Maandalizi ya chanjo Maandalizi ya chanjo 

Barua ya viongozi 145 wa kidini kwa Mataifa na kampuni za dawa!

Chanjo ni wemwa wa pamoja.Ni ulazima wa kimaadili kuwafikia watu wote.Ndiyo sauti moja katika barua ya viongozi 145 wa kidini kwa Mataifa na makampuni ya kutengeneza madawa."Kama viongozi wa dini,tunaunganisha sauti zetu ili chanjo itolewe kwa watu wote kama faida ya pamoja ya ulimwenguni.Hii ndiyo njia pekee ya kumaliza janga”.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Viongozi 145 wa dini kutoka ulimwenguni kote, Wakristo, Waislamu, Wayahudi na Wabudha, wameungaisha sauti zao kwa pamoja na kutuma barua kwa Mataifa na kampuni za dawa ili kuomba hupatikanaji wa chanjo ulimwenguni kote kwa watu wote. Katika barua hiyo wanaandika “Tunatoa wito kwa viongozi wote kukataa utaifa wa chanjo na kukubali kujitoa katika usawa wa ulimwengu. Kama viongozi wa dini, tunaunganisha sauti zetu ili  chanjo itolewe kwa watu wote kama faida ya pamoja ya  ulimwenguni. Hii ndiyo njia pekee ya kumaliza janga”.

Kila mmoja atakuwa salama ikiwa wote wanakuwa salama

Miongoni mwa waliosaini barua hiyo ni Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamami ya Binadamu,  Wafransiskani wa Assisi, Rowan Williams, aliyekuwa askofu mkuu wa zamani wa Canterbury, Martin Junge, katibu mkuu wa Shirikisho la Kilutheri Ulimwengu; Thabo Makgoba, Askofu Mkuu wa Kianglikana wa Cape Town; Jim Winkler, rais wa Baraza la Kitaifa la Makanisa la Marekani. Kwa mujibu wa Gazeti la Guardian, hata  Dalai Lama pia ameunga mkono kampeni hiyo. Katikati ya dharura ya huko India, viongozi wa kidini wanakumbuka kutegemeana na majukumu ya kujaliana. “Kila mmoja wetu anaweza kuwa salama tu ikiwa wote tuko salama. Ikiwa sehemu moja ya ulimwengu imesalia katika janga, sehemu zote za ulimwengu bado zitawekwa  hatari inayozidi ”.

Dini zinatelemka katika uwanja wa kuomba ufikiaji wa chanjo wote

Viongozi wa dini wanaandika kuwa “ufikiaji wa watu kwa chanjo za kuokoa maisha dhidi ya  Covid-19  hauwezi kutegemea utajiri wa watu, hadhi au utaifa. Hatuwezi kukataa majukumu yetu kwa dada na kaka zetu, kwa kukifikiria kwamba soko linaweza kusuluhisha shida au kujifanya sisi wenyewe kuwa hatuna jukumu kwa wengine katika ubinadamu wetu wa kawaida wa pamoja. Kila mtu ni wa thamani. Tuna wajibu wa kimaadili kufikia kila mtu, katika kila nchi”. Kinachotia wasiwasi ni tofauti kati ya nchi tajiri ambazo zina uwezo wa kupata dozi zao na nchi nyingi za kipato cha chini na cha kati ambapo chanjo zinaanza kusambazwa sasa".

Kasi iliyopo sasa yaweza kufikisha hadi 2024 ambapo ni hatari

Kwa kasi ya sasa ya uzalishaji na usambazaji wa chanjo, watu katika sehemu kubwa ya ulimwengu hawawezi kupata chanjo hadi labda 2024 na athari kwa watu maskini zaidi, familia na jamii zitakuwa mbaya. Kwa maana hiyo wito kwa viongozi wa serikali, asasi za kiraia na sekta binafsi kuongeza na kuharakisha uzalishaji wa chanjo ili kuwe na kipimo cha kutosha kwa kila mtu ulimwenguni. Wito huo ni sehemu ya hatua ya Muungano wa Chanjo ya Watu, umoja wa mashirika ambayo yanaendeleza chanjo ya watu na vile vile kutolewa kwa haki miliki ya hati miliki ya chanjo za kupambana na Covid-19.

01 May 2021, 10:29