Licha ya matatizo yake, bara la Afrika pia ni bara lenye nguvu kubwa ya kiroho,ambayo Watu wa Mungu waliowekwa wakfu na walei wanashiriki kikamilifu Injili kwa furaha ambayo inapaswa hata kuwa mfano kwa wote. Licha ya matatizo yake, bara la Afrika pia ni bara lenye nguvu kubwa ya kiroho,ambayo Watu wa Mungu waliowekwa wakfu na walei wanashiriki kikamilifu Injili kwa furaha ambayo inapaswa hata kuwa mfano kwa wote. 

Marekani:Makusanyo ya sadaka ya mwaka kwa ajili ya Kanisa Afrika

Hata mwaka huu,Baraza la Maaskofu nchini Marekani(Usccb)kupitiaTume maalum ya Baraza hilo inayoshughulikia kusaidia mipango ya kichungaji kwa ajili ya Maendeleo ya Kanisa Barani Afrika,hasa masuala ya vijana,shule katoliki,mafunzo ya wakleri na walei na kuhamasisha amani katika maeneo yenye mizozo wameanza kukusanya mchango mwezi Julai na kuendelea na Agosti kwa utamaduni wa kila mwaka.Mpango uliozinduliwa 2004.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kanisa nchini Marekani kiutamaduni linajikita kwa mwezi wa Julai na Agosti kwa ajili ya mshikamano na Afrika. Hata mwaka huu, waamini katoliki wamealikwa kutoa mchango wao  kwa ukarimu katika mkusanyo kwa lengo hili la kila mwaka la kusaidia mahitaji ya Kanisa mahalia barani Afrika. Anayeratibu mpango huo uliozinduliwa mnamo 2004 ni Tume maalum ya Baraza la Maaskofu Marekani (Usccb) inayoshughulika kusaidia mipango ya kichungaji kwa ajili ya Maendeleo ya Kanisa Barani Afrika, kwa namna ya pekee masuala ya vijana, shule katoliki, mafunzo ya wakleri na waleo na kuhamasisha amani katika maeneo yenye mizozo. Ufadhili wa Mfuko wa kusaidia Kanisa katika utume wake wa kupeleka mbele matumaini, kusaidia uelewa na kuponesha watu ndani ya bara la afrika na kusaidia kueneza Habari Njema ya upendo na huruma ya Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. Amesema hayo Kardinali Joseph Tobin, Mwenyekiti msaidizi wa Tume hiyo kwa kusisitiza umuhimu wake na wa kudumu wa ukarimu wa wakatoliki wa Marekani kuhusu maisha ya kaka na dada wa Afrika.

Ni umaskini wa kuenea, majanga ya kiekolojia, utawala duni, mizozo isiyo na mwisho na uhamishaji mkubwa wa idadi ya watu unaoendelea kulitesa bara kubwa, ambalo linabaki kuwa moja ya maeneo yaliyotengwa sana kisiasa na kiuchumi duniani. Lakini Kardinali Tobin amesisitiza kuwa, “Afrika pia ni bara lenye nguvu kubwa ya kiroho, ambayo Watu wa Mungu waliowekwa wakfu na walei wanashiriki kikamilifu Injili kwa furaha ambayo inapaswa hata kuwa mfano kwetu sisi wote kufanya hivyo”.

Michango kutoka kwa Wakatoliki wa Marekani kwa maana hiyo wao  hutoa rasilimali za msingi ambazo Kanisa mahalia linahitaji kwa ajili ya utume wake wa kichungaji, kuimarisha imani ya watu wake, kuinjilisha, kuimarisha uongozi wake na kukuza amani na haki”. Kila dola inayotolewa na matoleo ya Kanisa au kutumwa mtandaoni inaleta mabadiliko katika maisha ya imani ya watu binafsi, familia na jumuiya  ya Afrika  amesema  rais wa Tume Ndogo ya Maaskofu wa Marekani.

Kwa sababu ya vipangamizi vilivyowekwa mwaka jana dhidi ya janga la UVIKO-19, na kufungwa kwa makanisa kwa wamini, mnamo 2020 yaanai mwaka jana,  michango wa Mfuko wa Mshikamano kwa ajili ya Kanisa Barani Afrika imepungua sana, katika wakati  ambao  nchi za Kiafrika zilikuwa zikihitaji zaidi. Walakini, Tume Ndogo imeweza kufadhili mipango muhimu. Kwa mfano, nchini Kamerun iliyoharibiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya wanaozungumza Kiingereza na Kifaransa, katekista 65 walipokea kozi za mafunzo ya ushauri wa kisaikolojia na haki za binadamu ambazo ziliwafanya waweze kutoa msaada wa kichungaji kwa maelfu ya watu waliokimbia makazi yao wakikimbia vita.

Nchini Burundi, shukrani kwa fedha zilizopatikana, Baraza la  Maaskofu wa eneo hilo mwapanua programu zake za ulinzi na uhamasishaji dhidi ya unyanyasaji na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto katika majimbo yote. Kwa kuongezea, katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, semina ya kitaifa ya siku nne ya waalimu itatumika kufufua ufundishaji wa dini kwa ajili ya faida ya maelfu ya wanafunzi kitaifa. Nchini Zambia, nchi ambayo, kwa sababu ya idadi ndogo ya makuhani, wakazi wa maeneo ya vijijini zaidi hupitisha miezi bila kupata huduma ya kisakramenti, kwa maana hiyo semina mbili za mafunzo ya kibiblia zilifadhiliwa ili kusaidia viongozi wa eneo kuelewa na kutafsiri  Neno kwa usahihi ya Mungu. Habari zaidi juu ya mfuko wa mshikamano na jinsi ya kuchangia inapatikana kwenye tovuti ya Tume hiyo ndogo ya Baraza la Maaskofu Marekani: www.usccb.org/africa

05 August 2021, 14:09