2021.08.10 Padre Olivier Maire,Mkuu wa Provinsi wa Wamisionari wa  Monfort Ufaransa ameuwawa tarehe  9 agosti 2021. 2021.08.10 Padre Olivier Maire,Mkuu wa Provinsi wa Wamisionari wa Monfort Ufaransa ameuwawa tarehe 9 agosti 2021. 

Kuhani katoliki ameuawa nchini Ufaransa

Mwathirika ni Padre Olivier Maire mwenye umri wa miaka 60 na Mkuu wa Provinsi ya Shirika la Wamisionari wa Monfort kwenye makao yao ya Mtakatifu Laurent-sur-Sèvre,Vandea.Aliyekiri mauaji hayo ni mtu mwenyewe ambaye alikuwatayari anakabiliwa na kuchoma Kanisa Kuu la Nantes Julai 2020.Habari hizo zimethibitishwa na waziri wa Mambo ya Ndani nchini Ufaransa.Mshikamano kwa upande rais Macron kwa wakatoliki.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican.

Padre Olivier Maire, mwenye umri wa miaka 60 ambaye ameuawa tarehe 9 Agosti 2021 huko Saint-Laurent-sur-Sevre, Vandea nchini Ufaransa. Habari hizo zilithibitishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Oltralpe Darmanin na ambaye mara moja alikwenda eneo la tukio hilo. Muuaji kwa mujibu wa vyombo vya habari Ufaranza, ni raia wa Rwanda na ambaye mwezi Julai mwaka jana alihusika na ku choma Kanisa Kuu la Nantes. Alizaliwa miaka 40 iliyopita Emmanuel Abayisenga na ambaye amejikabidhi kwa vyombo vya usalama. Mtu huyo wa Rwanda akiwa na matatizo ya kiakili alikuwa ameachiwa chini ya Ulinzi wa mahakama akisubiri hukumu mwanzoni mwa Juni na alikuwa amekaribishwa katika Jumuiya ya kitawa ya Padre huyo Maire hadi mchakato huo mwaka 2022. “Ni uchungu na kuchanganyikiwa kuhusiana na kuuawa kwa Padre Olivier aliyekuwa ni Mkuu wa Provinsi wa Shirika la Wamisionari wa Monfort. Tunaungana katika sala na familia yake ya kidini”. Ameelza hayo katika taarifa yake ya kwanza katika mitandao ya kijamii msemaji wa Baraza la la Maaskofu nchini Ufaransa Padre Hugues de Woillemont. “Padre Olivier alikuwa anashughulika mafungo ya kiroho na alikuwa anapenda na kusifiwa sana kwa mahubiri yake”.

Maneno ya Rais Macron na ya serikali

Ukaribu na mshikamano na wakatoliki nchini Ufaransa na Shirika la Monfort umeelezwa na Rais Emmanuel Macron na wa Waziri Mkuu Jean Castex ambao wameonesha uchungu wa kina kwa kile kilichotokea. “Alikuwa na uso mkarimu na upendo wa ndugu”, ameandika rais kwenye twitter akiongeza kuwa “kulinda wale ambao anawaanimi ndiyo ilikuwa kipaumbele”. Kwa kuongeza amesema “ Tunataka uwazi juu ya tendo hili la chuki. Kumdhuru kuhani, mtu wa Kanisa ni kama kuchukia roho ya Ufaransa.” Mchana walifanya mkutano na vyombo vya habari katika mkutano na wajumbe wa Shirika la Monfort na waziri wa Mambo ya ndani. Hata hivyo Waziri huyo wa Mambo ya Ndani Bwana Gérald Darmanin amekataa mzozo wowote na kiongozi wa mlengo wa kulia Bi Marine Le Pen ambaye alidai kwamba mshukiwa wa Rwanda hakufukuzwa baada ya kuchoma Kanisa Kuu la  Nantes. Kwa maana hiyo amesema kwamba “Huu ni wakati wa maombolezo na sio wa  ubishani”, huku  akielezea kuwa mtu huyo hangeweza kufukuzwa kwa sababu alikuwa chini ya udhibiti wa korti akisubiri uamuzi wa haki.

Waathiriwa nchini Ufaransa kati ya makuhani na watawa

Mikasa kadhaa nchini Ufaransa imewaona makasisi na waathiriwa wa kitawa wakiamsha hisia za nguvu kwa watu wa Mungu. Tangu kuuawa kwa Padre Jacques Hamel mnamo tarehe 26 Julai 2016, katika tukio lilitokea wakati wa maadhimisho ya Ekaristi, tangu Mapinduzi ya Ufaransa. Nyuma zaidi lakini tunamkumbuka Padre Jean-Luc Cabes, wa Jimbo la Tarbes na Lourdes, aliyeuawa huko Tarbes usiku wa tarehe 10 na 11  Mei 1991. Jimbo Tulle pia linamkumbuka Padre Louis Jousseaume, kuhani wa parokia ya Égletons, huko Corrèze, ambaye aliuawa nyumbani kwake mnamo tarehe 26 Oktoba 2009. Ilikuwa tarehe 16 Agosti 2005, wakati mahujaji waliokuwa kwenye masifu ya jioni ilitokea mauaji ya mwanzilishi wa Jumuiya ya Taizé, Ndugu Roger Schutz, katika Kanisa la Upatanisho ndani kabisa ya jumuiya ya kiekumene.

10 August 2021, 15:22