Askofu Mkuu Kaigama wa Abuja, Nigeria Askofu Mkuu Kaigama wa Abuja, Nigeria 

Nigeria:maskini hauhalalishi vurugu au uhalifu.Fuata Injili ya Yesu sio ya utajiri

Kuna mamilioni ya Wanigeria ambao wamepoteza matumaini ya kupata chakula chao cha kila siku kwa sababu ya ukosefu wa ajira,walakini hii haidhibitishi vitendo vya uhalifu au vurugu ambavyo vinatishia shughuli za kibiashara au kilimo na kuishi kwa amani.Ni onyo kutoka kwa Askofu Mkuu Kaigama wa Abuja,ambaye Jumapili Mosi Agosti alizungumza kwa mara nyingine tena hali ngumu ya kijamii nchini Nigeria.

Na Sr. Angela Rwezaula –Vatican.

Shida nyingi zinazoikabili Nigeria leo hii hazitatuliwi na vurugu au kwa kufanya uhalifu, lakini zinahitaji majibu ya haraka kutoka kwa serikali. Kwa kifupi, ndiyo onyo lililotolewa na Askofu Mkuu Ignatius Kaigama wa Abuja, Nigeria, ambaye Jumapili tarehe Mosi Agosti alizungumza kwa mara nyingine tena  hali ngumu ya kijamii nchini humo. Mgogoro wa kiuchumi uliosababishwa na janga la UVIKO-19 kiukweli umechangia kuongezeka kwa uhalifu na ukosefu wa usalama katika jamii ya Nigeria, ambayo kwa miaka kadhaa tayari inakabiliwa na tishio la ugaidi wa Boko haramu na bila kutuliza kabisa mivutano ya kikabila.

Jumapili hiyo Askofu Mkuu Kaigama alisema kuwa “Kuna mamilioni ya Wanigeria ambao wamepoteza matumaini ya kupata chakula chao cha kila siku kwa sababu ya ukosefu wa ajira”, walakini alionya kuwa hii haidhibitishi vitendo vya uhalifu au vurugu ambavyo vinatishia shughuli za kibiashara au kilimo na kuishi kwa amani”. Kulingana na Askofu Mkuu Kaigama, hata hivyo amesisitiza kuwa ni muhimu kutumia njia zote za amani huku akihimiza serikali kufanya kile kinachohitajika, kwa kuiga mfano wa watu wa Kiyahudi wanaomfuata Musa aliyetajwa katika Kitabu cha Kutoka katika masomo ya siku. Serikali, kwa upande wake, lazima itoe majibu kwa wakati ili kuzuia watu maskini zaidi kushinikizwa katika shughuli haramu au za uhalifu. Miongoni mwa vipaumbele vitakavyoshughulikiwa, Askofu Mkuu wa Abuja alionesha kuondolewa kwa ufisadi kwamba inaweza kunguza rasilimali za nchi

Akizungumzia Injili ya siku hiyo, kuhusu “Yesu, Mkate wa Uzima”, Askofu Mkuu Kaigama aliwasihi Wanigeria kushukuru kwa baraka ambazo wanapokea na sio kulalamika sana juu ya ugumu wa wakati huu, akionya juu ya mwelekeo fulani  unaokua kuhusu uhusiano wa mtu na Mungu katika maadili, ambayo yanasukuma watu zaidi na zaidi kuhamia dini moja kwenda nyingine. Askofu Mkuu alisema kuwa urafiki wao na Bwana lazima uzingatie shauku yao ya kweli ya kumtumikia, na sio mali ya vitu anavyoweza kuwapatia. Askofu akiendelea emeongeza kusema kuwa "badala yake wengi wanataka Mungu mnganga wa kienyeji, kwa maana hiyo haishangazi kwamba leo hii Wakristo wengi huwa wanaepuka wahubiri hao ambao husema ukweli juu ya maadili ya kweli ya kiinjili, kama vile utu wa kazi, uaminifu, haki, ukweli, maadili, toba, upendo. Wao wanapendelea wale wanaouza Injili ya utajiri”. Kutokana na mahubiri hayo akihitimisha Askofu Mkuu Kaigama alitoa mwaliko wa kuwa daima na shukrani kwa kile ambacho wanapokea na si kumfuata Yesu tu kwa ajili ya mambo ambayo hayadumu. “Mfuateni kwa sababu mnampenda na mnataka kumtambua kwa kina upendo huo, huku mkikua na kumwelewa vizuri”.

04 August 2021, 14:55