Maaskofu nchini Kenya Maaskofu nchini Kenya  

Maaskofu nchini Kenya wameomba amani kwa ajili ya nchi,usalama na mafanikio

Katika ujumbe wa Baraza la Maaskofu nchini Kenya(Kccb)uliotangazwa tarehe 27 Mei 2021,baada ya kumaliza mkutano wao wa kawaida wameiombea nchi yao iwe ya amani, usalama na mafaniko.Hata hivyo katika mkutano wao masuala ya janga la covid-19, uchaguzi mkuu wa 2022,usalama,mabadiliko ya tabianchi na dharura ya vyakula ni masuala yaliyojadiliwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kati ya changamoto ambazo Maaskofu zinatakiwa kukabiliwa  kwa dharura kwa sababu ya wema wa taifa, ni kuanzia na janga la covid-19, uchaguzi mkuu wa 2022, usalama, mabadiliko ya tabianchi na dharura ya vyakula. Haya yanaonekana katika taarifa yao ya Mwisho wa Baraza la Maaskofu nchini Kenya (Kccb) mara baada ya kufanya Mkutano wao wa kawaida, iliyotangazwa tarehe 27 Mei 2021. Kuhusu hoja ya kwanza, maaskofu nchini Kenya wameelezea masikitiko yao na maumivu yao kutokana na kwamba serikali imeanzisha, kama hatua ya kupambana na maambukizi, kwa kufungwa kwa makanisa, lakini sio ile ya maeneo mengine ya umma, kama vile masoko.

Hatua hivyo pia maaskofu wanaomba njia ya mazungumzo katika kushughulikia shida na wanawaomba waamini waendelee kuzingatia itifaki za kiafya zinazotolewa, kwa sababu wanasema  ni muhimu kuzingatia thamani ya maisha na sadaka kama fursa yoyote ambayo inaweza kuwa chanzo cha kueneza au kupungua kwa virusi. Kwa maana hiyo maaskofu wanahimiza serikali kuhakikisha upatikanaji wa chanjo kwa  ajili ya idadi ya watu na wafanye hivyo kwa njia ya uwazi na inayowajibika iwezekanavyo, kwa sababu kilicho hatarini ni maisha ya raia wengi.

Kwa upande mwingine, kuhusu uchaguzi wa mwaka ujao, Baraza la Maaskofu nchini Kenya(Kccb) wamesisitiza kuwa lazima ufanyike kama inavyotakiwa na Katiba na kwamba hakuna jaribio la kuahirisha siku nyingine ya baadaye, bali siku hiyo izingatiwe, ili kuhakikisha mchakato wa kidemokrasia na unaojumuisha wote, na unaozingatia sheria na mazungumzo nchini kote. Baraza la Maaskofu pia wanaonesha wasiwasi juu ya hali mbaya ya ukosefu wa usalama katika eneo hilo, hasa katika eneo la Baringo, liliooko katika Jimbo katoliki la Nakuru. Hali ya machafuko katika eneo hilo lazima ikomeshwe, maaskofu wanasema, wakiongeza kuwa serikali ina jukumu la kutoa usalama kwa raia wake wote na kwamba Wakenya wote wana jukumu la kuhamasisha na kudumisha amani na kuepuka vitendo vyote vya chuki, ubaguzi na vurugu.

Kwa ujumla, katika taifa kuna ongezeko la vurugu pia katika familia, kati ya marafiki, na shuleni maaskofu wamebainisha na wamelaani mauaji, utekaji nyara, na miili iliyotelekezwa katika misitu na mito, yote hayo ni matendo yanayochukiza na ambayo yanaleta hatari ya kuendeleza utamaduni wa kutovumiliana na kifo wamebainisha. Kufuatia na hilo, ndipo wito kutoka kwa Maaskofu wa kuhamasisha utamaduni wa mazungumzo na kurejesha njia za jadi za kusuluhisha mizozo hiyo au pasikosekane njia kama hizo za kutumia sheria za kutuliza mizozo.

Kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa na dharura inayosababishwa na chakula, maaskofu wa kenye wanaomba mtendaji kushughulikia suala la ukame kwa kutoa msaada wa muda mfupi na wa muda mrefu kwa watu walioathiriwa nao ili kupunguza kukumbatia utamaduni wa hatua ya matendo inayotarajiwa ili  kukabili mgogoro huo. Na hatimaye Baraza hili limehimiza watu wote ili wasipoteze tumaini na wafanye kazi pamoja na jukumu la mtu mmoja mmoja na la pamoja, kwa amani kwa ajili ya Kenya salama na mafanikio.

29 May 2021, 15:22