Wahamiaji:Utazamaji wa mbali wa Boti katika bahari ambayo watu hawana makoti ya kuokoa maisha. Wahamiaji:Utazamaji wa mbali wa Boti katika bahari ambayo watu hawana makoti ya kuokoa maisha.  

Italia:Wito wa Askofu Lorefice ili kuokoa wahamiaji baharini!

Zaidi ya maisha ya watu 400 walioko kwenye moyo wa bahari ya Mediterranea wanasubiri maamuzi yetu wanasubiri ili kuokolewa.Ni wito wa Askofu Mkuu wa Palermo kisiwani Sicilia waondolewe wahamiaji ambao wako hatarini katika sehemu ya SAR,eneo la Malta.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican.

Kwa mara nyingine tena bado tuna wakati. Mamlaka ya Italia, mamlaka ya Malta, na mamlaka ya Ulaya bado iko katika wakati. Ubinadamu wetu bado una wakati. Jukumu letu kama Wakristo bado lina wakati. Zaidi ya maisha ya watu 400 yamo katikati mwa bahari ya Mediterania wanasubiri uamuzi wetu, wanasubiri kuokolewa. Hili ndilo  lililowasilishwa kwa taasisi husika na Askofu Mkuu wa Palermo, Italia Askofu Mkuu Corrado Lorefice, akiingilia kati mara moja katika kuomba uokoaji wa boti tano, na wahamiaji zaidi ya 450 waliomo ndani mwake, ambao wako  hatari ya kuvunjika kwa meli hizo katika eneo la SAR (Utafutaji na Uokoaji) la Malta, kama walivyo angazia mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayofanya kazikatika bahari ya  Mediterania bila kupokea majibu yoyote.

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Lorefice amesema “Ni mara ngapi katika miaka ya hivi karibuni tumeshiriki mshtuko wa ukosefu wa nguvu, kutokana na kufadhaika kwa kutokujali mbele ya hali mbaya ya mamia, sasa maelfu ya kaka na dada ambao wamepoteza maisha yao wakati wakijaribu kutafuta na hakuna kitu zaidi ya utu wao, haki yao ya kuishi! Kwa maana hiyo, mwaliko wa Askofu Mkuu wa Palermo  ni kwa wale wote ambao wana uwezo wa kufanya uamuzi juu ya hatima ya watu hawa 400 ili wafanye hivyo mara moja na wasilazimishe Ulaya kuwaomboleza katika masaa machache kama waathiriwa wa unyama huu.

“Kutoamua katika mwelekeo huu inamaanisha kukubali kutokusaidia ni katika sehemu zote za mkakati ambao Serikali zetu zinachukua kusimamia suala la uhamiaji, likiendelea kufanya mauaji ya mauaji ya kimbari ambayo walio wengi wanaendelea kukataa kuhudhuria, wakigeuza shingo zao upande mwingine” amesema Askofu Mkuu Lorefice”. Kama wanadamu hata kabla ya kuwa Wakristo, Askofu Mkuu wa Palermo amesema hatuwezi kushiriki kukaa kimya mbele ya uendelezaji wa uovu huu, hatuwezi lakini lazima kuendelea kukumbuka uharaka wa kuchukua hatua dhidi ya kila kitu kinachotokea karibu na katika moyo wa Mediterranean, kwa jina la haki za binadamu za kimataifa, Katiba ya Italia na Injili.

05 August 2021, 14:56