Bendera za Umoja wa Ulaya. Bendera za Umoja wa Ulaya. 

Kard.Hollerich:Katika janga Ulaya imejionesha umoja wao

Rais wa Tume ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Jumuiya ya Ulaya (Comece) amesisitiza sababu za siku kuu ya Ulaya katika mfululizo wa mwaka wa pili wa janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19. Katika kipindi cha dharura ya kiafya,kumegunduliwa mshikamano ambao haukuwa unajulikana kwa mwaka mmoja uliopita.

Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Ilikuwa ni tarehe 9 Mei 1950, ambayo ni tarehe ya kihistoria ya Robert Schuman, ambaye alipendekeza hatua ya kwanza kuelekea umoja wa Ulaya na kuanzishwa kwa Jumuiya ya Makaa ya Mawe na Chuma, kiongozi huyo wa serikali ya Ufaransa hasingewaza kufikiria kwamba matakwa mengi aliyoorodhesha, au hata kutarajia, yangetimizwa kidogo kidogo hadi miaka71 baadaye, kwa bahati mbaya siku kuu imekuwa ndani ya mgogoro wa janga ambao umeikumba Ulaya na dunia nzima kwa zaidi ya mwaka mmoja. Katika siku kuu ya Ulaya 2021, Kardinali Jean Claude Hollerich, Rais wa Tume ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Jumuiya ya Ulaya(Comece) akizungumza na Vatican news, kuhusu siku hii, amesisitiza jinsi ambavyo katika mateso ya janga, Ulaya imeweza kugunda kuwa kweli jumuiya kwa ajili ya kufikia lengo msingi. Awali ya yote kuridhia chanjo. walakini Ulaya haipaswi kusahau misingi ya mshikamano, uliyoundwa na Umoja ambao unapendekeza wajibu wa kusaidia Nchi zilizoko kwenye matatizo.

Na zaidi katika siku kuu hii, ambayo kwa mara nyingine tena mwaka huu ni katikati ya janga, Bunge, Baraza na Tume ya Comece wamezindua pendekezo la Mikutano ambayo kwa ratiba mbali mbali kuanzia tarehe 9 Mei zimeanza kufanyika, kwa nia ya kutaka kusikiliza sauti ya raia. Hasa vijana na kuwaruhusu wao wajieleza kuhusu wakati ujao wa Bara la kizamani kwa njia ya mfululizo wa majadiliano na mijadala. Kardinali amethibitisha kwamba sasa Ulaya wanajua mateso, kwa sababu wamefanya uzoefu. Katika hatua ya kwanza ya janga, Ulaya haukuwapo. Kulikuwa na serikali za mataifa ambazo zilikuwa zinatenda lakini bila kuwa na Ulaya yenyewe, ameakazia.

Hali hii imebadailika, kwa sababu wana msaada wa kiuchumi ambao ni kwa ushirikiano kati ya madaktari. Wameweza kushirikiana kwa ajili ya chanjo dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona, au Covid-19. Ulaya sasa ipo. Kardinali anelezea furaha yake kwa sababu, wameteseka wote na anafikiria hasa Italia ambayo imeteseka sana hasa akitazama takwimu zake zinazo karibia na zile ya Uingereza, ambao walianza wamechelewa kukabiliana na janga hili. Hii inaumiza amesema, kwa maana anafahamu Italia, amesomea Italia na anaipenda na hali hii inasikitisha sana na ni matarajio yake kuwa msada wa Umoja wa Ulaya unaweza kweli kuwapa msukumo mpya Italia kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi. Ni matarajio yake kwamba hata wao waliopata msaada, wasikunje mikono yao, kwa kulimbikiza, badala yake kutambua kushirikisha na nchi ambazo ni maskini, na ambazo sasa zipo katikati ya janga la covid. Kwa maana nyingine ni kuwa na roho ya mshikamano, roho ya msaada, mshikamano hata katika ugawaji sawa wa chanjo, kwa sababu janga haliwezi kushindwa tu katika bara moja. Kinachohitaji ni ulimwengu mzima unapaswa ushinde. Na hiyo ndiyo changamoto kubwa ambayo ipo mbele ya wote ili kukabiliana nayo.

Akiendelea kufafanua zaidi juu ya kile ambacho lazima kifanyike ili kushinda utaifa amesisitiza ni jinsi gani wameona kuwa jambo la kuwa pamoja kama Ulaya linafanya kazi. Kwa hakika wanafurahia kila nchi binafsi. Na kutokana na uzoefu wake wa kuishi nje ya Ulaya anaposikia nyimbo mbali mbali za mataifa, hata wimbo wa Taifa la Italia, anahisi kuwa kidogo Mwitaliano na kama hata mwana Ulaya. Hili ni jambo zuri lakini sasa, lazima kufikiria tena waathiriwa zaidi. Janga na si tu mgogoro wa kiafya, lakini hata majanga ya jamii nzima. Kuna aina nyingi za umaskini, kuna watu wengi ambao hawajuhi namna ya kupeleka mbele maisha hayo binafsi.

Kwa maana hiyo lazima wajionesha zaidi katika mshikamano wao kama wana Ulaya. Nchi tajiri lazima zijionesha mshikamano wao kwa nchi maskini. Aidha amefikiria kuwa wanazungumzia Jumuiya ya Ulaya, hiyo inaonesha tayari kuwa muhimu sana.  Wamefanya hatua moja mbele kufikia pwani, na lazima hata chanuzi hizi ziendelee na ambazo haziwezi kufanya Ulaya ya wakubwa, ya kifedha na kiuchumi. Lazima kufanya hata Ulaya ya watu na kwa maana hiyo lazima kutazama masuala ya kijamii.

Kwa kuhitimisha amezungumzia juu ya kampeni ya mikutano ambayo inazingatia kuomba raia wake waone Muungano wao.  Kardinali amesisitiza jinsi ambavyo ni fursa hata kwa wakristo. Kujionesha ushiriki wa mazungumzo makubwa hayo kwa sababu daima kumekuwa na ukosoaji kwamba Jumuiya ya Ulaya iko mbali na watu hasa katika masuala ya kiakili. Sasa wote wanaalikwa kutoa majibu ya maoni ya viongozi ambao  hawawezi kuingilia mijadala hiyo. Kardinali ameonesha upendeleo wake mkubwa kwa moyo kwamba wakristo, wakatoliki na wengine waweze kujionesha. Waingieli katika mjadala huo ili kufanya Ulaya, ya Muungano na angalau kidogo ya kweli ya watu.

10 May 2021, 19:20