Tafuta

Sudan Kusini Askofu Eduardo Hiiboro Kussala akitembelea jimbo Sudan Kusini Askofu Eduardo Hiiboro Kussala akitembelea jimbo 

Sudan Kusini:Ndoto za waamini za kutaka kuwa na Kanisa la matofali zimetimizwa

Ndoto za waamini na wateswa zimeanza kuonekana baada ya kujenga makanisa yao wenyewe kwa matofali na kuondokana na vikanisa vya mbavu za mbwa na nyasi huko Naadi karibu na mpaka wa Sudan Kusini na Jamhuri ya idemokrasia ya Congo na Uganda.Amesema hayo mmisionari mmoja aliyefika huko miaka mitatu iliyopita.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Padre Christopher Hartley Sartorius, akizungumza na Shirika la Habari za Kisimisionari Fides kutoa ushuhuda wa utume wake nchini Sudan Kusini amesema “Nilipofika Sudan Kusini, katika utume wa kimisionari huko Naadi mahali nilipo karibu na mpaka wa Sudan Kusini na Jamhuri ya idemokrasia ya Congo na Uganda kulikuwa na Kanisa moja lililotengenezwa kwa udongo tu na limeharibiwa na waasi wa kislam. Na vikanisa vingine vidogo vyote vilikuwa vimetengenezwa kwa majani na matawi ya miti tu”.

Padre Christopher amesema kuwa jambo la kwanza alipofika kwamba: “Padre tunataka Kanisa la matofali, kwani bila Kanisa tuko kama wanyama”. Tangu wakati huo, uhamasisho kwa waamini ulikuwa katika jumuiya tofauti ili kutengeneza matofari yao kwa mikono yao wenyewe na zaidi ilikuwa waamini wenyewe kutoa zawadi ya ardhi kwa ajili ya kutengeneza nyumba ya Bwana. Matofari baada ya matofari, ndoto za milenia ya waamini wa watu na mateso yao zimeweza kuonekana, kwa mijibu wa mmisionari huyo aliyefika huko Naadi hivi karibuni, miaka mitatu iliyopita yaani kunako mwaka 2019. Makanisa mawili ya Andari na Baragu katika utume wa kimisionari wa Naadi kwa ujumla yamekamilika; ni makubwa sana, wanafikia waamini karibu 700 katika makanisa hayo. Kwa mujibu wa Padre Christopher amesimulia kuwa hata hivyo majengo haya ni kiini cha maisha ya watu na yanawakilisha ahadi; ni urithi wa imani ya Kanisa kuelekea mji wao, amefafanua.

Padre Christopher amesema: “Kristo yuko hapa, Kanisa liko hapa, Askofu na mchungaji wako hapa na hawaendi mbali, kwa lolote lile liwalo. Sina jinsi ya kuweza kueleza kwa maneno rahisi kutokana na hisia nzuri za watu walipoingia kwa mara ya kwanza katika Kanisa. Licha ya kuwa katika nchi kumeanza kipindi cha mvua, lakini mvua inawanyeshea waamini wanaokuja na ambao wanataka kuingia ndani ya Kanisa jipya hata kama bado linahitaji mambo mengine ya kumalizia vizuri, kwa mfano madirisha bado hayajafika kutoka Kampala” amesisitiza Padre.

Akifafanua zaidi Padre Christopher amesema “mabenchi ya Kanisa bado na lazima yatengenezwe kwenye kiwanda. Na zaidi zinaandaliwa picha takatifu kutoka Uhispania ili kuweza kuzibandika kwenye ubao wa miti mahalia, na baadaye zitatundikwa Kanisani. Waamini wa vijijini hivi katika nyakati zilizopita walikuwa wanasubiri kuwa na Kanisa moja ambalo walikuwa wanataka wenyewe.  Kwa upande wao hawakujali hali halisi ya kukaa katika nyumba duni au kama maji yalikuwa mbali au kutembea maili nyingi hadi kwenye nyumba zao, Wao walikuwa wanataka kuwa na Kanisa lao wenyewe” amehitimimisha.

30 July 2021, 15:18