2019.11.14 Wakati wa uwakilishi wa Barua ya Utambulisho wa Bwana Martin Pascal Tine Balozi wa Senegal  jijini Vatican 2019.11.14 Wakati wa uwakilishi wa Barua ya Utambulisho wa Bwana Martin Pascal Tine Balozi wa Senegal jijini Vatican 

Senegal:Mfano wa mazungumzo ya kidini na nuru ya Hati ya Abu dhabi!

Matendo ya dhatijuu ya kutangazwa Hati ya Udugu wa Kibinadamu,mazungumzo ya waislamu na wakristo na utamaduni wa amani nchini Senegal,ndiyo mada iliyozungumzwa tarehe 11 Mei 2021 katika mkutano ulioandaliwa na Ubalozi wa Senagal,jijini Vatican pamoja na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio.Sura ya waasisi wakristo wa Afrika:Sédar Senghor,Nyerere,Tanzania na Houphoet-Boigny,Ivory Coast.

Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ujenzi wa nchi ya pamoja umekuwapo daima nchini Senegal katika maono ambayo yaliunganisha, tangu mwanzo wa uhuru wao kutoka kwa ukoloni wa kifaransa, dini zote. Na ni katika Nchi ambayo sehemu kubwa ya wakazi ni wa imani ya Kiislam na sehemu ndogo tu ambayo unajumuisha wakristo na dini nyingine za kimila. Mazungumzo ya kidini yamekuwa ni muhimu sana hadi leo hii kama utamaduni wa nguvu ambao umekita mizizi yake  kwa mtu maarufu sana kama vile Léopold Sédar Senghor, mwanasiasa na Rais wa kwanza nchini Senegal. Baada ya ukoloni wa kifaransa, mkristo huyo alichagulikwa kwa kura na sehemu kubwa ya raia wake, wakiwemo waislamu na ambaye kutokana na  ujasiri wa udugu wa kuishi na si tu katika kushabikiwa, lakini ambaye hata leo hii, amekuwa katika vinasaba vya watu wa Senegal. Padre Angelo Romano, mtaalam wa masuala ya Nchi za Afrika, kama mwanajumuiya ya Mtakatifu Egidio na mwandaaji wa tukio la Mkutano akishirikiana na Balozi wa Senegal akiwakilisha nchi yake  jijini Vatican ameeleza katika mahojiano na Vatican News, kuhusiana na umuhimu ya tukio hili katika fursa ya furaha kwa ajili ya kutafakari mada ya Hati ya Udugu wa Kibinadamu na kwa ujumla kwa ajili ya kutafakari umuhimu wa mazungumzo ya kidini  ili kujenga amani na ambapo wameshiriki hata sehemu ya watu walio mstari wa mbele wa Hati ya Abu Dhabi, Kardinali  Miguel Angel Ayuso, Rais wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini na Mohamed Abdel Salam, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Udugu wa Kibinadamu.

Changamoto ya Senegal na Hati ya pamoja kuhusu Udugu

Hati ya Abu Dhabi inasaidia na kuzindua kazi ya pamoja kati ya wakristo na waislamu kwa ajili ya wema wa pamoja wa nchi ambayo mbele yake tayari ina changamoto, ameeleza Padre Angelo, kwa mfano ile ya maendeleo endelevu, hadi ile ya vijana kizazi kilichopo ndani ya jamii hiyo, na ni changamoto ambazo waamini wanapaswa kukabiliana nazo kwa pamoja. Hata hivyo ni miezi miwili tu iliyopita ambapo Nchi ilijikuta inakabiliana na hali ya ghasia  ya nguvu, wakati wa mivutano mikubwa iliyotokana na kukamata kwa kiongozi mpinzani lakini pia  hata kusasababishwa na hali halisi ngumu ya kiuchumi, iliyoongezwa  makali ya madhara ya janga la Covidi-19, na ukosefu wa furaha kwa vijana.  Kipindi hiki kwa wastani kigumu ambacho kiliona hata vifo vya baadhi ya vijana, na kuingiliwa shukrani kwa viongozi wa kidini: sehemu moja katoliki ya  Baraza la Maaskofu  Nchi humo, vile vile kiongozi  mkuu wa Muridi, wa chama muhimu cha Waislamu na hata viongozi wengine wakuu wa kiislamu nchini Senegal.

Senegal na uhusiano na Mapapa

Padre Romano vile ameelezea hata sura muhimu kama ishara ya mazungumzo kati ya wasilamu na wakristo nchini Senegal ambayo kwa hakika amesema ni ile ya Kardinali Hyachinthe Thiandoum, aliyekuwa Askofu Mkuu wa  Dakar, na mmoja wa makardinali wa kwanza wa Afrika, na ambaye mkutano huo vile vile wamejikita kutazama sura yake kwa kina, na mchana pia wakatazama sura ya ulimwengu mzima katika matendo ya dhati ya Mfuko wa Yohane Paulo II kwa ajili ya Sahel. Ishara ya kuhamasisha ya Yohane Paulo II ilikuwa inaelekeza kwa dini zote. Vile vile  Papa Yohane Paulo II alipofika nchini Senegal, mnamo mwaka 1992, alisema kwamba anakwenda kukutana na watu ambao wanaamini dini mbali mbali, lakini wanaotambua kukubali kupokea tofauti zake na kuwa na imani katika mazungumzo, na zaidi alisisitizia kupendezwa kimataifa kwa ajili ya upendo wa kuishi pamoja kwa maelewano kati ya watu wa imani tofauti.  Hii ni historia ndefu ambayo inaunganisha nchi ya Senegal na mapapa kwa mujibu wa maelezo ya Padre Romano, na tena kwamba, Papa Yohane XXIII alimpokea Senghor, kabla ya kuchaguliwa kuwa rais, akiwa pamoja na waandishi wengine wa Afrika katika fursa ya Mkutano wa II wa Wasanii na waandishi wa Afrika, jijini Roma mnamo mwaka 1959.

Viongozi wakristo: Nyerere, Tanzania na Houphoet-Boigny, Ivory Coast

Na zaidi Senghor, alikuwa ni mmoja wa waandishi wa vitabu ambao walikuwa mwamenukuliwa sana na Papa Paulo VI katika tafakari zake kuhusu Afrika na alikuwa ndiyo mmojawapo wa marais waliopokelewa mara nyingi yaani mara nne na Papa, amebainisha  Padre Romano. Rais Seghor, na kama alivyokuwa Rais Julius Nyerere wa Tanzania na  Félix Houphoet-Boigny wa Ivory Coast walikuwa ni viongozi wakristo ambao katika kipindi cha kwanza vya kujinyakulia uhuru wao, walitambua vema kutoa utambulisho wa nchi  zao kwa namna ya kuishi pamoja kwa amani kati ya wakristo na waislamu  na kuwa na uwabikaji wa nguvu uliosaidiwa na Mapapa na  uhusiano ambao kadiri ya miaka kuongezeka umeweza kukua, na ambao kwa hakika unawakilisha mfano wa furaha ya uhusiano, amehitimisha Padre Romano.

12 May 2021, 14:06