Papa Francisko akiwa na mkutano na Patriaki wai Babilonia ya wakaldayo (Iraq),Patriaki wa  Antiokia ya Wamaroniti (Libanon),Patriaki wa Kilikia ya Waarmenia (Lebanon),Patriaki wa Antiokia dei Kisiria,Patriaki wa Antiokia ya Wagiriki-Wamelkiti. Papa Francisko akiwa na mkutano na Patriaki wai Babilonia ya wakaldayo (Iraq),Patriaki wa Antiokia ya Wamaroniti (Libanon),Patriaki wa Kilikia ya Waarmenia (Lebanon),Patriaki wa Antiokia dei Kisiria,Patriaki wa Antiokia ya Wagiriki-Wamelkiti. 

Iraq:Askofu mpya Mwandamizi wa Upatriaki wa Alquoch ya Wakaldayo

Mhemishwa Thabet Habib Yousif Al Mekko,ambaye hadi sasa alikuwa msimamizi wa Protokali za Jimbo Kuu la Mosul mahali ambapo alikuwa amepewa idhini na Baba Mtakatifu.amechaguliwa na Sinodi ya Maaskofu wa Kanisa la Kipatriaki la Babilonia ya Wakaldayo kuwa Askofu Mwandamizi wa Upatriaki wa Alquoch nchini Iraq.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Sinodi ya Maaskofu wa Kanisa la Kipatriaki wa Babilonia ya Wakaldayo wamemchagua Askofu Mwandamizi wa Upatriaki wa Alquoch (Iraq), Mhemishwa Thabet Habib Yousif Al Mekko, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa msimamizi wa Protokali za Jimbo Kuu la  Mosul,mahali ambapo alikuwa amepewa idhini na Baba Mtakatifu

Muheshimiwa sana Thabet Habib Yousif Al Mekko alizaliwa tarehe 14 Februari 1976 huko Karemlesh (Iraq). Alihitimu katika Sayansi ya Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Mosul na kisha akaanza mchakato njia ya useminari jijini Roma, na kijipatia shahada katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urubaniana na shahada katika masomo ya Mababa wa Kanisa katika Taasisi ya Augustinianum Roma. Kwa kurudi nchini Iraq, alipewa daraja la upadre  mnamo tarehe 25 Julai 2008 huko Karamlesh.

Alijishughulisha na huduma ya kichungaji huko Karemlesh hadi uvamizi wa Uwanda wa Ninawi mnamo 2008 na baadaye akawasindikiza waamni wake kumbilia huErbil.  Baada ya kurudi tena huko Karemlesh alikuwa Paroko akifuatilia kwa karibu mipango ya ukarabati na kuendelea na shughuli za ufundishaji wa somo la Mababa wa Kanisa na Taalimungu katika Chuo cha Babel. Hadi sasa alikuwa ni msimamizi wa Protokali za Jimbo kuu la Mosul ya Waladayo nchini Iraq.

14 August 2021, 15:52