Hali mbaya iliyosababishwa na Tetemeko la ardhi nchini Haiti ni ngumu Hali mbaya iliyosababishwa na Tetemeko la ardhi nchini Haiti ni ngumu 

Haiti:Idadi ya vifo inazidi kuongezeka na Cei imetoa msaada!

Takwimu zimefika kutoka kikosi cha Ulinzi wa Kiraia wa eneo la Haiti limethibitisha kuwa watu 2,189 wamekufa,12,000 wamejeruhiwa na 332 hawapatikani.Lakini baada ya tetemeko la ardhi, nchi inapaswa kushughulikia hali mbaya tabiachi ambayo inapunguza kasi juhudi za misaada.UNICEF inaripoti watu wasiopungua 600,000 wako katika hali ya uhitaji wa haraka,Baraza la Maaskofu Italia watenga euro milioni moja.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kadri masaa yanavyopita, ndivyo idadi ya waliokufa kutokana na tetemeko la ardhi lililoharibu Haiti mnamo 15 Agosti inazidi kuwa ya kushangaza. Takwimu za hivi karibuni, zilizotolewa na Wakala wa Ulinzi wa Kiraia nchini, zinaripoti idadi ya vifo hadi zaidi ya 2,000 na waliojeruhiwa hadi 12,000. Shughuli za uokoaji, kwa siku nzima ya tarehe 18 Agosti, zilikuwa ngumu kutokana na kusafiri kwa dhoruba ya kitropiki Grace lakini, licha ya ugumu ambapo wanakujitolea na polisi wamefanya kazi na kuwaoka watu kumi na sita waliopatikana wakiwa hai chini ya kifusi cha jengo la zamani la Umoja wa Mataifa  UN katika kijiji cha Brefet.

Msaada unaendelea kutolewa kwa majeruhi huko Haiti
Msaada unaendelea kutolewa kwa majeruhi huko Haiti

Na wakati Caritas Intarnationalis  inaendelea kuhamaisha msaada kutokana na ukosefu wa maji na chakula, Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI) wameamua kutenga euro milioni moja kwa ajili ya msaada, kufadhiliwa kupitia 8X1000, na wametangaza kuwa Jumapili ijayo tarehe 22 Agosti itakuwa siku ya maombi katika parokia zote za Italia kwa ajili ya kuliombea taifa hili la Haiti.

Watoto wengi hawana mahali pa kulala
Watoto wengi hawana mahali pa kulala

Ni wakati mgumu, wa majaribu, ambayo lazima  kuyainisha kwa imani kuu, amesema hayo Askofu  Pierre André Dumas, wa Anse-à-Veau-Miragoâne, moja ya majimbo ya Haiti yaliyoathirika zaidi. Pia ni wakati pia ambao lazima waingilie kati  kuwa karibu na kusikiliza mahitaji ya watu. Eneo lote la jimbo la Anse-à-Veau-Miragoâne lilibomolewa kabisa; nyumba saba kati ya kumi ziliharibiwa na tetemeko lenye nguvu ya Kipimo cha Ritcher 7.2. Na bado hawawezi kuwasiliana na watu wanaoishi milimani na katika maeneo yaliyotengwa. Watu sasa wanahitaji kila kitu, hata maji. Kwa hili wanaomba msaada kutoka nchi nyingine.

Msaada unaendelea kupelekwa kwa manusura
Msaada unaendelea kupelekwa kwa manusura

Askofu Dumas anasema kwamba makuhani wa jimbo lake pamoja na watawa na wamisionari, wanafanya kila wawezalo kuwasaidia manusura: Usindikizaji  wa makuhani wake na watawa wapo kila wakati. Wakati wa mshikamano ndiyo huuna wanasali pia kwa pamoja.Kwa kuongezea, mahitaji machache  msingi ambayo Kanisa lao slililopokea yalishirikiwa mara moja .Hali ya miundo ya jimbo pia ni ya kushangaza: nyumba nyingi za kikuhani na parokia zimefutwa kabisa. Walfanya ukaguzi na waligundia  kuwa zaidi ya nusu ya makanisa hayapo tena. Lakini, licha ya kila kitu, makuhani wapo: wanawasindikiza waamini na kujaribu kukidhi mahitaji yao. Kwa maana hiyo yeye pia ni miongoni mwa watu kuonesha kuwa Mungu hajawaacha watu wake, amesisitiza.

19 August 2021, 14:40