Maaskofu nchini Australia wanaalika Wakatoliki wote kugundua sakramenti ya Uumbaji, kwa kutambua uwepo wa Mungu ulimwenguni,na kujibu kwa mshangao na shauku waraka wa Laudato Sì Maaskofu nchini Australia wanaalika Wakatoliki wote kugundua sakramenti ya Uumbaji, kwa kutambua uwepo wa Mungu ulimwenguni,na kujibu kwa mshangao na shauku waraka wa Laudato Sì 

Maaskofu wa Australia kwa ajili ya uendelevu na ulinzi wa mazingira

Tunakabiliwa na shida ya ekolojia na Papa Francisko anataka Kanisa lote kwa ngazi ya ulimwenguni lifanye kwa hisia kubwa ya uharaka katika kilio cha dunia na kilio cha maskini.Nchini Australia, watu wenye shauku,taasisi za kidini,shule na mashirika wamekuwa wakifanya kazi juu ya maswala ya ekolojia kwa muda mrefu.Amesisitiza hayo rais wa Tume ya Maaskofu ya Haki za Jamii,Utume na Huduma,Askofu V.Long

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kujitoa kwa kihistoria kwa Kanisa endelevu zaidi na ile iliyotolewa na maaskofu wa Australia ambao wametoa Azimio la pamoja kila mwaka kwa kuongozwa na tema ya haki ya kijamii ambayo mnamo 2021 ina jina “Kilio cha Dunia, kilio cha maskini”. Safari ya miaka saba kuelekea malengo saba yaliyoorodheshwa na Laudato Si ', kwa njia hiyo, ndio ambayo wanachama wa Baraza la Maaskofu wa Australia waliazimia kufanya.

Mgogoro wa kiekolojia ni wa kushughulikiwa haraka

Sababu zinaelezewa mara moja na rais wa Tume ya Maaskofu ya Haki za Jamii, Utume na Huduma, Askofu Vincent Long: “Tunakabiliwa na shida ya ekolojia na Papa Francisko anataka Kanisa lote kwa ngazi ya ulimwenguni lifanye kwa hisia kubwa ya uharaka. Nchini Katika Australia, watu wenye shauku, taasisi za kidini, shule na mashirika wamekuwa wakifanya kazi juu ya maswala ya ekolojia kwa muda mrefu. Ninataka kuwashukuru wote na kuhimiza jamii nzima ya Wakatoliki kuungana nao”.  Mkuu huyo aidha amesema kwamba “watu wa asili na wakazi wa visiwa vya Torres Strait wamekuwa wakitunza mazingira tangu zamani. Wengine wetu tunahitaji kusikiliza, na kujifunza jinsi tunaweza kutembea pamoja kutunza kazi ya Uumbaji, pamoja na wengine ndugu wote”.

Harakati ya Laudato Si: ukweli ulioimarishwa ambao umefanywa upya

Kulingana na yaliyomo katika Azimio hilo, malengo ya Laudato Si 'yatakayofuatwa yanalenga kutekeleza Waraka wa Baba Mtakatifu Francisko wa mwaka 2015, na kuzifanya jaumuiya zote ulimwenguni ziwe endelevu katika roho ya ekolojia fungamani”. Kwa njia hiyo maaskofu wanaalika Wakatoliki wote kugundua sakramenti ya Uumbaji, kwa kutambua uwepo wa Mungu ulimwenguni, na kujibu kwa mshangao na shauku; wanaomba kuwa na uongofu mkubwa uliodhihirishwa katika njia mpya ya maisha, kibinafsi na ya pamoja. Tumeitwa kwa njia mpya ya kufikiria, kuhisi, kuelewa na kuishi”, viongozi hao wanasema katika Azimio hilo. “Matumaini yangu ni kwamba 'Kilio cha Dunia, kilio cha maskini' kitatia moyo mwitikio wa Kikristo zaidi na kwa ufanisi zaidi kwa kilio cha haraka cha Dunia na cha maskini”, alihitimisha Monsignor Long.

Haki, ekolojia, amani

Azimio linashauri familia, shule, parokia, majimbo na mashirika yote kuunaga na maaskofu ili kutia saini ya Jukwaa la Utekelezaji la Laudato Si. Huu ni mpango wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa maendeleo Fungamani ya Binadamu, ambayo itakusanya maoni ya kuchukua hatua kutoka ulimwenguni kote katika kusaidia washiriki katika mchakato wa safari yao ya utunzaji wa mazingira nyumba yetu ya pamoja. Ofisi ya Haki ya Jamii ya Baraza la Maaskofu Australia ilihusika katika kukuza Jukwaa,na katika pendekezo hili, Rais Long pia ametangaza jina jipya la wakala, ambayo ni Ofisi ya 'Haki, Ekolojia na Amani', kwa sababu amesema kuwa“haki ya kijamii, ekolojia na amani" haviwezi kutenganishwa” kamwe ni kama chanda na pete.

06 August 2021, 15:28