Kituo cha  AOSIS huko  Douala, Camerun Kituo cha AOSIS huko Douala, Camerun 

Cameroon:Mkurugenzi wa Utume wa Kanisa Uingereza:Kanisa liko karibu na watu

Mkurugenzi wa Utume wa Kimisionari Uingereza amesema Kanisa liko karibu na watu wa Kameruni ambao wako katikati ya mgogoro wa wao kwa wao kati ya wanaozungumza kiingereza na kifaransa ambapo sasa imefikia miaka mitano.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Kukaa karibu na watu kama nguvu ya amani na mapatano katikati ya moto unaokutana kati ya sehemu mbili za migogoro, ndiyo nafasi kuu ya Kanisa ambalo linaendelea kujikita nalo nchini Kameruni, ambapo mara nyingi kumekuwa ni malumbambo kati ya wapigania uhuru na umoja ambapo mizozo, vurugu, umaskini na hofu zinaendelea kuenea. Mzozo uliosahaulika una mizizi yake katika enzi ya ukoloni, wakati eneo la Kamerun, zamani lilikuwa tayari ni koloni la Ujerumani, ambalo liligawanywa kati ya Uingereza na Ufaransa na baadaye kuungana tena katika shirikisho moja baada ya uhuru. Aliyeeleza hayo katika mahojiano yaliyopo kwenye tovuti ya Baraza la Maaskofu wa Uingereza na Walles(Cbcew) ni Padre Anthony Chantry, Mkurugenzi wa Missio-Uk, ambalo ni shirika la kimisionari la Kanisa la Uingereza na Walles.  Ni miaka 5 sasa ya mizozo kati ya serikali ya Kati na vikundi vya kujitenga ambao katika maeneo ya Mashariki ya Nchi wanaomba kuunda serikali yao wenyewe. Migogoro hadi sasa imesababaisha vifo vya watu elfu tatu na kulazimisha kukimbia kwa watu karibu nusu milioni na kupunguza eneo lenye utajiri wa rasilimali hadi kikomo, na watu milioni tatu wako katika dharura zaidi ya kibinadamu.

Katika muktadha huu wa kushangaza ameelezea Padre Chantry, ambaye ametembelea nchi hiyo ya Afrika mara kadhaa na anajua hali ya eneo hilo vizuri, kwamba Kanisa halitazami upande mmoja kwa sababu, liko upande wa watu ambao mara nyingi hujikuta katikati ya mateso haya. Lakini kuwa katikati, na kutokuwa na upande wowote amesisitiza kuhani huyo ndiyo msimamo hasa inapotakiwa kudumishwa ili kuhamasisha amani na upatanisho, hata kama hii haieleweki kila wakati na wahusika wawili. Serikali, kwa upande mwingine na watengano wa Kiingereza Amba, kwa upande mwingine, mara nyingi huishutumu kwa kuzunguka kwa upande mmoja au upande mwingine.

Ujumbe wake kwa watu ni kwamba njia ambayo mgogoro huo unashughulikiwa -pande zote mbili itasababisha vurugu zaidi, vifo na mateso. Hii ndiyo sababu, kulingana na mkurugenzi wa Missio, kwamba Kanisa kutokuwa upande wowote katika mzozo huo ndio nafasi pekee inayowezekana ya kuiunganisha nchi, hata kama anakubali kuwa hii inajumuisha hatari na sio bila gharama kwa maisha ya wanadamu Yeye anasema kuwa “Kanisa ni taasisi pekee ambayo watu wanaamini. Imekuwa ikihubiri ujumbe wa amani kwamba hakuna vurugu bali amani na haki na watu wanaamini kile ambacho Kanisa linasema. Hawaamini serikali na labda, hawaamini hata kuamini viongozi wao wengi, lakini wanalisikiliza Kanisa. Kwa njia hiyo utume wa Cameroon ni kuhamasisha watu kutafuta njia za amani za upatanisho, wasitumie vurugu chini ya hali yoyote na wapatanishe kutolewa kwa watu waliotekwa nyara wakati wa vita.

Maaskofu wa Kameruni wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii mbele suala hili amesema Padre Chantry na kwamba wanaelezea sauti ya watu ili kupunguza vurugu, ikipelekea ukiukaji mwingi wa haki za binadamu ambao unafanywa nchini Kamerun na pande zote mbili. Hii ndiyo sababu Padre huyo amesisitiza katika mahojiano kwamba Kanisa nchini Kamerun linahitaji msaada kama ule wa Uingereza. Ni msaada, kwanza kabisa, kwa njia ya sala, lakini pia kuvuta hisia za viongozi wa kisiasa wa Uingereza kuhusu janga hili ambalo linaendelea nchi hiyo barani Afrika. Kuhani pia ameomba mchango wa kifedha kwa waamini kupitia mashirika kama vile Missio ambayo inasaidia Makanisa katika nchi za kimisionari.

Ziara ya Kardinali Parolin Katibu wa Vatican nchini Kameruni mwezi Februari iliyopita
Ziara ya Kardinali Parolin Katibu wa Vatican nchini Kameruni mwezi Februari iliyopita

Ikumbukwe kwamba nchini Cameroon kuna mikoa 8 inayozungumza Kifaransa na 2 zinazozungumza Kiingereza, ziko Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi. Mapigano hayo yalianza mnamo 2016 wakati serikali iliamua kupeleka wafanyakazi wa utawala, walimu na majaji kutoka maeneo yanayozungumza Kifaransa kwenda maeneo hayo mawili yanayozungumza Kiingereza. Maandamano kadhaa yalitokea ambayo yaliandaliwa na kikundi cha wanaozungumza Kiingereza cha Cameroon, kupinga hatua kama hizo zinazodhaniwa kuwa za kibaguzi na za kutengwa. Uingiliaji mkali wa vikosi vya jeshi juu ya umati ulizidisha mvutano, ukongezea kiwango cha mizozo halisi na kupelekea mnamo 2017 kuunda  kwa vikundi vya msituni vya wanaozungumza Kiingereza ambavyo vilidai kujitenga kwa mikoa yao, kujitangazia uhuru wa serikali ya Ambazonia. Kwa miaka iliyopita, Baraza la Maaskofu wa Cameroon (Cec) limezindua miito kadhaa za maridhiano na amani. Miito pia imesisitizwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican ambaye alitembelea nchi hiyo tangu Januari 28 hadi Februari 3 mwaka huu, akielezea ukaribu wa Baba Mtakatifu Francisko kwa watu wa eneo hilo na, kwa jumla, kwa bara zima la Afrika. Kardinali Parolin alisema kuwa nuuiwa na nchi hiyo mpendwa na ya ajabu kuelekea kwa Mungu.

06 August 2021, 15:04