Picha ya maono huko katika  madhabahu ya Mama Maria Knock Ireland. Picha ya maono huko katika madhabahu ya Mama Maria Knock Ireland. 

Ireland:Maria atukumbushaa kuwa Mungu yu karibu hata kipindi kigumu

Askofu Mkuu Neary amesema Mama Maria anatukumbusha kuwa Mungu daima yuko karibu hata katika nyakati ngumu.Amesama hayo wakati wa kuadhimisha misa ya kumbukizi la tokeo la Bikira Maria wa Knock katika Kijiji cha County Mayo nchini Ireland mnamo 21 Agosti 1879.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika nyakati ngumu zenye uchungu na mahangaiko kama zile walizoishi watu wa Ireland wakati wa balaa la Karne ya XIX au kama ile ya sasa ya janga la UVIKO 19, Mama Maria anatukumbusha kuwa moyo wa Mungu daima huko karibu na wale ambao ulimwengu unaweza kuwaacha, wale ambao hawana nguvu tena, maskini na walioacha peke yao. Amesema hayo kwa ufupi Askofu Mkuu Michael Neary, wa Tuam wakati wa Misa ya kiutamaduni iliyoadhimishwa tarehe 21 Agosti 2021 katika kumbukizi la tokeo la Mama Maria katika Madhabahu ya kimataifa ya Knock, nchini Ireland. Katika jamii inayofanya kujitawala na uhuru wa mtu binafsi wa kujivunia, amesema Askofu Mkuu katika mahubiri yake, kuwa mtu huyo anaweza kuhisi kuteleza katika bahari ya maisha, anahisi hisia za kukosa nguvu mbele ya peo za kiuchumi na kisiasa ambazo yeye kwake  udhibiti mdogo sanana, na hali hii inaweza kuondoa matumaini kutoka katika moyo wa mwanadamu. Lakini kwa “tazama mimi hapa ya Mama Maria wakati wa kupashwa habari, yeye kinyume chake anatuweka mbele ya mtazamo mpana ambao ni utajiri, ukina na jumuishi  zaidi  kuliko ule unaopendekezwa na utamaduni wa kisasa, kwa sababu ni kulingana na imani yake wanyenyekevu kwa Mungu, ambayo inahitajika sana leo”, amesisitiza Askofu Mkuu Neary,

Askofu mkuu wa Tuam aidha ameongeza kusema kuwa “Katika nyakati hizi ngumu zilizowekwa alama na UVIKO-19, imani yetu inaeleweka kuwa imetetemeka. Tumepoteza wapendwa wetu, labda hata kazi zetu, tumeona kaka na dada wamefadhaika na wapweke, lakini wakati tunajaribiwa kufunga milango au tunaona kuwa imefungwa kwetu, tunahitaji Maria kufungua milango hii na utuongoze katika ulimwengu mkubwa, mpana, na wenye furaha zaidi. Ushujaa usioweza kushindwa, tumaini lenye uhai, imani thabiti, furaha ya kupendeza, utamu na nguvu wa kufundisha mambo muhimu sana leo, hii hasa wakati ambapo sifa hizi ni muhimu sana,  zinahutajika katika utamaduni wa kisasa”. Jambo la kukusha ni kwamba Madhabahu ya Knock yako katika kijiji kimoja cha County Mayo, magharibi mwa Ireland, ambapo jioni ya tarehe 21 Agost, 1879, Bikira Maria Mtakatifu, Mtakatifu Joseph na Mtakatifu Yohane walionekana kwa watu 15 pamoja na madhabahu na Msalaba na Mwanakondoo, picha ya utamaduni ya  Yesu, na malaika wakiwa katika kuabudu. Tangu wakati huo eneo hilo limekuwa mahali pa hija za wakristo wa ndani na nje kwa Bikira Maria huko Ireland,

Hija umuhimu ni ambyao imedhihirishwa na ziara za mpapa kwa mfano ambayo Mtakatifu Yohane Paulo II alifanya mnamo 1979, kwenye karne moja ya maajabu, lakini pia na ziara za baadaye za Mtakatifu Teresa wa Calcutta, mnamo 1993 na ya hia karibuni ya Papa Francisko, mnamo 2018, wakati wa safari yake ya kitume kwa ajili ya Mkutano wa Ulimwenguni wa Familia huko Dublin. Ibada ya Mama yetu wa Knock iliidhinishwa mnamo 1936 baada ya kutambuliwa kwa ukweli wa maono na tume maalum ya Kanisa. Ikumbukwe pia kwamba mnamo Machi 19 ya mwaka huu, katika Sikukuu ya Mtakatifu Joseph, Baba Mtakatifu Francisko ameipa sifa ya madhabahu ya Knock kuwa ya kimataifa ya Maria na Ekaristi. Miujiza na uponyaji ambao ulianza katika siku zilizofuata na maajabu yameandikwa katika patakatifu hapo. Mnamo mwaka wa 2019 Kanisa la Ireland lilitambua kama miujiza uponyaji usioeleweka kisayansi wa mwanamke aliyekuwa ugonjwa wa kupooza kabisa, ambaye baada ya kubarikiwa na monstrance wakati wa baraka za wagonjwa, alianza tena kutembea na akaponywa.

24 August 2021, 16:02