Mashambulizi ya kila mara maeneo ya Butembo Beni, Congo DRC. Mashambulizi ya kila mara maeneo ya Butembo Beni, Congo DRC. 

Congo Drc:Askofu Paluku atoa wito wa amani

Tangu tangu mwanzo wa 2021,wimbi la mashambulio ya vikundi vyenye silaha na mapigano baina ya jumuiya yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 300 na kuchochea hali ya taifa la DRC,ambalo tayari limepondwa na mzozo mkubwa wa kibinadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kufanya kila linalowezekana ili kurejesha amani na mamlaka ya serikali katika mkoa wa mashariki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ndivyo Askofu wa jimbo la Butembo-Beni, Melchisédech Sikuli Paluku, anaomba mbele ya hali ya kuzingirwa iliyo tangazwa katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri. Imewekwa na Rais Félix Tshisekedi na kuanza kutumika tangu tarehe  6 Mei kwa muda wa siku 30, “hali ya kuzingirwa" iliamuliwa kufuatia na kuongezeka kwa vurugu katika maeneo yaliyoko mashariki mwa nchi.

Tangu mwanzo wa 2021, kiukweli  wimbi la mashambulio ya vikundi vyenye silaha na mapigano baina ya jumuiya yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 300, na kuchochea hali ya taifa hilo, ambalo tayari limepondwa na mzozo mkubwa wa kibinadamu. Kwa sababu hiyo katika tamko la kichungaji lililotangazwa na Redio Okapi, Askofu Sikuli Paluku anawataka watu watulie na kuwa macho, akialika viongozi wa serikali kurudisha amani.

Utulivu na busara zilikuwa, fadhila zilizo kumbukwa na kiongozi wa dini ambaye anaongeza kusema: “Mbele ya kukabiliwa na hali ya kushangaza na mauaji ya mara kwa mara ambayo tunapata katika eneo hilo, kishawishi cha kuvunjika moyo na kukata tamaa ni kubwa”. Kwa hiyo askofu anawaalika waamini kutazama mfano wa Mtakatifu Joseph, hasa katika mwaka huu uliowekwa wakfu kwa ajili yake katika kusherehekea miaka 150 ya kutangazwa kwake kama Mlezi wa Kanisa zima la ulimwengu. Askofu amesema, “tujifunze kutozidiwa na matukio hayo au kudanganywa katika hali halisi iliyopo” ameelezea.

Kwa nguvu, pia ametoa mwaliko wa Rais Tshisekedi ambaye, kama mdhamini wa taasisi za Jamhuri, ana jukumu la kufanya kila kitu kwa uwezo wake ili kuhakikisha kuwa mamlaka ya Serikali, amani na usalama wa raia hakika inarejeshwa mashariki mwa nchi . Sawa na hiyo kutoka moyoni mwake  ni wito wa askofu ni kwa wale wote ambao, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, wanahusika katika mikasa  inayowaathiri kaka na dada zao. “ Muwe na busara”. Hatimaye Askofu Sikuli Paluku ameelezea ukaribu na mshikamano wake kwa waazi wote wa Kivu Kaskazini na Ituri, haswa wale wa Mbau, Oicha, Mayi-Moya, Erengiti, Kainama, Mangina, waathiriwa wa mauaji.

Kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya UNICEF, karibu ukiukwaji mkubwa wa watu  175 ulifanywa huko Ituri pekee, tangu  Januari hadi Aprili 2021, ikiwa ni pamoja na kuajiri watoto katika vikundi vyenye silaha, mauaji na ukeketaji wa watoto, unyanyasaji wa kijinsia na mashambulizi kwa shule na hospitali. Inakadiriwa pia kuwa katika Jimbo hilo kuna zaidi ya wakimbizi milioni 1.6 kati ya idadi ya watu milioni 5.7, wakati kuna watu milioni 2.8 wanaohitaji msaada wa dharura na zaidi ya watoto elfu 100 chini ya miaka 5. wanaougua ugonjwa wa papo hapo na utapiamlo wa kukithiri.

10 May 2021, 19:29