Tafuta

Askofu Mkuu Nguyen Nang -wa Vietnam Askofu Mkuu Nguyen Nang -wa Vietnam 

Vietnam:Samehaneni,saidieni wagonjwa,walemavu na maskini!

Waamini wa jimbo kuu la wa Jimbo Kuu la Ho Chi Minh,wamehimizwa sana kusamehana mmoja na mwingine na kuwasaidia wagonjwa,walemavu na maskini kwa mfano wa Yesu katika fursa ya Dominika ya Huruma ya Mungu tarehe 11Aprili 2021.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Askofu Mkuu Joseph Nguyen Nang, wa Jimbo Kuu la  Ho Chi Minh C, tarehe 11 Aprili 2028 akiwa katika Kanisa la mama Yetu, wakati wa maadhimishp ya Dominika ya Huruma ya Mungu amewashauri waamini   kusamehana mmoja na mwingine, kusaidia wagonjwa, watu wenye ulemavu na wale wanaoisho kwa umaskini na hali mbaya zaidi. Akikumbuka jinsi ambavyo Mtakatifu Faustina alivyowaalika wakatoliki kuheshimu picha ya Huruma ya Mungu, kusali novena na rosari ya huruma ya Mungu amewaalika wakatoliki kushiriki mazoezi haya Aljamishi Jioni katika Kanisa Kuu na kila siki kufanya ukimya wa dakika moja kwa ajili ya kuwaombea wafu na wadhambi saa 9 alasimu hata bila kwenda Kanisani.

Akiendelea kueleza kwa mujibu wa Shirika la habari za Kanisa barani Asia amesema: “Wakati tunapougua, lazima kumwomba Mungu kwa sababu atuponesha na kutafuta haraka madaktari”, amesisitiza Askofu Mkuu Nang. Lakini pamoja na hayo si mara zote tunapokuwa tunasali tunapata kupona. Mungu anaweza kutuacha tuteseka kwa ajili ya kuunganisha na Yesu juu ya msalaba na kutoa mchango wetu katika Mpango wa wokovu”,vamebainisha Askofu Mkuu.

Askofu Mkuu Nang kwa maana hiyo amekumbusha kuwa wasisahau fumbo la msalaba kwa maana kwamba Yesu Mwana wa Mungu aliweza kufanya uzoefu wa mateso kabla ya ufufuko. “Hatuwezi kutokuwa na mateso, na kila tendo la kuheshimu Huruma ya Mungu si kwa ajili ya kupona, bali kwa ajili ya kukumbuka mateso ya Yesu na kuomba kupunguzwa na kubadilika kwako mwenyewe na kwa wengine”. Askofu Mkuu Nang, akiwaonya waamini dhidi ya kuamini katika miujiza ya kuponya kabla ya kuthibitishwa na Kanisa, amewataka Wavietnam kumwamini Mungu; "ambaye hutupatia utimilifu wa maisha hapa duniani na utimilifu wa maisha baada ya kifo”. Pia tarehe 11 Aprili 2021, Askofu Mkuu Joseph Nguyen Chi Linh alibariki sanamu kubwa ya Huruma ya Mungu na kikanisa cha  ibada ya Kuabudu Ekaristi katika Kanisa kuu la  Phu Hanh.

13 April 2021, 14:36