Bado kuna haja ya kubadili maisha ya watu wa Burundi Bado kuna haja ya kubadili maisha ya watu wa Burundi 

Burundi:Rais Ndayishimiye ameomba maaskofu kushirikiana kwa maendeleo ya nchi

Hivi karibuni,maaskofu katoliki nchini Burundi wamekutana na Rais Ndayishimiwe.Katika maongezi yao,wamegusia serikali,maridhiano na maendelo ya kijamii na kiuchumi.Kiongozi wa nchi hiyo anapongeza mchango wa Baraza la Maaskofu hasa katika uwanja wa Elimu,upatanisho na maendeleo ya jumuiya nzima kwa ujumla.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Serikali nzuri, maridhiano na maendeleo ya kijamii na kiuchumi ndiyo mada zilizo kabiliwa katika juma lililopita na maaskofu wa Burundi wakati wa kukutana na Kiongozi mkuu wa Nchi hiyo, Bwana Evariste Ndayishimiye. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maaskofu kama ilivyoripotiwa na Afrique sur 7, Rais amekubali kuwatia moyo watu ili waanzishe mipango ambayo inaweza kuwapa maisha ya kushirikiana katika kuzalisha na amebainisha kuwa kati ya watu kumeongezeka ile imani kwa watawala wao, licha ya kesi nyingine za manyanyaso ya madaraka kutoka kwa baadhi za tawala za mikoa na wilaya

Mbele wasi wasi ulioelezwa na Maaskofu Katoliki nchini Burundi kuhusiana na hali halisi ya kijamii katika Nchi hiyo, Rais Ndayishimiye, ambaye pia ameeleza ushirikiano kati ya Kanisa Katoliki na Taasisi za serikali, huku akipongeza mchango mkubwa wa Baraza la Maaskofu katika uwanja wa Elimu, upatanisho na maendeleo ya jumuiya kwa ujumla ameonesha utashi wa serikali wa kuendeleza msimamo kijamii na kulinda haki kijamii na za kisheria.

Kwa upande wake kiongozi wa Nchi ya Burundi, ameelezea jinsi gani Kanisa katoliki lina nafasi muhimu katika maendeleo ya Nchi. Na mwisho maaskofu na rais wamekubali  na kuelezea furaha yao ya kurudi kwa wingi wakimbizi na wametoa wito wao kwa wale wote ambao wanataka kurudi ili kujiandikisha katika vituo vilivyopewa jukumu hilo kurahisha kurudi kwao.

18 August 2021, 14:05