Kanisa nchini Brazil liko linaadhimisha mwezi 8 wote wa Kuombea Miito kwa kuongozwa na kauli mbiu:Kwa kuongozwa na kaulimbiu “Kristo anatuokoa na kututuma”: anayesikiliza Neno langu ana uzima wa milele Yh 5,24, Kanisa nchini Brazil liko linaadhimisha mwezi 8 wote wa Kuombea Miito kwa kuongozwa na kauli mbiu:Kwa kuongozwa na kaulimbiu “Kristo anatuokoa na kututuma”: anayesikiliza Neno langu ana uzima wa milele Yh 5,24,  

Brazil:Mwezi wa kuombea miito,'Kristo anatuokoa na kututuma'

Kristo anatuokoa na kukutuma na anayesikiliza Neno langu anao uzima wa milele kutoka Injili ya Yohane 5,24,ndiyo kauli mbiu inayoongoza mwaka huu kwa Mwezi 8 wa kuombea Miito nchini Brazil ulioanzishwa na Baraza la Maaskofu nchini humo mnamo 1981.

Kwa kuongozwa na kaulimbiu “Kristo anatuokoa na kututuma”: anayesikiliza Neno langu ana uzima wa milele kutoka Injili ya Yohane 5,24, Kanisa nchini Brazil liko linaadhimisha kwa mwezi huu wote wa  Kuombea Miito, ambapo Kanisa lote limejikita katika sala, tafakari na matendo yanayohusu miito mbali mbali. Kwa kila wiki ya siku 28, kwa dhati kutakuwa na sekta maalum kama ifuatavyo: ya kikuhani na huduma za waliowekwa wakfu; sekta ya familia; ya maisa ya kitawa na miito ya walei wakristo. Katika fursa hii, umeandaliwa mwongozi uliopewa jina “saa ya miito” ambao unaunganisha mihimili mbali mbali, miongoni mwao kuna Tume ya Baraza la Maaskofu kwa ajili ya huduma ya wakfu na maisha ya kitawa.

Zana hizi zinakusudia kutolewa kwa kila mwamini ile fursa ya wakati wa maombi, ili kusikiliza, kusoma masomo na kutafakari Neno la Mungu kwa muktadha wa miito. Ndni ya mwongozo huo pia kuna pendekezo la kusali Rosari kwa ajili ya miito na kufanya mkesha wa kuombea miito, ikiwa ni pamoja na tathmini ya ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko wa Siku ya kuombea miito duniani wa mwaka huu. Ni toleo la 58 ambalo liliadhimishwa mnamo tarehe 25 Aprili iliyopita katika Dominika ya IV ya Pasaka, ambapo siku hiyo iligusia tema ya Mtakatifu Yosefu: “ndoto ya miito”. Uchaguzi ambao sio wa bahati mbaya, kwa kufikiria kuwa hadi tarehe 8 Desemba tumo ndani ya mchakato wa Mwaka wa Mtakatifu Yosefu, uliotangazwa na Baba Mtakatifu katika kufanya kumbu kumbu ya miaka 150 tangu Mchumba wa Mama Maria kuwa msimamizi wa Kanisa la Ulimwenguni.  

Ikumbukwe kuwa Mwezi wa kuombea miito nchini Brazil ulianzishwa mnamo 1981 wakati wa Mkutano Mkuu wa XIX wa Baraza la Maaskofu nchini humo. Lengo la kuanzisha mwezi huo ni kuwafanya jumuiya ili daima wawe na uelewa wa uwajibikaji wao katika mchakato wa mafunzo ya miito.

04 August 2021, 14:20