Rais  Alassane Ouattara na mtangulizi wake Laurent Gbagbo tarehe 27 Julai wakati wa mkutano wao Ikulu huko Abidjan. Rais Alassane Ouattara na mtangulizi wake Laurent Gbagbo tarehe 27 Julai wakati wa mkutano wao Ikulu huko Abidjan. 

Ivory Cost,Askofu Bessi:Mkutano wa Ouattara-Gbabgo ni hatua muhimu ya amani

Askofu Mkuu Ignace Bessi Dogbo,wa Jimbo Kuu Korhogo na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Ivory Coast(Cecci) wakati akiwasalimia viongozi katika mkutano wa hivi karibuni wa amani kati ya Rais Alassane Ouattara na mtangulizi wake Laurent Gbagbo ameelezea matashi mema ambayo ni hatua muhimu ya magezi na ishara hizo ziendelea ili kufikia kilele cha amani kwa kila mtu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Tukio ambalo lilisubiriwa kwa muda mrefu na watu wa Ivory Coast, ambalo linatoa fursa moja ya kutazamia amani na mapatano kwa ajili ya nchi hiyo ndiyo matashi mema yaliyoelezwa Askofu Mkuu Ignace Bessi Dogbo, wa Jimbo Kuu Korhogo na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Ivory Coast (Cecci) wakati akiwasalimia hivyo viongozi katika mkutano wa hivi karibuni wa amani kati ya Rais Alassane Ouattara na mtangulizi wake Laurent Gbagbo. Wapinzani hao wawili wa zamani walikutana mnamo tarehe 27 Julai 2021 katika ikulu ya rais, zaidi ya mwezi mmoja baada ya Gbagbo kurudi nchini kwake, baada ya uthibitisho wa kuachiliwa huru kwa Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa (ICC) kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Kiongozi huyo wa zamani wa nchi wa Ivory Coast, aliyekuwa madarakani tangu 2000 hadi 2010, alikamatwa mnamo Aprili 2011 na kupelekwa mahakama ya Aia baada ya vurugu zilizosababishwa na kukataa kwake kumtambua Ouattara kama mshindi wa uchaguzi wa 2010 ambapo watu kama elfu tatu walikufa. Gbagbo baadaye aliachiliwa huru kwa mara ya kwanza mnamo 2019 na mwanzoni mwa mwaka huu hukumu hiyo ilithibitishwa na majaji wa rufaa, ikitengeneza njia ya kurudi tarehe 17 Juni.

Mnamo Julai 10 alikutana na rais mwingine wa zamani na mpinzani wa zamani, Henri Konan Bédié, ambaye alielezea nia yake ya kuzindua mpango wa upatanisho na kusisitiza udharura wa kufanya kazi ya kurudisha amani ya kudumu nchini Ivory Coast. Nia hii ilithibitishwa mwishoni mwa mazungumzo na Ouattara ambayo yalifanyika katika hali ya utulivu na maridhiano. Katika mahijiano yaliyochapishwa tarehe 3 Agosti, katika ukarasa wa Facebook wa Baraza la maaskofu wa Ivory Coast, Askofu Mkuu alielezea tukio hilo kama hatua muhimu na ishara muhimu ya kusonga mbele katika mchakato wa upatanisho. Akiendelea alisema kuwa kuna wakati wa kufanya vita na wakati wa kufanya amani [...] na wakati watu wana nguvu na kutafuta masilahi ya watu wao, ni wakati unaoitwa Kairos na kama Kanisa hawawezi kuacha kutofurahia juu ya jambo hili.

Rais wa Baraza la Maaskofu wa Ivory Coast kwa maana hiyo ameelezea matashi mema ambayo ni kwamba hatua ya mageuzi isibadilike kuwa wigo. Badala yake: “Ishara hizi lazima ziongezeke na lazima kila wakati tupande yaliyo ya juu ili kufikia kilele ambapo kuna amani kwa kila mtu” amesisitiza huku akiwataka rais Ouattara na mtangulizi wake Gbabgo wasiruhusu wale wasiotaka upatanisho, wale ambao wanatupa mafuta kwenye moto. Kwa kuhitimisha ametoa mwaliko wa kufanya mchakato wa upatanisho  ambao ni umuhimu kwa wote ili waweze kusonga mbele kwa haraka zaidi, kwa uwazi, kwa ukweli na  katika kutafuta faida ya wote. Maslahi binafsi hayatapelekea kamwe amani”.  Kurudi kwa Gbagbo nchini Ivory Coast baada ya miaka kumi ya uhamishoni kulilakiwa na shauku na wafuasi wa chama chake Front Populaire Ivoirien, (FPI) chama kilichoanzishwa na Rais wa zamani. Hata hivyo wakati wa kurudi kwa Gbagbo Kardinali Jean Pierre Kutwa, Askofu Mkuu wa Abidjan alimzawadia Rozari akimshauri kuchangia mchakato wa upatanisho ambao umeanza sasa.

05 August 2021, 14:29