yote maskini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Utajiri mkubwa wa maliasili, ufisadi na umasikini, ni mambo matatu ambayo yamekuwa yakiwika katika bara la Afrika na katika nchi nyingi kusini mwa ulimwengu. Hii ni pamoja na nchi ya Sierra Leone, nchi tajiri ya almasi na madini mengine ya thamani na ambayo uchimbaji wa madini unachukua zaidi ya asilimia 80 ya mapato ya nchi yote kutokana na mauzo kwenda nje. Walakini, ni mashirika ya kimataifa ya madini yanayofaidika, shukrani kwa mifumo ambayo wanapata njia ya ukwepaji  ya ushuru na mapungufu ya udhibiti kwa madhara ya idadi ya watu! Hali hii ilijadiliwa katika semina ya utafiti ya “Hazina iliyiozikwa” Kampuni za Uchimbaji Madini zimejificha Ulimwenguni Pote”, ulioandaliwa na kufanyika wiki iliyopita jijini Freetown na chama cha wanawake cha Uchimbaji wa Madini nchini Sierra Leone. Katika kiini cha mkutano huo kulikuwa na ripoti iliyochapishwa na Oxfam-Australia kuhusu mali zilizofichwa ulimwenguni na kampuni kubwa za madini kwa sababu ya kuepukana na ushuru katika nchi ambazo zinafanya kazi, kwa kuzingatia nchi ya Sierra Leone. Mkurugenzi wa Caritas Kitaifa, Padre Peter Konteh, aliweza kuzungumza katika semina hiyo, huku akisisitiza kwamba kuepukwa kwa ushuru kwa mashirika ya kimataifa ni shida ya ulimwengu inayoathiri mataifa yote ulimwenguni, lakini imezidishwa nchini Sierra Leone na usimamizi wa idhini ya madini ambao una hatari kubwa za ufisadi.

Ripoti ya Oxfam-Australia ilibainisha kuwa mnamo 2013 pekee yake faida ya dola trilioni 8 zilifichwa kutoka mamlaka ya ushuru ulimwenguni; na hii inamaanisha kuwa, kwa wastani, kila nchi ilinyimwa dola bilioni 190 kwa mwaka katika mapato ya ushuru. Kati ya hizo, bilioni 15 zimeibiwa kutoka bara la Afrika. Kulingana na ripoti huyo tangu 2009 hadi 2016 nchini Sierra Leone ilikusanya faida ya jumla ya fedha inayokadiriwa kuwa dola milioni 40, jumla inayotosha kuhakikisha huduma ya bure ya afya kwa mwaka mmoja kwa zaidi ya wanawake na watoto 67,000 nchini Sierra Leone kwa muktadha wa Mpango wa Huduma ya Afya. Iluka Resources, ambayo ni kampuni inayoongoza ya madini ya Australia ambayo inadhibiti moja ya migodi inayoongoza kudhibiti madini ya zirconi nchini, inalipa asilimia 0.4 tu ya ushuru kwa mapato yake na imekusanya mkopo wa ushuru wa dola milioni 500.

Mbele ya kukabiliwa na hali hii, iliyosababishwa hata zaidi na mgogoro wa Covid-19 ambao ulipunguza sana mapato ya ushuru wakati wa kuongezeka kwa gharama za kiafya na kijamii, kwa mujibu wa Padre Konteh, ni haraka kuunda mfumo wa ushuru ulio wazi, haki na ujumuishaji. Kwa maneno halisi, ni suala la kuondoa mikunjo hiyo ya mfumo wa ushuru unaotumiwa na mashirika ya kimataifa ili kuepuka kulipa sehemu yao ya ushuru, lakini pia kwa usimamizi wa uwazi wa umma wa makubaliano na mapato ya ushuru kutoka kwa sekta ya madini. Kwa njia hiyo, alihitimisha mkurugenzi wa Caritas, kwamba “tutaweza kuleta hazina ambayo Mungu alitupatia wakazi wa Sierra Leone na kwamba kampuni za madini zinatuficha”.

Nchini Sierra Leone ambayo zamani ilikuwa chini ya ukoloni wa Uingereza, imekuwa mhusika mkuu wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya umwagaji damu tangu 1991 hadi 2002 ambavyo vilisababisha vifo vya watu wasiopungua 50,000. Shukrani kwa rasilimali yake kubwa ya madini, uchumi wa eneo hilo umepona, lakini unaendelea kuteseka kutokana na uharibifu wa mzozo mrefu wa wenyewe kwa wenyewe, na pia majanga ya asili ya mara kwa mara. Mbali na hiyo kumekuwa na janga la UVIKO-19 kwa mwaka wote wa 2020 ambalo limepelekea kushuka kwa mapato ya madini. Mapato ya madini yalipungua kutoka $ 2.24 milioni mnamo mwezi Aprili 2019 hadi $ 0.33 milioni tu mnamo Aprili 2020, kwa maana hiyo 85% ilipungua mwaka hadi mwaka.

03 August 2021, 15:16