Maaskofu nchini Benin wato wito wa kuthibiti uhalifu wa kuua Albino na kafara Maaskofu nchini Benin wato wito wa kuthibiti uhalifu wa kuua Albino na kafara  

Benin:Wito wa maaskofu dhidi ya ushirikina na mauaji ya albino

Katika tamko la kumaliza kazi yao ya mkutano wa maaskofu wa Benin wanalaani kuibuka tena kwa uhalifu wa kimila na kafara za wanadamu,ambazo wakati mwingine hufanyika katika sehemu nyingine za taifa lao.Wametoa wito wa kuheshimu hadhi ya maisha ya binadamu ambaye ni wa Mungu na ambaye mwanadamu atawajibika juu yake siku moja.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kuheshima hadhi ya utu wa binadamu, hasa mbele ya kuongezeka kwa uhalifu wa kimila au ushirikina nchini ndiyo wito uliozinduliwa na na Baraza la Maaskofu wa Benin (CEB), mwishoni mwa Mkutano wao, uliofanyika katika siku za hivi karibuni. Katika taifa, kiukweli, mauaji yanaongezeka hasa ya watu albino, kwasababu ya kuenea kwa imani potofu au kishirikina kuwa viungo vyao vinaweza kusaidia matibabu ya magonjwa kadhaa.

Katika tamko la kumaliza kazi yao ya mkutano huo, maaskofu wanalaani kuibuka tena kwa uhalifu wa kimila na kafara za wanadamu, ambazo wakati mwingine hufanyika katika sehemu nyingine za taifa lao.  Kufuatana na hiyo ndipo wametoa wito wa kuheshimu hadhi ya maisha ya binadamu ambaye ni wa Mungu na ambaye mwanadamu atawajibika juu yake siku moja.  Wamewahimiza watu wajiepushe kujichukulia haki wenyewe na kuwaalika kuwa na uongofu. Wale wanaotenda uhalifu wa kimila watubu juu ya matendo yao maovu na watafute huruma ya Mungu.

Katika barua hiyo, iliyosainiwa na rais wa  maaskofu Katoliki wa Benin (CEB), Askofu Victor Agbanou, pia  wanaelezea wasiwasi na hisia za kuchanganyikiwa kwa mgawanyiko kati ya wanasiasa, kukamatwa mara nyingi, hali ya kutokuaminiana na hofu ambayo inatawala katika mioyo ya idadi ya watu. Wakuu hao baadaye wamezindua wito wa ujenzi wa mpangilio mpya wa kuishi kwa kuzingatia mchango wa wote, katika mazungumzo, uvumilivu na upatanisho kulingana na kauli mbiu ya Nchi: undugu, haki na kazi. Neno udugu, ambalo ni sehemu ya kauli mbiu yao wamesisitiza kuwa inaalika kuishi pamoja kama ndugu, licha ya tofauti halali walizo nazi. Ni juu yao kuonesha ulimwengu wote njia ya kuishi udugu halisi katika haki, kwa kuzingatia umuhimu wa familia na kazi.

Miongoni mwa mada nyingine zilizochunguzwa na Mkutano Mkuu, ni masuala yanayohusiana na seminari na nyumba za malezi kwa makuhani wa baadaye. Mkutano pia ulimkaribisha Balozi moya wa Kitume nchini, Askofu Mkuu Mark Gerard Miles, ambaye Papa alimteua mezi Februari mwaka huu. Hatimaye wameomba wingi wa neema za kimungu katika huduma yenye kuzaa matunda ya kitume katika huduma ya watu wa Mungu barani Afrika. Na maaskofu wanamalizia na sala kwa Mungu, ili aendelee kubariki na kulinda Benin.

26 May 2021, 15:26