Ukame katika maene mengi ya dunia na hasa Afrika ni mkubwa Ukame katika maene mengi ya dunia na hasa Afrika ni mkubwa 

Kenya:Uzinduzi wa mpango wa miaka 5 kwa ajili ya kusaidia maeneo ya ukame

Caritas ya Marsabit imezindua mpango wa miaka 5 unaolenga kupunguza uhaba wa maji lakini pia huduma ya afya kwa watu ambao wanateseka sana na kuongezewa na janga la sasa la Uviko-19.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mpango mkakati wa miaka mitano wa kujibu vya kutosha mahitaji ya kibinadamu ya watu wanaoishi katika maeneo yenye ukame na nusu ukame huko Kenya, umezinduliwa tarehe 30 Julai 2021 na Caritas Jimbo Katoliki la Marsabit.  Kama alivyo thibitisha askofu Peter Kihara wa eneo hilo, kuwa mpango huo unawakilisha fursa ya kuelewa kwamba wote  ni Kanisa linalohama na kwamba wanasonga mbele kwa pamoja na jumuiya na mahitaji yake yaliyopo. Kwa maana hiyo, ombi la askofu Kihara kwa washirika wa ndani na wa kimataifa ni kuunga mkono juhudi za mpango ambao unakusudia kuboresha hali ya maisha ya watu na ambao wanateseka, sio tu kwa ukosefu wa maji, lakini pia kutokana na hukosefu wa upatikanaji wa huduma za afya, ambao ni mkubwa sana hasa kwa kuongezewa kipindi hiki kigumu cha UVIKO-19.

Msaada wa kimataifa

Kwa upande wake, mkurugenzi wa Caritas, Isacko Jirma Molu, amesisitiza kuwa mpango mkakati unakusudia kupunguza mateso ya wanadamu kwa kubadilisha hali ya jumuiya kwa njia endelevu.Hata hvyo amebainisha kuwa haishangazi, kaulimbiu ya mpango huo isemayo “Maendeleo endelevu ya mabadiliko kwa jumuiya za Kata ya Marsabit”. Kwa kuongezea, aliyehakikisha msaada wake katika mpango  huo pia ni  gavana  wa Marsabit, Mohamud Ali, ambaye amebainisha jinsi inavyoshikamana sana na mpango jumuishi wa maendeleo ya eneo hilo na kwa maana hiyo kuiwezesha ili kuanza ushirikiano kama ajenda muhimu katika kufufua maendeleo ya eneo.

Miongoni mwa washirika wanaoshirikiana katika mpango wa miaka mitano ni Caritas ya Kenya, Italia, Ujerumani, Austria, Uhispania na Ulaya, pamoja na Cafod (shirika la misaada la Kanisa Katoliki nchini Uingereza na Wales) na Huduma za Usaidizi Kikatoliki(shirika la misaada ya kimataifa ya kibinadamu ya jumuiya ya Wakatoliki nchini Marekani).

08 August 2021, 14:06