Patriaki wa Kikaldayo nchini Iraq, Kardinali Louis Sako. Patriaki wa Kikaldayo nchini Iraq, Kardinali Louis Sako. 

Kard.Sako:Tunahitaji kufikiria kwa njia mpya ya kusimamia Kanisa

Imehitimishwa Sinodi ya Kanisa mahalia nchini Iraq ambayo imeweza kujadili nafasi ya walei,wanawake na hali halisi ya kisiasa.Patriaki wa Kikaldayo,Kardinali Sako anaunga mkono mawaziri na manaibu wake wakristo kwa ajili ya wema wa Nchi yap.Wameamua kufanya mabaliko ya jina la Upatriaki kwa kuondoa Babilonia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Sinodi ya Kanisa la Kikaldayo nchini Iraq iliyofanyika kuanzia tarehe 9 hadi 14 Agosti kwa kutafakari juu ya ulazima wa kuwa na mabadiliko kwa ujumla na kuhusu hali halisi ya Kanisa wakati huo huo kuangazia juu ya mambo mapya ya kisiasa na kijamii katika nchi. Kulikuwa ni kipindi cha kina kwa maaskofu wote hata wale wa kidiaspora. Walithimini hali halisi ya Iraq kwa karibu sana na kuona mahitaji ya watu na mabadiliko yanayo endelea siku hadi siku nchini humo. Vile vile walisali kwa pamoja, kwa mujibu wa maelezo ya Kardinali Louis Raphael I Sako, Patriaki, wa Kanisa la Kikaldayo. Kwa sababu ya janga la UVIKO-19, ilibidi wasubiri kwa miaka miwili kabla ya kufanya sinodi hiyo. Katika mkutano uliokuwa unatarajiwa kwa hamu sana, wamezungumizia juu ya maana ya kisinodi, juu ya nafasi za wanawake, liturujia na walei kwa ujumla.

Katika kuzungumzia nafasi ya wanawake, Kardinali Sako amesema miaka miwili iliyopita, Kamati ya walei ilikutana kwanza na katika fursa hii, wametuma ripoti yao kuhusu ushiriki wa walei katika maisha ya Kanisa kwa ngazi ya kijamii, kiutamaduni, kiuchumi na kiuchungaji. Na katika muktadha huo, walijadili hata jukumu la mwanamke. Kwa kipinid kirefu amebainisha kwamba, Kanisa lao limekuwa na wanawake ambao wamekuwa wakihudumia katika liturujia, ambao wanafanya kazi kwa ajili ya upendo na ambao wamekuwa wakifundisha katekesi. Kutokana na hili wamejifunza vema yote hayo. Na sasa kila askofu wataweza kuwapelekea baraka wanawake hao ambao wanazo karama za kuhudumia Kanisa kwa dhati.

Kuuhusu suala la kisiasa, Kardinali Sako amesisitiza kwamba walitathimini juu kuwasaidia mawaziri au manaibu wao wakristo kwa ajili ya wema wa taifa lao. Vile vile Kardinali ameeleza uamuzi wa sinodi kubadilisha jina la upatriaki wa Babilonia ya wakaldayo ili kubaki jina moja tu la Upatriaki wa Kikaldayo, kwa sababu amesema, awali ya yote walikuwa na matatizo na jina hilo kwani Babilonia ni jina la kisiasa, kitaifa ambalo halionesha maana Kanisa lao. Makao Makuu ya Kanisa la Kikaldayo au Kanisa ma Mashariki lilikuwa mbali, sasa liko mji wa Baghdad. Kwa maana hiyo walipendelea kuwa na jina la pamoja, kwa Kanisa lao lote ambalo limeenea hata nchini Iraq, Siria, Uturuki, Lebanon na sehemu nyingine za ulimwengu. Jambo jingine ambalo wametafakari ni maana ya kisinodi.

Kardinali Sako aidha amefafanua kwamba Kisinodi ni asili ya Kanisa. Hiyo ni kwa sababu kila kitu kinafanyika kwa pamoja: mmoja hawezi kutawala Kanisa bali ni katika kufanya kazi kwa pamoja kwa ushirikiano kama walivyofanya mitume. Kardinali amsisitiza kwamba kama wao Kanisa la mashariki, wana uzoefu wa muda mrefu wa kisinodi na htya kwa Kanisa la Magharibi ambalo linaweza kuiga mfano wa uwezo wao huo. Kwa mfano tangu zamani wao walikuwa na Sinodi ya kudumu na ya kawaida. Kwa njia hiyo “Kanisa la kilatino linaweza kuchukua hatua hii kama kianzio cha kutoa mamlaka zaidi kwa maaskofu au mabaraza ya maaskofu kwa sababu kila nchi ni tofauti na nyingine. Tunahitaji kufikiria kwa njia mpya ya kusimamia Kanisa katika ngazi zote”, amehimimisha kufafanua Patriaki wa Kikaldayo, Kardinali Sako.

18 August 2021, 14:18