KILA MTU ANATAFUTA NAMNA YA KUWEZA KUISHI NA KULALA BAADA YA TETEMEKO HUKO HAITI KILA MTU ANATAFUTA NAMNA YA KUWEZA KUISHI NA KULALA BAADA YA TETEMEKO HUKO HAITI 

Haiti:Wito wa mshikamano kutoka Baraza la makanisa(Coe)

Hali halisi mbaya inayosubiriwa tena katika kisiwa cha Caribbien kwa dhoruba ya kitropiki ambayo inaweza kusababisha ugumu wa wakoaji huko Kusini mwa kisiwa hicho mahali ambapo wanaendelea kuchimba vifusi kuona kama wanaweza kuoka watu kufuatia na tetemeko la ardhi Agosti 14.Baraza la Makanisa(Coe linatoa mshikamano wao na waathiriwa wakati.Caritas internationalis imezindua mfuko.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika barua iliyoandikwa kwa wahaiti, Baraza la Kiekumene la Makinisa ulimwenguni, linaelezea salamu za rambi rambi kwa wathriwa wa tetemeko la tarehe 14 Agosti 2021 ambalo limesababisha vifo zaidi 1400 vingi na zaidi ya majeruhi 6000 na wengina kupotea. Mtetemeko wa ardhi wenye nguvu wa 7.2 Richter ambao uliikumba Nchi za Carribien zaidi umerekodi majerui wengi kwa sababu ya uharibifu wa nyumba, barabara na miundombinu mingi ya serikali kwa mijibu wa taarifa za serikali.  Baraza la Makanisa linawakilishie maombi yao kwa wale wote ambao wamepoteza wapendwa wao, kwa ajili ya watu wengine na Makanisa ambayo mara moja wameanza mchakato wa kusaidia. Caritas internationalis imezindua mchakato wa ukusanyaji wa fedha kwa ajili ya mfuko wa  kusaidia.

kijana aliyeumia kutokana na matokeo ya tetemeko anasaidiwa na ndugu
kijana aliyeumia kutokana na matokeo ya tetemeko anasaidiwa na ndugu

Unaweza kutoa chochote kupitia: www.caritas.org/donate-now/haiti-earthquake-2021/

Hata hivyo  Jumapili 15 Agosti 2021, Papa Francisko mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana alisema: “Katika masaa machache yaliyopita, tetemeko kubwa la ardhi limetokea huko Haiti na kusababisha vifo vingi, majeruhi na uharibifu mkubwa wa mali. Ninaonesha ukaribu wangu na wale watu wapendwa waliokumbwa sana na tetemeko la ardhi. Ninapoinua maombi yangu kwa waathiriwa kwa Bwana, ninawasilisha neno langu la kutia moyo kwa walionusurika, nikitumaini kuwa mwitikio wa ushiriki wa msaada kutoka kwa jumuiya ya  kimataifa. Na mshikamano kutoka kwa wote ili upunguze matokeo ya janga hilo". Baadaye Papa ameongeza kuwaomba waamini wasali wote kwa Mama wa Yesu sala ya salamu Maria...

Papa Francisko Jumapili 15 Agosti aliwaombea waathirika wa Haiti
Papa Francisko Jumapili 15 Agosti aliwaombea waathirika wa Haiti

Haiti, pamoja na mambo mengine, iko katika koni ya dhoruba ya kitropiki iitwayo ‘Grace’  kama walivyo bainisha wataalam na kwamba upepo mkali na mvua zinahofiwa ambazo zinaweza kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi. Tayari imeharibiwa na mtetemeko wa ardhi mnamo Januari 2010, na vile vile na mizozo ya kiuchumi na kisiasa iliyofuata, watu wa Haiti wanakabiliwa tena na maumivu na wasiwasi,  wakati wanapaswa kuhamasisha na njia ndogo ili kusaidia waathiriwa wa janga jipya, ameandika naibu katibu mkuu wa Baraza la Makanisa (Coe), Mchungaji Odair Pedroso Mateus. Na ikiwa hasira inakua kati ya wale ambao wanahisi kutishiwa na vurugu za asili na kutelekezwa na serikali, “sauti ya Makanisa, ambayo waamini kama manabii wa kibiblia wameomba kwa wenye nguvu kwa ajili ya walio hatarini zaidi. Na kwamba sasa ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kuonesha mshikamano wa Coe na hatimaye wanatoa wito kwa Makanisa ambayo ni sehemu yake kutoa msaada wao kwa watu wa Haiti.

Watu wa Haiti wakiwa wanatafuta maji
Watu wa Haiti wakiwa wanatafuta maji
17 August 2021, 14:57