Ubuntu ni utamaduni wa Afrika chini ya Jangwa la Sahara Ubuntu ni utamaduni wa Afrika chini ya Jangwa la Sahara  

Afrika ni bara kijana,tajiri la rasilimali na fursa!

“Afrika:Wasiojulikana.Rasilimali na Faida.Ni kitabu ambacho ni tunda la Kazi ya utafiki wa ya Shule ya Sinderesi ya Kituo cha Alberto Hurtado kilicho wasilishwa tarehe 17 Mei 2021 katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana.Maandishi, kuanzia kanuni ya Ubuntu na kwa mantiki inayojumuisha Waraka wa Fratelli tutti, yanaangazia mafanikio na rasilimali zilizopo katika bara la Afrika,katika uwanja wa siasa,uchumi,utamaduni na katika nyanja ya kidini na Kanisa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kuzungumiz Afrika, katika mtanzo wa kitab, jinis ambazo bara na rasiliamizia na faifa zake. Ndiyo kutika kuelezea katika kitabu kilichoewa jina la “Afrika. Rasilimali na faida”. Ni kitabu ambacho kinakusanya safu za michango ya wataalam wa sekta, bila kudharau matatizo na vikwazo vya Afrika, ambacho pia kinataka kuanza na maono tofauti, yaani ya Ubuntu, itikadi za tamaduni wa Afrika kwa pande zote za watu, kukabiliana na ubinafsi ambao unaharibu ulimwengu na kuunga mkono upatanisho na uelewano kati ya pande zinazogombana na ambazo zinatakiwa kuongozwa kutazama zaidi ya masilahi yao kwa ajili ya faida ya wote na kupata suluhisho kwa hali ya sasa yenye  mgogoro wa kiuchumi na mazingira. Kwa mujibu wa Monsinyo Samuele Sangari, mratibu wa Shule ya Sinderesi amesema hii ina maana ya kuzungumzia juu ya Afrika isiyojulikana, kwa sababu walitaka kuwasilisha kama bara la rasilimali na lenye mafanikio, badala ya kuliona tu kama lililopitiwa shida zake. Mtazamo wao  kwa upande mwingine, ulikuwa tofauti kabisa, kwa sababu  Afrika ni bara ni kijana, kwa sababu Afrika  kuna kiwango cha hali ya juu cha kuzaliwa na wastani wa umri ni mdogo sana na una rasilimali zake.

Monsinyo Samuele akijibu swali juu kukakabiliana na nadharia ya Ubuntu katika kitabu hicho  amesema: “Nadharia ya maadili ya Ubuntu inategemea falsafa ya Kiafrika, ambayo inapendekeza kutegemeana kama ubora wa ndani na sio kuonekana wa pili kwa utambulisho wa watu wa afrika binafsi. Ndani ya maono hayo ya kiikolojia, na ambayo ni karibu sana na yale yaliyopendekezwa na Baba Mtakatifu Francisko katika waraka wa ‘Fratelli tutti’, yaani ‘Wote ni Ndugu’, hali ya maadili ya Ubuntu, ambayo kwa kiukweli inamaanisha “Mimi ni kwa ajili ya fadhila ya ubinadamu wa wengine”, inatuambia kwamba kimsingi, ikiwa tutazama mzizi wa kina wa utamaduni wa Kiafrika, kuna hali hii ya ushirikiano na uwajibikaji wa pamoja katika kukabili changamoto yoyote maishani, hata kama utandawazi na athari  za tamaduni zetu za Magharibi zinapata  shida na majaribu  juu ya maono haya ya Kiafrika.

Aidha amesema kuwa kieleza juu ya matokeo ya maendeleo ya bara la Afrika kuhusiana na kanuni ya ubtntu amethibitisha kuwa katika utafiti wao, ambao uligusa maeneo tofauti ya bara, walitaka kuangalia ukweli kutoka katika maoni tofauti: ya kihistoria, kiutamaduni, kiuchumi, kisiasa, mazingira na afya, kisha wakazingatia nchi tofauti kwa kila eneo, na jinsi hii kanuni ya 'Ubuntu imewezesha kupelekea njia mpya. Kwa mfano, kutegemeana kijamii, ambayo imekuwa chachu ya kisheria katika katiba ya umoja ya Afrika Kusini na inaendelea kuwapo hata baada ya kipindi kikuu cha kihistoria cha Nelson Mandela.

Vile vile wameona jinsi kanuni hii ya uwajibikaji wa mtu mwingine inazalisha uhusiano mzuri  wa kidini katika Afrika Kaskazini, kama vile Senegal, uhusiano wa kuishi kati ya makabila na dini tofauti ambazo huenda zimetokana na mtazamo wa Ubuntu. wamejifunza shida nchini Kamerun na Congo zinazoendelea hivi sasa, kuwa na upungufu wa michakato ya hali hizi, ambazo tunaweza kuzielewa tu ikiwa zinaunganishwa na kanuni hii ya uwajibikaji wa pampoja kama utambulisho wa Kiafrika (Ubuntu). Na kiukweli, Mabaraza ya Maaskofu wa nchi hizi, kwa wakati huu, waatakiwa kuwa jasiri sana katika kuonesha njia hii, ili kupata suluhisho la amani, ustawi na kuishi kati ya watu, licha ya tofauti za kiutamaduni, kijamii na kidini.

21 May 2021, 09:35